1.Sekta ya afya hali mbaya--Madawa hakuna hospitalini. Kuna vituo hata panadol havina.
2. Sekta ya viwanda naona bado tuko nyuma sana.
3.Sekta ya elimu bado tunasuasua. Ile sera ya elimu bure naona ina hali mbaya.
4.Uchumi bado unadorora.
5. Ukusanyaji kodi tumerudi kulekule alipotuacha Rais Kikwete 900 bil.
6.Sekta ya kilimo na ufugaji bado hamna mipango inayoeleweka.
7.Michezo bado tuko nyuma sana..Huwa najiuliza kwa nini kila siku serikali ina-finance timu ya taifa ya mpira wa miguu na hamna mafanikio.
8.Uhuru wa kujieleza umeminywa.
......Na mengineyo
Sasa najiuliza ni kwamba serikali inajipanga au ni nini shida. Kama nchi ni nini priority yetu? Wapi tumekwama na tufanyaje kurekebisha? Je tutafika uchumi wa kati kwa style ya sasa?