SoC01 Nini kifanyike? Wasomi wetu wamekuwa vibogoyo

Stories of Change - 2021 Competition

Gnyaisa

Member
Jul 13, 2021
23
24

Ukipata fursa ya kuonana na kuongea na daktari bingwa yeyote wa magonjwa ya watoto au yule wa afya ya kinywa na meno, miongoni mwa ushauri mkubwa atakaokusisitizia ni ule wa kutowapa watoto wako vyakula vyenye sukari kwa wingi hasa biskuti, pipi au keki. Madhara yatokanayo na kuupuzia ushauri huu huwa ni kuoza kwa meno na hatimaye mtoto huyu kujikuta akiwa kibogoyo katika umri mdogo kabisa wa maisha yake.

Mfumo wa elimu unaotumika kuwaandaa wasomi wetu nchini na barani Afrika kwa ujumla ni wazi kabisa umekuwa ukitengeneza vibogoyo kwa miaka nenda rudi. Kwa faida ya msomaji, kibogoyo ni mtu asiye na meno au kwa lugha rahisi mtu asiye na madhara kwa vitu vitamu kama nyama, mahindi ya kuchoma au karanga.

Nchini Tanzania kijana hupitia mfumo wa elimu wa takribani miaka 16 mpaka kuwa mhitimu wa Chuo Kikuu. Huanza na miaka 7 ya elimu ya msingi, kisha miaka 4 ya sekondari na mingine 2 ya sekondari ya juu na baadaye kuanza miaka mingine mitatu hadi mitano ya elimu ya Chuo Kikuu.

Kwa matarajio ya kawaida tunategemea msomi wa shahada ya utawala katika biashara aliyetumia Zaidi ya muongo mmoja na nusu akiwa shule atakuwa msaada mkubwa kwa mamalishe pale mtaani asiyezingatia utunzaji bora wa mahesabu na asiye na dira yoyote au maono makubwa ya biashara yake ya chakula. Tunategemea msomi wa shahada ya kilimo na ufugaji atakuwa mkombozi mkubwa wa mkulima pale kijijini kwake kwa kumpa mbinu za kisasa za kilimo na kumuunganisha na wadau muhimu wa kilimo walioko ndani na nje ya nchi. Tunategemea mtaalamu wa masuala ya sheria aliyetumia Zaidi ya miaka 18 darasani atakuwa msaada mkubwa kwa mwananchi wa kawaida anayezulumiwa kila siku na mgambo wa jiji pale Dar es Salaam.

Tofauti na matarajio hayo, wasomi wetu wamegeuka vibogoyo! Hawana meno, hawang’ati, hawatishi tena, wamegeuka kuwa matanuru ya lawama zisizokwisha dhidi ya serikali yao, wazazi wao na taifa lao. Wanatamani bora ukoloni ungeendelea kwa kuwa mzungu angethamini elimu yao na kuwapa ajira ya kuwachapa viboko manamba wenzao ambao hawana elimu!

Ukizunguka katika taasisi mbalimbali nchini utakutana na vioja lukuki juu ya wasomi hawa. Mabenki na taasisi nyingi za fedha wafanyakazi wao (bank tellers) ni wahitimu wa masuala ya sayansi na kompyuta badala ya wataalamu wa fedha, wasomi waliobobea katika kilimo au ufugaji wamejivika utaalamu wa fedha na utawala katika biashara! Siasa za nchi kwa maana ya nafasi za ubunge na udiwani, ukuu wa mikoa na wilaya wameachiwa wafanyabiashara, wahandisi na wastaafu wa fani zisizo na taaluma ya siasa ilhali wataalamu wa sayansi ya siasa wakisukumana kupata ajira ndani ya jeshi! Wataalamu wa utawala katika biashara wamegeuka wasuluhishi wa masuala ya kisheria ilhali wataalamu wa sheria wamekuwa wachuuzi wa bidhaa kutoka China na mataifa mbalimbali ya ulaya. Mwisho wa siku mambo yamekuwa hayaendi kwa kasi iliyotarajiwa na taifa limejaa manung’uniko kila kona.

