Nisaidieni Ndugu zangu

Kwetu Tunduru

Member
Feb 7, 2023
16
57
Wakuu habari!!!
Natumaini tuko poa sote,na kwa wale wapitao katika magumu Basi Mungu aweke rehma zake mambo yaweze kuwa mepesi.

Tuje kwenye mada,ndugu zangu Mimi ni baba wa familia ya watoto wawili na mke mmoja.
Nimeamua nije kwenu nahitaji msaada maana duuh!Hali inakoelekea naona mwanga unazidi kuwa hafifu,sielewi,mambo yangu
kiuchumi hayaeleweki kabisa.

Niko na familia ni mwaka wa tano Sasa na shughuli zangu Mimi nyingi si rasmi ni za kuunga unga(vibarua).yaani ile baba atoke ndio riziki ya mlo siku hiyo ipatikane.kiujumla kipato changu Ni kidogo Sana kutosheleza majukumu ya kifamilia,hata kuweka akiba na ikatulia nichangamoto Sana.

Nawaza na kuwazua,majibu Ni magumu,nitokako kugumu na niendako sielewi,madeni madogo mtaani ni mengi,Kodi ya nyumba hiyo nayo inatimiza miezi sita nadaiwa,napambana sioni pa kutokea😰😰.nikiiangalia familia daah!!

Ndugu zangu ni mengi ya kuongea lakini nafsi pia inauma zaidi.naomba mnisaidie kupata leseni ya udereva na cheti pia.hii Ni fani Niko nayo kwa miaka Sasa na ndio naijua.

Mwenyewe nimeshindwa kufanikisha sababu kipato changu hakitoshelezi kujikimu na akiba.unajiwekea inafika kiasi fulani jambo linatokea unatumia unarudi kuanza moja.

Ninaomba mnisaidie ndugu zangu.nigeuze ujuzi wangu huu kuwa ajira yangu tegemezi.

Niko tayari hata kwa makubaliano maalumu baada ya kupata leseni.pia sitahitaji pesa cash kama nasaidiwa,niwe mfuatiliaji tu wa zile process Basi Hadi kukamilisha leseni.

Mtanisamehe pia kwa uandishi wangu usioridhisha.
Mungu awabariki.

Nawasilisha.
 
Pole Sana! Ndio kawaida na ndio majukumu..

Ushauri: Jiunge na vyama wa wasifirishaji abiria eneo ulilopo na kuwa mvumilivu na maneno ya kijiweni..
 
Tuma namba inbox
 
Back
Top Bottom