SoC04 Nini tufanye ili kuboresha sekta ya afya miaka kumi ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Salimu Maulidi idd

New Member
Jun 14, 2024
2
0
Afya ndiyo mtaji wa maisha ya binaadamu,bila kuwa na afya bora huwezi kufanya shughuli za uzalishaji mali na badala yake ni kupoteza kile ulichokuwa ukikifanya kama chanzo cha mapato, sababu hiyo pia hupelekea umaskini.

Kumbe basi Serikali ni watu ili nchi iwe katika hali nzuri ya kiuchumi Afya ni moja ya kichocheo kikubwa katika maendeleo.

Serikali inapaswa kuhakikisha inaboresha sekta ya afya kwa kiwango kikubwa, kwani Serikali ni watu na watu wenye afya njema ndiyo wanaweza kufanya shughuli za izalishaji mali pia pato la Taifa hukua kwa namna hiyo.

Mambo ya kufanya ili kuboresha sekta ya afya.
-Kuwekeza katika kuzalisha Madaktari na wauguzi wabobezi''serikali inapaswa kusaidia kwa scholarship vijana wenye vigezo na malengo ili kwenda kupata ujuzi kwa nchi zilizoendelea"
-Serikali inapaswa kununua au kubuni kutoka kwa wataalamu wa ndani mitambo yenye Teknolojia ya hali ya juu inayofaa kutumiwa hospitalini.
-Serikali inapaswa kusamehe kodi za dawa tiba zote zinazotoka nje ya nchi.
-Serikali inapaswa kuweka miundombinu wezeshi katika maeneo husika. (majengo bora na ya kisasa)
Hitimisho.
Ili Mabadiliko ya Sekta ya Afya yaweze kupata mafanikio, ushirikiano wa karibu kati ya sekta na mamlaka mbalimbali ni muhimu. Mwananchi shiriki kikamilifu katika Mabadiliko haya ili kuboresha utoaji wa huduma za afya.
 
Back
Top Bottom