Mtu Alie Nyikani
JF-Expert Member
- Nov 9, 2022
- 821
- 1,815
Habari,
Leo Katika siku tulivu, nilipata muda wa kutafakari juu ya maajabu ya ulimwengu. Niliketi nje, nikisikiliza upepo ukivuma na kutazama anga pana. Katika utulivu huo, swali moja lilinijia: "Je, maisha ni nini?" Swali hili liliamsha hamu ya kutafuta majibu, lakini pia lilinifanya nijiulize maswali mengi zaidi.
Ni kweli kwamba tunapambana sana hapa duniani, tunatafuta mali, madaraka, na mafanikio. Lakini je, haya ndiyo yote ambayo maisha yanatupa? Tunapoangalia nyuma, tunaona jinsi vitu vingi tunavyovifanya vinavyoonekana kuwa vidogo sana ikilinganishwa na ukuu wa ulimwengu. Tunapojilinganisha na muda mrefu wa historia, maisha yetu ya hapa duniani ni kama chembe ndogo sana mithiri ya mbegu moja ya mchicha. Yote haya huwa ni kazi bure kwa sababu mishoni tunaishia ardhini na kuviacha hivi vyote tulivyo vipambania , kwa hakika maisha ya mwanadamu ni kazi Bure. Sababu yote haya kifo kinakuja kuyamaliza.
Kifo ni ukweli usioepukika. Ni mwisho wa safari yetu duniani. Lakini je, kifo ndicho kinachofanya maisha kuwa na maana? Au kuna kitu kingine zaidi? Labda maana ya maisha ipo katika safari yenyewe, katika uzoefu wetu, katika mahusiano yetu na wengine, na katika mchango wetu kwa ulimwengu.
Nilijikuta nikifikiria wimbo mmoja wa Bushoke unaoitwa "Dunia Njia". Wimbo huu umenipa ukumbusho muhimu kwamba maisha ni safari tu, na kwamba hatimaye tutaondoka duniani. Matendo yetu hapa duniani ndiyo yatakayotufanya tukumbukwe na ndiyo yatakayoamua hatima yetu.
Katika mwisho, tunaweza kuhitimisha kwamba maisha ni zawadi ya thamani. Ni fursa ya kujifunza, kukua, na kuacha alama ya kudumu katika ulimwengu. Lakini ni muhimu kukumbuka kwamba maisha ni ya muda mfupi, na kwamba tunapaswa kuitumia kwa busara na Kwa utu.
"Tusichoke kuomba kila tunapo amka, na kabla ya kulala"