Nini maana ya Banana Republic? Je, Urusi ni Banana Republic?

George Betram

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
4,522
6,008
Leo nimekutana na mchango wa mwanachama wa Jamii Forums (Imeloa) akisema kuwa Russia ni Banana Republic, hili jina limenishtua kiasi, of course sielewi maana halisi ya Banana Republic.

Ila kwakuwa Jamii Forums kuna manguli wa GEOPOLITICS, ninaamini leo nitatolewa ujinga kidogo.

Wakongwe, nini maana ya Banana Republic? Nini sifa za Banana Republic? Je, Russia ni Banana Republic?

Nilikuwa na uwezo wa ku-google, lakini nahitaji kujifunza zaidi kupitia mjadala wa hapa jukwaani, watu tofauti tofauti wanavyotoa maoni na ujuzi wao kuhusu hili swali langu, tena kwa lugha rafiki ya Kiswahili inakuwa ni zaidi ya elimu na watu wengine wanapata nafasi ya kujifunza pia.​
 
Banana Republic inatokea au ni pale serikali ya nchi flani inaendesha nchi katika uchumi wa kibepari, nchi inaendeshwa kama biashara ya mtu/watu binafsi na kwa faida pekee kwa tabaka tawala la nchi hiyo.
Je, Russia ni Banana Republic?
 
Kwa ufupi maana ya banana ni Nchi ambayo haiko huru.yaani haijiwezi Kwa Kila kitu.mfano kama mama anavyotembeza bakuli kule ulaya na kupewa mikopo ya riba kubwa na kutumia hovyo.Au ni sawa na kusema dependent government (tz under kizimkazi)
 
Banana Republic =Tanzania government
😠
20240621_173534.jpg
 
Walei kwenye moja na mbili,rais awapo mvaa kobazi,mtaacha lini wazee,au ni doctrine ya vigango!?..ngozi huwasha sana au koromeo,ikulu akikaa mvaa kobazi!?
 
Huyo Imeloa si kichaa kama vichaa wengine ni wale Pro Western hata akiombwa na mzungu Figo moja yeye atampa mawili yani wajinga kweli kwa Western, wanamini kila wanacho ongea hao ma Western
 
Banana Republic inatokea au ni pale serikali ya nchi fulani inaendesha nchi katika uchumi wa kibepari, nchi inaendeshwa kama biashara ya mtu/ watu binafsi na kwa faida pekee kwa tabaka tawala la nchi hiyo.
Vipi Tanzaniha yetu?.... nahisi nayo ni Banana republic!
 
Navyojua jamhuri ya ndizi ni nchi ndogo yenye uchumi mdogo isiyoweza kujitegemea, inayotegemea export ya maliasili hasa mazao na inayoendeshwa kiujanjaujanja na collaboration ya tabaka tawala la wanasiasa, wanajeshi na wafanyabiashara tabaka hili ndio linanufaika hasa na linafanya kazi kama mawakala wa mabepari wa nje. Mfano wa nchi ambazo ni jamhuri za ndizi ni Guatemala ambako hasahasa ndiko jina lilikoanzia kutoka kwa msomi wa siasa William S. Porter.

Kwa mantiki hiyo Russia kamwe si jamhuri ya ndizi. Kwa sababu:
1. Inajitegemea kiuchumi

2 inajitegemea kiteknolojia

3.inajitegemea kisiasa na kiadeolojia

4. haina tabaka tawala linalofanya kazi ya kunyonya uchumi wa nchi kwa maslahi ya mabepari wa ulaya na amerika
 
Huyo Imeloa si kichaa kama vichaa wengine ni wale Pro Western hata akiombwa na mzungu Figo moja yeye atampa mawili yani wajinga kweli kwa Western, wanamini kila wanacho ongea hao ma Western
Na wewe pia tukusemeje kwa nchi za kiislam na mataifa ya kiimla kama Russia, China, Iran na North Korea.
 
Kwa ufupi maana ya banana ni Nchi ambayo haiko huru.yaani haijiwezi Kwa Kila kitu.mfano kama mama anavyotembeza bakuli kule ulaya na kupewa mikopo ya riba kubwa na kutumia hovyo.Au ni sawa na kusema dependent government (tz under kizimkazi)
Hauko sahihi kwa 100%
 
Back
Top Bottom