Nipo Afrika Kusini mwaka wa 6 huu binafsi maisha ya huku sijayaelewa

Aratif

Member
Aug 27, 2023
13
81
Habari zenu

Naomba nielezee kiufupi
Nikisema sejayaelewa maisha ya huku naomba mnielewe hivi yaani sina furaha nayo na malengo yangu kiujumla kimaisha ya binafsi na kimaendeleo yangu yaani hayaendani na mipango yangu ya kuanzisha familia na maendeleo kimaisha kiujumla

Nilikuja huku miaka mitatu baada ya kumaliza form 4, lengo lilikuwa kuja kutafuta lakini kila miaka inavyokwenda naona nakuwa ndio mwenyeji wa huku alaf na hakuna maendeleo ya kweli si haba napata vijisenti lakini siioni vision yangu yaani sioni miaka yangu 20 mbele nakuwa mtu gani? Katika maisha yangu, nikianza kwenye maisha ya mahusiano yaani maisha ya kutafuta mchumba/mke yaani sioni yalee maadili niliyoyafahamu kama mtanzania naona naenda kuharibu familia yangu nikipata kabinti huku kwa ajili ya kuwa mke wangu na kujenga nae familia kiujumla

Utamaduni wao na wetu ni tofauti kabsa isitoshe wao wana uzungu mwingi so nafikiri cha kwanza kwenye hilo la kuanzisha familia ni changamoto sana kwangu na nimefatilia wengi wanaokuja kuanzisha maisha huku huwa wanafeli kwenye swala zima la kupata mke na kutulia naye kwenye familia wanaoshia kuzaa nao na kuingia nao kwenye migogoro ya kugombea watoto, wanawake wengi wa huku wapo kwa ajili ya kustahareheka nao tu na sio kuanzisha familia na kuishi kwenye ndoa yaani ukipata wa kutulia naye kwenye ndoa wewe ni umebahatika sanaa

Nahofia naweza nikapoteza miaka mingi na nguvu zikaniishia nikawa mzee wa huku na nikashindwa kurudi nyumbani

Nimejipa miaka miwili kuanzia sasa ya kujichanga chochote kilee nitakachokuwa nacho baada ya miaka miwili nirudi nyumbani nacho kwa ajili ya kuishi nyumbani mazima, Moyo unaniuma sanaa naona watanzania wanavyoteseka sanaa na maisha ya huku yaani bora uwe unapata vijisenti ila kama ndio choka mbayaa unateseka sanaa aisee, inauma sanaa, unakuta wengine ni watu wazima yaani yale makamo ya kuitwa babu na amepanga pahala hana kitu na anaishi maisha ya kubangaiza inauma sanaa aisee nahofia hio hali isije ikanikuta mimi nikaja pata tabu wakati nina uwezo wa kuamua sasa hivi na nikaja kuwa zaidi ya hapa nilivyo nikiwa nyumbani

Ukweli ni kwamba tunaangaika tu manchi ya watu ila nyumbani ndio pahala pa kufanya maisha na zipo nchi za kwenda kufanya maisha ila sio Africa Kusini maana changamoto ni nyingi nyingi sanaa

Kwenye swala la kipato siwezi danganya Africa Kusini ni rahisi sanaa kwenye kupata pesa ukiringanisha na nyumbani Tanzania, hofu yangu ni kwamba kwa mda gani nikirudi nyumbani nitaweza kusimama kiuchumi na kujitegemea Kama huku hapo ndipo kichwa kinapoanza kuniuma zaidi lakini kiukweli nimeamua kurudi nyumbani na kuanza maisha upya liwalo na liwe na najikubali ni mchakalikaji InshAAllah mambo yakatakaa sawa tu hata ikichukua muda mpaka kusimama nipo tayari

Mimi binafsi sio mwenye kipato kikubwa huku nilipo ila MashaAllah kinapatikana cha kusaidia wazee wanapokwama ila ukweli ni sio pesa kubwa ambayo naweza kujenga wala kufungua biashara na isitoshe mi ni bado kijana bado nna nguvu so naona nikirudi nyumbani nitajishughulisha na nitakaa sawa tu kiuchumi na kuendelea kusaidia wazazi na mimi binafs kiujumla

Changamoto ingine huku ni Stress , stress inaumiza sanaa huku aisee yaani ukijicheki kuna vitu haujaseto then nyumbani kuna jamaa zako hawajasafiri na wapo vizuri kimaendeleo aisee unazidi kupagawa, wanakwambia usimwangalie mwenzako ana nini? Ila kwa kawaida lazima ujiringanishe ili ujione upo upande gani!!