Nani wa kulaumiwa katika hili? Je, ni serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa zaidi ya nusu karne sasa au wasomi hawa waliogeuka vibogoyo? Kudhani au hata kujaribu kuamini kwamba chama kipya cha siasa kikifanikiwa kuingia madarakani na kuongoza serikali kitabadili hali ya mambo ni upunguani kwakuwa vibogoyo hawa wapo katika vyama vyote vya siasa vinavyoongozwa na wasomi barani Afrika. Kuwalaumu wasomi hawa kwa kugeuka vibogoyo ni upunguani pia. Utawezaje kulaumu kikokotozi chako kwa kukupa jibu la “sifuri” ilhali ni wewe mwenyewe uliyejaza taarifa za “tisa kutoa tisa”?

Lawama zote unatupiwa MFUMO WA ELIMU tulioachiwa na mkoloni ambao haujabadilika hadi leo licha ya maendeleo makubwa ya kiutamaduni, kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia. Mfumo unaomwachisha masomo ya kuendelea na elimu mwanafunzi wa kidato cha nne aliyetumia miaka minne darasani kwa mtihani wa taifa wa masaa matatu pekee! Mfumo unaomtaka mwanafunzi akariri alichofundishwa na mwalimu wake na acheue kilekile siku ya mtihani! Mfumo unaomwaminisha mwanafunzi kwamba kufaulu maana yake ni kuongoza katika masomo darasani na kufeli maana yake ni kushika mkia katika masomo darasani! Mfumo ambao mitaala na hata vitabu vinavyotumiwa na Vyuo Vikuu nchini katika fani mbalimbali vinatoka moja kwa moja ulaya na Marekani kisha tutegemee akili ya msomi huyu itawaliwe na mawazo ya Sinza au Manzese!

Wasomi hawa wakija katika maisha halisi mtaani wanakuta mambo kinyume na walivyofundiswa. Wanajikuta wakipewa masaa matatu pekee ya kusoma katika darasa la maisha na kisha miaka minne ya kupambana na mitihani ya maisha kila siku! Wanakuta katika maisha kuongoza darasani au kuwa na akili nyingi ya masomo si kitu bali uwezo wa kubadili akili hizo kuwa bidhaa zenye kuuzika kwa umma wa watanzania. Wanagundua kumbe hawana meno! Hawafai katika jamii! Wamelaghaiwa! Wanageuka kuwa matanuru ya lawama huku wakizungusha vyeti kutafuta kazi yoyote itakayowalipa mshahara wa kujikimu! Wanageuka kuwa wasaliti wa taaluma zao walizozisotea kwa miaka nenda rudi!

Kulaumu MFUMO bila kutoa suluhisho si jambo la busara. Suluhisho si kuufuta mfumo huu kwa sababu ni mfumo wa elimu unaotumiwa na dunia nzima. Wazungu wana usemi wao maarufu usemao “If you can’t fight them, join them” (Kama huwezi kupambana nao, ungana nao). Pia wana usemi mwingine usemao “If you know your enemy, half of the battle is won” (Kama unamfahamu adui yako, umeshinda nusu ya vita). Kwakuwa tumetambua chanzo cha ubogoyo wa wasomi wetu, tayari tumejihakikishia ushindi. Na kwa vile hatuwezi kupambana na adui MFUMO, njia bora ni kuungana nae.

Tuungane na adui MFUMO kwa sisi vijana kujitambua kifikra na kutumia muda wetu mwingi kujifunza mbinu bora za maisha kutoka kwa watu waliofanikiwa katika fani au ndoto kama tulizonazo badala ya kukesha tukiunda makundi ya urafiki na kutukanana katika mitandanao ya kijamii.

