Nimepitia mengi katika maisha. Pamoja na juhudi kubwa za kusoma na kuwa na akili nyingi, bado naishi maisha magumu na yenye kudharaulika.
Nina familia na watoto, lakini nahisi kama mke wangu haniheshimu tena baada ya yeye kujipatia mafanikio. Nahisi muda wowote anaweza kufanya uamuzi mgumu dhidi yangu kwa sababu kauli zake ni ngumu kuelewa. Nahisi kama nilishapoteza mwelekeo siku nyingi zilizopita.
Nimepata hasara nyingi kwenye mambo mengi niliyowekeza. Ingawa nimeajiriwa, nahisi hakuna kitu ninachoweza kufanya ili kuboresha hali yangu. Zaidi ya hayo, madeni niliyonayo yanazidi kunisumbua. Siwezi kufanya jambo lolote la kumuumiza mtu mwingine, lakini mara nyingi nashutumiwa kwa vitu ambavyo sijafanya au sikuhusika navyo.
Kwa kweli, ninakabiliwa na changamoto nyingi sana, na sijui nifanye nini ili kuboresha hali yangu.