Binafsi sina furaha na maisha ya huku kwamimi binafsi sio watu wote waliokuwepo huku, yaani naishi maisha ya wasi wasi sanaa haijalishi niwe napesa kiasi gani? Lakini sina raha kabsa na kingine sio mtu wa pombe,bange,sigara,wanawake kama wengine nafikiri hilo nalo linachangia

Hapo kwenye furaha, nilishawahi kurudi bongo na nikaona jinsi gani? Nikiwa Africa kusini sina furaha nikiringanisha nikiwa Tanzania, aisee niliporudi nilikuwa na amani ya moyo sio ya kawaida na nilikaaga miezi miwili nililazimika nirudi tena Africa kusini na hauwezi amini nilianza kuumwa nilipokaribia kusafiri yaani nilisafiri nikiwa naumwa yaani binafsi nafsi ilikuwa haitaki kusafiri nilikuwa najilazimisha, nafikiri sio Africa kusini labda nchi nyingine kwa miaka hii 6 hapa Africa kusini inanitosha nahitaji kurudi nyumbani kutulia

Ugonjwa wa akili na maisha ya huku ni kawaida sanaa kukutana na wabongo hawapo vizuri kiakili ni kawaida sanaa nafikiri ugumu wa maisha unasababisha mtu kuumia akili binafsi nasikitikaga sanaa nikimkuta mtu akili yake ime confuse aisee naumiaga sanaa

Nishakutanaga na mijadala ya matusi kwa watanzania wanaoishi South Africa na naumiaga sanaa nikisikiliza au kusoma mijadala hio yaani inauma, ukimkuta mtu yupo nchi za watu alaf ajielewi inauma sanaa

Na wengi wetu tunakujaga huku tukiwa hatuna kitu kabsa tunakuja kujitafuta nafikiri ndio sababu wengi maisha yanatuchapa ila kama unakuja huku kwa kazi maalum yaani unakuja huku kwa mission maalum labda kwa mfano umekula mkataba wako na kampuni fulani labda wa mwaka mmoja unafanya na ukimaliza unaondoka nchini kwako hio isingekuwa tatizo kama tulivyorundikana hivi

Wachache sanaa wenye akili ndio wanafanikiwa kweli ila kusema ukweli wengi sanaa wanapata tabu na kuishi maisha ya tabu sanaa yaani wengine wanaingia kwenye biashara ambazo haramu bila wao wenyewe kupenda na bila mafanikio yeyote yalee

Wageni wengi tunanyanyasika kwa wazawa Kama mnavyojua na kusikia kuhusu Africa Kusini na wageni kwa ulee ukweli hatuna haki kama anayopata mzawa wa nchi kulingana na nchi zingine zinavyowaheshimu wageni, uwenda ukadharauliwa na kufanyiwa mabaya na serikali isichukulie kwa serious, nafikiri zipo nchi za kwenda kufanya maisha ila sio hapa Africa kusini

Wageni wengi hatuna vibali hilo halipingiki, wachache sanaa ndio wanazingatia vibali na uzembe unaweza ukawa mgumo mbovu wa nchi na wa wageni kidogo nchi haionyeshi kama ina haja na wageni yaani mgeni sio kipaumbele kabsa kiufupi mgeni hatakiwi Africa kusini

Vijana wengi wameharibikiwa, wezi, wanatumia mihadarati na kuiuza yaani mbaya zaidi kuwa teja tena nchi za watu au mwizi nchi za watu hakuna mtu anayeweza kukukalisha chini na kukupa somo uachane na tabia hizo mbaya kila mtu anajiangalia yeye mwenyewe so utazidi kuharibikiwa na maisha yako unatakiwa kuwa na akili tulivu sanaa kufanikiwa ukiwa huku kwani maisha ambayo hayakupi second chance ukishayakosea

Ukikutana na watu wazima waliopigika na maisha haya lazima watakusihi sana kuhusu uwe na utaratibu wa kurudi nyumbani kila baada ya mda yaani ukimsikiliza kwa sikio la tatu kana kwamba anakwambia mwanagu rudi nyumbani ukajitafute kwani ukipata ukiwa nyumbani ndio umepata kweli ila sio ukipata ukiwa huku sawa sawa na haujapata kitu

Nimeamua kurudi nyumbani baada ya miaka miwili, ninachofanya sasa hivi ni kuzima simu ili kukimbia vizinga na kujimeki kweli kweli kwa hali na mali yaani ni kujinyima kisawa sawa na isitoshe ni kijana mdogo miaka 28, bado naweza nikalisaidia taifa langu kama mtanzania naweza kufanya jitihada mbali mbali za kujisaidia na kuisaidia familia yangu na kujenga maendeleo yangu kiujumla nafahamu mwanzo ni mgumu sanaa lakini najua kwenye kufanikiwa na maumivu pia yapo, ntapambana kwa hali na mali ili mambo yawe sawia

Shukrani
 
Duuh pole sana!umeongea kwa uchungu sana!Kweli rudi nyumbani kumenoga huko hakufai,wamesahau wema wa Watanzania,waliishi kwetu,Mazimbu-Morogoro,Bagamoyo-Pwani,Kongwa-Dodoma.
 
Cha ajabu si watu wa mazimbu tuna nduguzetu wameolewa na kuzaa watoto na wale wakimbizi alafu hatushobokei huko kwa makabulu, yaani unaenda kule unajua nafikia wapi, Cha ajabu wanaojitosa wakifika wanalandalanda tu huzuni kweli.
 
Nakushauri rudi kwa jinsi ulivyoandika naona kabisa una vita kali ndani tako. Ila kabla ya uamuzi huo ngumu mshirikishe Mungu sana wazo lako ili usije ukajilaumu pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…