SoC04 Nini kifanyike katika utekelezaji wa mtaala mpya ili kuzalisha wahitimu wenye weledi katika soko la ajira

Tanzania Tuitakayo competition threads

dour

Member
Aug 7, 2017
7
9
UTANGULIZI
Changamoto ya ukosefu wa ajira nchini imeendelea kukua kwa kasi huku sababu zikielezwa kua ni ufinyu wa bajeti na wahitimu wasio na weledi. Ukosefu wa ajara unapelekea vijana wengi wakijiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na kuongezeka kwa vijana tegemezi. Ukosefu wa ajira unapunguza uzalishaji katika taifa, hali inayo athiri uchumi kitaifa, kwakua serikali itatumia fedha nyingi kuhudumia taifa ambalo uzalishaji wake ni mdogo.

Kwa mujibu wa ripoti ya mtakwimu mkuu wa serikali imeeleza hali ya ukosefu wa ajira ilifika 9% 2021, Wastani wa kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Tanzania kuanzia mwaka 2001 hadi 2022 ulikuwa asilimia 10.3 hii inaonyesha kwamba katika kipindi hiki, Tanzania kwa ujumla imekuwa na kiwango cha ukosefu wa ajira cha juu. Tarehe 15 jun 2023 wakati waziri wa fedha na mipingo Dkt Mwigulu Nchemba akiwasilisha bajeti hiyo alikiri hali ya ajira ni mbaya

Uzalishwaji wa wahitimu wasio kua na weledi imekua ni sababu kubwa ambayo inatajwa kuchangia vijana wengi kukosa ajira. Wazazi hulalamika juu ya wahitimu wanao maliza masomo kushindwa hata kutatua changamoto ndogo ndogo za nyumbani huku wakiwa na maswali mengi juu ya ubora wa elimu unayotolewa nchini. Kutokana na changamoto hiyo serikali iliona haja ya kuanzisha mchakato wa mtaala mpya utakao tatua changamoto hiyo na hadi kutangaza kuanza kwa mtaala huo mwaka 2024.

Ili kutekeleza mtaala huo ulioboreshwa uweze kufikia shule zote kwa ufanisi napendekeza yafuatayo yafanyike

1. Kuongezwa kwa bajeti katika sekta ya elimu kuwezesha mtaala mpya.
Katika utekelezaji wa mitaala mipya ambayo inahitaji uwekezaji mkubwa wa rasilimali watu na nyenzo za ufundishaji inahitaji upendeleo mkubwa katika bajeti. Katika mafunzo ya amali(vitendo) kunahitajika vifa vingi vyenye gharama kubwa, inashangaza kuona ongezeko la bajeti katika wizara ya elimu ni ndogo sana kutoka 1.68 trilioni 2023 hadi 1.97 trilioni 2024 bajeti hii haionyeshi utayari wa serikali katika utekelezaji wa mtaala mpya maana ni ndogo sana

2. kuzingatia uwezo wa wanafunzi kitaaluma katika ufaulu.
Moja kati ya malalamiko ya walimu na wakufunzi wa ngazi ya juu hulalamika kupokea wanafunzi ambao hawakufuzu vizuri elimu ya msingi huku wakisema wengi wao hawajui hata kuandika wala hisabati rahisi. Nashauri serikali kutotumia taaluma kisiasa kwa kujisifia ongezeko la ufaulu wa wanafunzi hii itapelekea wanafunzi wasio na uwezo kupelekwa ngazi za juu ili kufikia lengo hilo. Kutokuzingatia taaluma ya wanafunzi kutapelekea kuzalisha wahitimu wasio na weledi

3. Vipaumbele katika masomo yanayogusa jamii katika maendendeleo
Inashangaza kuona nchi ambayo kilimo ni uti wa mgongo kufanya somo la kilimo kua la chagua. Katika mabadiliko ya kiteknolojia lakini bado somo la tehama ni la chaguo na kwa shule chache. Hivyo serekali iwezeshe kujifunza masomo haya kwa wanafunzi wote ili kuendana na malengo ya kimaendeleo

4. Uhusishwaji wa sekta binafsi na wizara nyingine katika utekelezaji wa mtaala mpya.
Fikiria kila wizara au kila halmashauri iajiri walimu hamsini, au wawekezaji binafsi kuchangia asilimia ya kodi katika maendeleo ya elimu hasa katika kufanikisha mtaala mpya. Katika ushirikishwaji huo baadhi ya taasisi kubwa zingekabidhiwa shule kadhaa zisimamie na kuziwezesha kimiundo mbinu na kutoa ufadhili wa walimu kadhaa. Hii itasaidia kuwezesha upatikanaji wa nyezo mbalimbali za kufundishia pamoja na walimu wa kutosha katika uwasilishwaji wa mtaala mpya.

5. Kuzingatia mahitaji ya wahitimu na soko la ajira katika malengo ya maendeleo kitaifa.
Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti ya kupunguza umaskini REPOA ya 2019 takribani vijana milioni moja huhitimu katika elimu ya juu huku idadi ya ajira zinazo zalishwa ni 250000. Mwaka 2023 jumla ya walio omba ajira za elimu na afya ni 153,512 huku walio ajiriwa ni 18,449. Serekali ingeweka malengo ya mahitaji ya wahitimu na kuwazalisha kulingana na mahitaji hayo.

6. Kuanzishwa kwa sera itakayo ruhusu shule zetu kuongozwa na mashirika
Moja katika shule iliyo fanikiwa ni kibaha sekondari japo ni shule ya serikali ila maendeleo yake yamechangiwa na kuwa chini ya shirika la elimu kibaha. Nashauri serikali iziondoe shule katika wizara na kuziweka katika mashirika na mashirika hayo kuruhusiwa kuwekeza sehemu mbalimbali.

7. Ushirikiano wa shule na ofisi mbalimbali za kazi.
Japo kua mitaala mipya imetangazwa kuanza 2024, bado elimu ya amali imeanza katika shule chache sana zenye miundombinu rafiki. Badala kusubiri shule zetu zitengeneze miundo mbinu hiyo ni bora kushirikiana na ofisi mbalimbali za serekali na binafsi katika mazoezi ya amali kama vile mazoezi ya vitendo(field) yanavyo fanyika elimu za juu.

Kwa ujumla maboresho ya sera na mtaala umeonekana kuleta mwanga katika utatuzi wa kuzalisha taifa lenye weledi katika soko la ajira. Japo changamoto zinazo ikabili wizara ya elimu ni nyingi, wadau wa elimu, wizara mbalimbali, mashirika ya kiserekali na yasio ya kiserekali pamoja na wananchi wote wangeshirikiana na serikali katika utatuzi wa changamoto hizo.
 
Back
Top Bottom