Nipo njia panda wandugu

Umesema una mpango nae hivyo bado hajawa mke wako, akiwa mkeo unafikiri nini kitatokea? Unalazimisha kupendwa wewe wa wapi?!!! Hakupendi unamlazimisha, sasa subiri aje akumalize kabisa. Umepata uhakika kuwa kuna kijeba kina kuibia bado unavumilia, mwache aende wewe (huwa nachukia kumuona mwanaume mwenzangu analialia kisa mapenzi, wakati huko nje yuko mutoto muzuri anayesubiri fursa).
 
Mkuu fuatilia hiyo namba leo leo ikiwezekana mlazimishe kuipokea ukigundua anacheat achana naye kwq amani.

Ila kama sio hivyo mbembeleze tu atatulia.
Hawa watu sio wa kucheka Cheka nao saana.

Tabia ya kucheka na kuwaachia achia some time inazaa viburi

Yani mtu hataki kupokea simu!??? Ambayo unaisuspect?????

Anakufyonza???? Alafu unambembeleza

Ipo siku atakufyonza mbele ya watu wengine.

Mkishindwa kuishi kwa mipaka Bora kuanza upya kutafuta mwingine
 
Binafsi kama unauhakika namba ni ya mwanaume na umemwonya hataki kwangu naona achana naye... ila mengine jiongeze mwenyewe maana wew unayajua vizuri kuliko mimi.
nashukuru mkuu japo naumia sana kupoteza time yangu kwa kudhani nilikuwa kwenye mikono sahihi
 
Bro, kama ni mimi simu utapokea ukikataa nitaipokea mimi.

Halafu kwangu naona wanawake wengi wanaheshima hadi akufyonze utakuwa na shida. Japo viburi vipo.
 
mkuu sio mimi napenda kulialia ila ni moyo ndio uliona mahala salama kumbe ni kinyume
 
ni kweli mkuu
 
mkuu umepigilia msumari yaani ni mtu anayejiona malaika hapendi umkosoe hata kama unaona kabisa jambo fulani lina dosari ya moja kwa moja yeye huona unambishia na humuungi mkono
Mkuu ni heri tukaambiana ukweli ambao unaumiza kuliko kila siku tukaimbiana nyimbo za mapambio
 
Bro, kama ni mimi simu utapokea ukikataa nitaipokea mimi.

Halafu kwangu naona wanawake wengi wanaheshima hadi akufyonze utakuwa na shida. Japo viburi vipo.
inavyoonekana makuzi ya home kwao yamemuasiri kwa sababu anajijua yeye ni mzuri kitu ambacho ni kweli pia home kwao nadhani matusi ni jambo dogo sana
 
Mi nadhani kama unakiri umemvumilia vya kutosha na habadiliki basi ni busara pia ukamwambia maisha mema na uzuri anakiri kuwa anarudi kwao hivyo we cha msingi kumpa nauli nakuhakikisha amefika kwao.

Kumfyonza Mme au mke ni dharau kubwa sana kwa upande wa tamaduni zetu.

Ombi kwako kama umeweza kumpiga kibao kwa hasira basi ipo siku utafanya baya zaidi la kukuweka matatani na kujutia. Late her go nothing else.
 
Hiyo Namba iangalia kupitia huduma za kipesa utajua mmiliki usikute jirani yako au vijana wa nyumbani kwao unaowajua
 
huwezi sijawahi hata ile kumfinya ila nilijikuta nimemuwasha na pia nilichokosea toka mwanzo ni ile hali ya kudhani ipo siku nitambadilisha kuwa kwenye uelekeo sahihi jambo ambalo naona kabisa sasa hivi haliwezekani na pia kuna viashiria fulani mbeleni hata kama nitashupaza shingo nitakuwa nimesogeza mbele tu maumivu ila ni comparsary shida niliyonayo sasa hivi natokaje hapa nilipo ninavyoongea muda huu bado amelala
 
inavyoonekana makuzi ya home kwao yamemuasiri kwa sababu anajijua yeye ni mzuri kitu ambacho ni kweli pia home kwao nadhani matusi ni jambo dogo sana
Uzuri wake si kitu kama tabia Ni mbovu. Hivi vitu vinategemeana bro.

Kuwa makini saana usipoweza kurekebisha nidham ya huyo mrembo atakusumbua saana utakapo muoa

Watch up
 
Hiyo Namba iangalia kupitia huduma za kipesa utajua mmiliki usikute jirani yako au vijana wa nyumbani kwao unaowajua
nimeicheck hyo namba mpesa kiukweli simfahamu na pia si jirani nilitaka nidukue mawasiliano yake ila nashindwa maana ningeona kila kinachoingia na ningekuwa na ushahidi wa kutosha
 
Bro, kama ni mimi simu utapokea ukikataa nitaipokea mimi.

Halafu kwangu naona wanawake wengi wanaheshima hadi akufyonze utakuwa na shida. Japo viburi vipo.
Hiyo nafasi ya kukataa kupokea anaitoa wapi?????
 
Pole sana. Umeumizwa sana. Lakini tunza heshima ya kiume. Kama haujamtolea mahari ongea naye kuwa uko karibu kutoa mahari. Akikubali umepata muda wa kumchunguza zaidi.
Muoneshe upendo wa hali ya juu kipindi hiki unamchunguza, mtoe out ,Nk. Ukijiridhisha na mwenendo wake utakuwa psychologically prepared .
 
Uzuri wake si kitu kama tabia Ni mbovu. Hivi vitu vinategemeana bro.

Kuwa makini saana usipoweza kurekebisha nidham ya huyo mrembo atakusumbua saana utakapo muoa

Watch up
ni kweli mkuu nimeimba na kuimba ila huyu ni kufunzwa na walimwengu tu ndo hayo atayaelewa mimi ninachotaka ninatokaje kwenye hii situation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…