Tuungane na adui MFUMO kwa kuacha lawama dhidi ya wale tunaodhani ndio chanzo cha kuharibikiwa kwetu ikiwemo serikali, dini flani, ndugu au jamaa zetu na kuamini kwamba pale tunapojikuta tukizungukwa na changamoto nyingi za maisha ndipo pia zilipolala fursa nyingi za mafanikio. Lawama siku zote ni kufuri la milango ya mafanikio, lawama hupofusha macho yenye kuziona fursa za utajiri.

Tuungane na adui MFUMO kwa kuacha kula vyakula vyenye sukari nyingi hasa pindi tuwapo mashuleni. Vyakula hivi si biskuti, pipi na keki bali maisha ya mteremko kwa kudhati zipo njia za mkato za mafanikio kama zile za kukaa masaa matatu pekee kwenye chumba cha mtihani na kisha kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano. Maisha ni mapambano na taifa letu linahitaji vijana wenye nguvu na wapambanaji. Wenye meno marefu na makali ya kupambana na adui UJINGA kwenye jamii na wenye macho angavu yenye kuziona, kuzitambua na kuzichangamkia fursa tele za mama Tanzania.
 
Ukisema ulaumu mfumo wa elimu , Phyics na Chemistry na Math inayofundishwa Tanzania , ni hiyo hiyo inayofundishwa Marekani , India na China.

Mi nazani tufundishe kwa vitendo zaidi ( kuhusisha na mazingira ya kawaida ), kuliko kwa maandishi. Kwa mfano minakumbuka nilimaliza Form 4 najua definition ya Diode na aina za Diode , lakini nilipopewa redio na braza wangu nioneshe Diode ipo wapi nilikuwa sijui.

Pia Elimu yetu itolewe katika biashara , iendeshwe na serikali tu. Ili kila mwanafunzi mtanzania apate Elimu sawa. Hii itachangia wananchi wote kutafuta ufumbuzi wa kila changomoto inayoikumba elimu na ndio mwanzo wa kunufaika wote na sio mtu binafsi.

Nikurudishe elimu ya mkoloni iliongozwa na serikali tu, na wanafunzi waliotokana na elimu ya mkoloni wapo vizuri hadi leo. Lakini baada ya elimu kubinafsishwa na kuwa biashara - fijisu zimekua nyingi - yani hata shule imekua sio shule tena - bali ni mtaro wa kukupeleka ukapate ajira
 
Ukisema ulaumu mfumo wa elimu , Phyics na Chemistry na Math inayofundishwa Tanzania , ni hiyo hiyo inayofundishwa Marekani , India na China.
Mi nazani tufundishe kwa vitendo zaidi ( kuhusisha na mazingira ya kawaida ), kuliko kwa maandishi. Kwa mfano minakumbuka nilimaliza Form 4 najua definition ya Diode na aina za Diode , lakini nilipopewa redio na braza wangu nioneshe Diode ipo wapi nilikuwa sijui.

Pia Elimu yetu itolewe katika biashara , iendeshwe na serikali tu. Ili kila mwanafunzi mtanzania apate Elimu sawa. Hii itachangia wananchi wote kutafuta ufumbuzi wa kila changomoto inayoikumba elimu na ndio mwanzo wa kunufaika wote na sio mtu binafsi. Nikurudishe elimu ya mkoloni iliongozwa na serikali tu, na wanafunzi waliotokana na elimu ya mkoloni wapo vizuri hadi leo. Lakini baada ya elimu kubinafsishwa na kuwa biashara - fijisu zimekua nyingi - yani hata shule imekua sio shule tena - bali ni mtaro wa kukupeleka ukapate ajira
Kweli kabisa. Shule zetu zipunguze nadharia, zijikite katika mafunzo kwa vitendo.
 
Nlimsikiliza mtaalamu flani kwenye clip iliyotembea sana last week mitandaoni hasa whatsapp alieleza kwamba elimu ya Waafrica ni kushindana kukariri, mwenye uwezo wa kukariri ndio anaonekana ana akili, akasema tunajazwa vitu ambavyo havina msingi maishani akatolea mifano unamkaririsha mwanafunzi Mlima mrefu zaidi, ziwa kubwa zaidi mto mrefu, maporomoko na historia za nchi za watu wengine halafu zinamsaidia nini. Mi nikaona ana mantiki, Giografia ya Ulaya na Historia ya Amerika inakusaidia nini we mtanzania?

Hii tunaiona wahitimu walivyojazana mitaani na tunawaita wenye akili kumbe kiukweli walikuwa na uwezo wa kumbukumbu tu. akija mtaani hana cha kufanya.

Niwakati sasa tusome historia yetu tu tuachane kujazana ubongo na akina Mao, Hitla na wengine.

Tuachane na kukaririshana milima, mito, bata tredi, triangular trade
Tuachane na mavitabu ya akina OKONKO, CHINUA ACHEBE, SONG OF LAWINO.

TUJIKITE KWENYE VITU VYENYE TIJA KWA TAIFA. Vitu vitakavyomfanya muhitimu ajitegemee.

China ina teknishiani wengi kuliko wahandisi na ndio hawa wanatujengea magorofa na madaraja na mabarabara. Wahandisi wachache sana hawa unaowaona wanakimbizana na vibarua wa kibongo ni merely technicians tu.

Bongo tuna wahitimu wa uhandisi wakimaliza wanapambana ERB kupata sifa ya kuwa wahandisi wakitoka hapo wanabakia kuwa vibarua wa kuwashikia technitians wa kichina madaftari na kukimbizinana na vibarua huku wakilipwa ujira mdogo sana.

Lets reviews our education systems

NB: KAMA KUNA MAKOSA YA KIUCHAPAJI NISAMEHE MAADAM TU UELEWE YALIYOMO.
 
Nlimsikiliza mtaalamu flani kwenye clip iliyotembea sana last week mitandaoni hasa whatsapp alieleza kwamba elimu ya Waafrica ni kushindana kukariri, mwenye uwezo wa kukariri ndio anaonekana ana akili, akasema tunajazwa vitu ambavyo havina msingi maishani akatolea mifano unamkaririsha mwanafunzi Mlima mrefu zaidi, ziwa kubwa zaidi mto mrefu, maporomoko na historia za nchi za watu wengine halafu zinamsaidia nini. Mi nikaona ana mantiki, Giografia ya Ulaya na Historia ya Amerika inakusaidia nini we mtanzania?

Hii tunaiona wahitimu walivyojazana mitaani na tunawaita wenye akili kumbe kiukweli walikuwa na uwezo wa kumbukumbu tu. akija mtaani hana cha kufanya.

Niwakati sasa tusome historia yetu tu tuachane kujazana ubongo na akina Mao, Hitla na wengine.

Tuachane na kukaririshana milima, mito, bata tredi, triangular trade
Tuachane na mavitabu ya akina OKONKO, CHINUA ACHEBE, SONG OF LAWINO

TUJIKITE KWENYE VITU VYENYE TIJA KWA TAIFA. Vitu vitakavyomfanya muhitimu ajitegemee.

China ina teknishiani wengi kuliko wahandisi na ndio hawa wanatujengea magorofa na madaraja na mabarabara. Wahandisi wachache sana hawa unaowaona wanakimbizana na vibarua wa kibongo ni merely technicians tu.

Bongo tuna wahitimu wa uhandisi wakimaliza wanapambana CRB kupata sifa ya kuwa wahandisi wakitoka hapo wanabakia kuwa vibarua wa kuwashikia technitiaans wa kichina madaftari na kukimbizinana na vibarua huku wakilipwa ujira mdogo sana

Lets reviews our education systems

NB: KAMA KUNA MAKOSA YA KIUCHAPAJI NISAMEHE MAADAMU TU UELEWE YALIYOMO
Tuna safari ndefu sana kama Taifa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom