Nini Sababu Wasio Wakristo Kujaza Kwenye Ibada za Kilokole?

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,288
15,240
Nimekuwa nikitazama sana vipindi vya kimahubili luningani hasa vya wale wachungaji wakubwa mno kama Vile Much Mwamposa wa Arise&Shine TV, Kuhani Mussa Richard wa JehovaJireTV nakadhalika.

Katika nyakati za kutoa ushuhuda wa Yale waliyotendewa na Mungu, iwe uponyaji au kufunguliwa kutoka katika monyororo ya shetani, pamekuwa na watoa ushuhuda wengine wenye majina yasio fanana na ya kikristo kwa Mfano, Ashura, Jummane, Fadhili, Abdul, Huseni na mengineo yenye kunasibu dini nyingine.

Nini Sababu ya ongezeko la wasio wakristo katika madhabahu za bwane Yesu.?

Je inawezekana kuwa nyakati zinakaribia na kwamba Kristu analikusanya KANISA lake?

Au ni kwasababu ukweli inaanza kutamalaki machoni pa walio si wakristo?

Karibuni.
 
Kuna mawili.
1) Ni watu wanaolipwa kufanya maigizio msikilize 100.5 FM anayejiita Kiboko Cha Wachawi anaye igiza kufua watu usiku kucha kwa kupigiwa simu tuu,
2) Wengine huenda kama wanavyo kwenda kwa mganga wa kienyeji kutafuta suluhisho la matatizo yao (baadala ya kuiitikia TAWIRE kwa mganga wao kiitikio BWANA YESU ATUKUZWE) wakitoka hapo Imani ya kidini hakuna Wala hawajui Masiha alibatizwa wapi na nani au hata kujisomea Biblia.
 
Siungi mkono kuhama Hama kanisa, huo ni sawa tu na ukahaba
Topic haizungumzii kuhama Makanisa.

Ni kuhusu wale ambao sio wakiabudu ktk Makanisa ,kuja kuanza kuabudu ktk Makanisa ya kiroho.

(Kwani ujanielewa?)
 
1) Ni watu wanaolipwa kufanya maigizio msikilize 100.5 FM anayejiita Kiboko Cha Wachawi anaye igiza kufua watu usiku kucha kwa kupigiwa simu tuu.
Inawezekana.

Lakini kwenye kulipwa hapo ninapinga kidogo.

Mtu kama Mwamposa ameanza huduma tngu kitambo sana. Tusema tuanze kuhesabu watu walio kuwa wanatoa USHUHUDA tangu anaanza huduma.

Kwa mwaka Kuna juma pili 52. Kila Juma pili watu 10 hutoa USHUHUDA kanisani

Hivyo 52 X 10 = 520 watoa USHUHUDA kwa kulipwa (kwa mwaka)

Mwamposa huduma yake ilianza kushamiri mwaka 2010. Hivyo ni miaka 14 mpaka Leo hii.

Watu 520 X 14 = 7,280 watoa USHUHUDA kwa kulipwa.

Jumla ni watoa USHUHUDA 7,280 wa kulipwa.

SWALI:-
Umeshawahi kutana na mtoa USHUHUDA wa kulipwa hata mmoja (1) kati ya hao 7,280 ambaye akakuthibitishia kuwa alilipwa na Mwamposa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom