Prince Kamugisha
Member
- Jul 29, 2018
- 96
- 237
Naombeni Msaada wenu wadau,
Nataka kununua Gari mojawapo kati ya hizi mbili RAV4 na Vanguard ya mwaka 2010. Kwa mtazamo wangu naona kama haya magari yamefanana kwa kila kitu, sasa basi mwenye kuyafahamu vizuri haya Magari naomba anichagulie nichukue lipi
Asanteni.
MAONI KUTOKA KWA WADAU
Nataka kununua Gari mojawapo kati ya hizi mbili RAV4 na Vanguard ya mwaka 2010. Kwa mtazamo wangu naona kama haya magari yamefanana kwa kila kitu, sasa basi mwenye kuyafahamu vizuri haya Magari naomba anichagulie nichukue lipi
Asanteni.
MAONI KUTOKA KWA WADAU
Kwa uelewa wangu, Vanguard na RAV4 ni gari lile lile. Tofuati kubwa kati ya hayo magari mwili ni kitu wanaita wheelbase, na majina tu. Vanguard ni long wheel base ya RAV4. RAV4 ilikuwa ikilalamikiwa saana US kwa engine ndogo na ukosefu wa third row seat (uwezo wa kubeba watu 7). So kwenye third generation, yaani model ya kuanzia 2006 Toyota wakatengeneza RAV4 ya kawaida ya engine ya cylinder 4, na hiyo ndefu ambayo kwa US ilikuwa na cylinder 6.
Sasa kwa Japan nafikiri na baadhi ya masoko, hiyo RAV4 ya long wheelbase ilibadilishwa jina na kuitwa Vanguard, sababu ile short wheelbase ilipendwa saana Japan, so wakaamua waichae iendelee sokoni, ila wanaotaka long wheelbase wakapewa Vanguard. Ni kweli Vanguard ilikuwa na features baadhi ambazo hazikuwa kwenye RAV4 ukizingatia ilianza kutengenezwa miaka miwili baada ya 2nd gen RAV, ila ni chache saana, nyingi zinafana. Kasoro mbele tu, hasa kwenye bumper na nyingine zinakuja na CVT. Vingine vinafanana.
Kingine kikubwa kilichokuwa introduced kwenye Vanguard, na baadhi ya RAV4, nafikiri ya mwaka 2009 ni kitu wanaita Run Flat Tyre (RFT) ili kuweza kupata nafasi ya kuweka third row seat. Hili ni tairi ambalo haliishiwi upepo hapo hapo linapopata pancha. Kiuhalisia, upepo unaisha, ila walichofanya ni kuweka kuta ngumu za pembeni za tairi hizo kiasi kwamba hata likipata pancha tairi halibonyei kwa umbali kadhaa mpaka utakapofika kwenye sehemu ya kuzibia pancha. Ndio maana Vanguard nyingi hazina spare tyre kwa nyuma kama RAV4 (Ni chache saana nimeona zina spare tyire). Mara nyingi unakuta zina vifaa vya kuzibia pancha, na ki mini compressor cha kujaza upepo.
Hizo RFT kwa kweli huwa sizipendi, as zinafanya gari inakuwa uncomfortable. Na sijui kama zinapatikana huku kwetu. So inamaana tairi zinazokuja na gari zikiisha, inabidi uanze kubeba spare tyre kwenye boot ambayo inachukua nafasi ya mizigo, sababu Vanguard inayokuja na RFT haina sehemu ya kuwekea spare tyre.
.