Nini hatma ya Shilingi ya Tanzania baada ya kuporomoka dhidi ya Dola ya Marekani?

Nasdaq

Member
Sep 22, 2024
17
45
Ukweli ni kwamba tokea mwaka 2023 shilingi ya tanzania imeporomoka kutoka 2330 mpaka 2730 kwa dola moja ya marekani ukilinganisha na shilingi ya majirani zetu KENYA ambao shilingi yao inazidi kupata nguvu dhidi ya dola ya marekani hasa mwaka huu wa 2024

Nini maoni yako, wapi tunakosea turekebishe nini au tufanye nini kama nchi.
 
Nadhani inabidi tutoke huko kwa kutegemea Dollar ili maisha yetu yaweze kwenda..., Tungekuwa wazalishaji basi tungeshangilia hii hali sababu vitu vyetu vingekuwa cheaper katika soko....

Na tunafanyeji hivyo ? Ni kuacha kutafuta dollar ili kununua vitu ambavyo mahitaji yake sio ya lazima au tunaweza tukawa na alternative..., Mfano mdogo Sasa hivi tunapigia chepuo nishati safi kuacha kutumia mikaa na tunapigia chepuo LPG ambayo tunaagiza, kitu ambacho tunatumia fedha za kigeni; wakati tungeweza kutumia umeme katika kupikia hence kuondoka na matumizi hayo...

Ukweli ni kwamba tokea mwaka 2023 shilingi ya tanzania imeporomoka kutoka 2330 mpaka 2730 kwa dola moja ya marekani ukilinganisha na shilingi ya majirani zetu KENYA ambao shilingi yao inazidi kupata nguvu dhidi ya dola ya marekani hasa mwaka huu wa 2024

Nini maoni yako, wapi tunakosea turekebishe nini au tufanye nini kama nchi.
Mwaka huu mwishoni itafika 2,900

Hapo ndo mtajua Kwa Nini Maghufuri alifungia Bureau de change.
 
Shilingi ya Kenya na ya Tanzania hazina tofauti kwa miaka mitano iliyopita.
Mwezi February Shillingi ya Kenya ilidondoka kwa asilimia karibu 30 na kufanya GDP ya Kenya na Tanzania kuwa na thamani sawa kwa takriban wiki moja.
Shilingi ya Kenya imedondoka sana, ni basi tu inalazimishwa kukaa ilipo.
 
Shilingi 22 za Tanzania ilikua ni shilingi 1 ya kenya kwa muda mrefu sana, Hela yetu ilipanda sana compare na Kenya hadi ikawa shilingi 16 Za Tanzania ni 1 ya kenya, sasa hivi ni around 21 tsh ni 1ksh so almost zinarudi parity. Upo sahihi.
 
Back
Top Bottom