Nini kinafanya Sekta ya Ngozi nchini ishindwe kukua kulinganisha na nyingine?

its official B

New Member
Sep 16, 2021
2
6
Je, Wewe unafahamu Nini kuhusu sekta ya NGOZI nchini hapa Tanzania? Na nichangamoto gani zinaifanya ishidwe kukua hapa nchini?

Ukilinganisha na nchi zingine kama Ethiopia n.k?
 
Najuwa banda la ngozi imebaki kituo tu cha daladala, na bora shoes sijui imefia wapi?
 
Shida kubwa ni jinsi ya kuiandaa ngozi jinsi ya kuikata ngozi na ubora wa ngozi hasa kwenye ile sehemu ya kuweka alama kwenye mnyama huwa inapoteza ubora wa Ngozi, kunakipindi Serekali ilikuwa inapitisha matangazo kwaajili ya kuwaelimisha wafugaji jinsi ya kuweka chapa kwenye mifugo ili isiharibu ubora wa Ngozi.
 
Tatizo letu kubwa ni UBORA wangozi kwa maana ya kuiandaa ngozi toka mnyama anapozaliwa hadi anapochunwa ngozi na namna ya kuhifadhi ngozi hiyo

Wasukuma ambao ni wafugaji wakubwa sana na wamasai wanaharibu sana ngozi za mifugo kwa kuweka alama nyingi zinazo haribu ubora wangozi

Uchunaji nao ni shida ngozi inatobolewa tobolewa sana

Na kikubwa kabisa ni namna ya kuitumza ngozi baada ya kuwa tayari imechunwa hadi kuja kuiuza...... hapa ndio kunachangamoto kubwa

Kenya wanajitahidi sana
 
Kuna mahala kwakweli tulilogwa vibaya sana maana kwenye hii sekta Kenya wametupita kila mahala sio ngozi tu hata uuzaji wa wanyama hai na Nyama iliyo tayarishwa na kuwa na mbegu bora ktk kuzalisha .
 
Je, Wewe unafahamu Nini kuhusu sekta ya NGOZI nchini hapa Tanzania? Na nichangamoto gani zinaifanya ishidwe kukua hapa nchini?

Ukilinganisha na nchi zingine kama Ethiopia n.k?
Tanzania hakuna wazalishaji wengi tunategemea biashara tena za mchogo, kukwepa TRA ,uchawa wa chama ili kulegezewa maisha ,hivyo kila kitu na roho zetu tumezitelekeza kwa mchina hatuzie chochote ,hata akitumia taka ngumu za china kama nywele,kucha,ped wanatutengenezea vitu kama miguu ya meza,kabati, urembo nk.hvyo ili kuiokoa Tz njia sahihi ni kupata dikteta au mtu mwenye upeo mkubwa kama mimi kuishauri serikali kwa ukaribu sana.
 
DIT Kampasi ya mwanza kwa sasa wanatoa wataalamu wa ngozi kwa ufadhiri wa serikali. Karibuni sana.
IMG-20240811-WA0040.jpg
 
Back
Top Bottom