Ninaamini katika hizi tu ili mtu aweze kuongoza nafasi ya juu kabisa ya madaraka ya nchi lazima awe amesoma walau taaluma moja kati ya hizi

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
3,791
10,833
Wakuu asalaam.

Binafsi naamini siasa ni sayansi na wanasiasa ni lazima wawe wanaweza kuimonitor na kuiishi sayansi hii ya siasa. Ili MTU yoyote aweze kuungoza umma wa watanzania ni vyema akawa amesoma na kuhitimu angalau taaluma zifuatazo

1. Sheria
Hii ni kwa maana kuwa sheria ndo nguzo kuu ya utawala wa kiraia na kiongozi mkuu anapokuwa amepitia na kufuzu sheria anakuwa ni kiranja mkuu kwa sheria zetu.

2.Uchumi
Shahada ya uchumi ni kigezo muhimu sana kwa kiongozi kutawala taifa, lazima tuwe na kiongozi anaejua vizuri maana ya uchumi na namna ya kuupigania.

3.Diplomasia na mahusiano ya kimataifa.
Kiongozi bora lazima ajue umhimu wa mahusiano ya kimataifa, zama za umimi zimeshapitwa na wakati.

2020 Tutafute mtu mwenye uelewa wa mambo Haya tuache kummpa MTU madaraka kwa sababu ya ukali wake... Silaha ya kiongozi ni sheria, uchumi na diplomasia.
 
Uongozi ni kipawa, haitegemei sana aina ya elimu uliyosoma. Hu Jintao rais wa china aliyepita ni mhandisi wa mitambo ya maji, lakini ameongoza taifa lenye uchumi mkubwa na idadi kubwa ya watu duniani.
Yule nae ni dikteta tu.
 
Paul kagame kasomea nini?

Rais bora kuliko wote Nyerere ni Mwalimu kwa taaluma.. na jembe linalojenga stieglers gorge kipenzi chetu wananchi nalo kama nyerere vile ni mwalimu kwa taaluma...

Ushindi wa kishindo unakuja..

Zamani mlikuwa mnatembelea nyota ya wamachinga na mama ntilie kupata amsha amsha kwenye kampeni..

Jembe la chato ni kipenzi cha wamachinga, mama ntulie na wanyonge wotee nchi nzima...sijui mtapatia amsha amsha za uchaguzi wapi mwaka huu
 
Kwa 'Uwasilishaji' wako tu huu unaonekana hizi ni Moja ya Kozi zako ulizosemea na wenye Akili tumejua kwanini umeanza na hiyo ya Sheria Mkuu.
 
Sasa IDD AMINI anaweza kuwa na jambo gani la kujivunia zaidi ya kujenga jeshi la kuvamia nchi nyingine, kuuwa watu na kupora ardhi!
Kujenga jeshi pia ni uongozi. Siyo kazi rahisi kuunda kikundi na kuwa kitiifu.
Wenyeviti wa vyama vya siasa nchini kwetu wengi hawana taaluma ulizozitaja hapa. Wenye nazo wameshindwa kuzitumia barabara. Hivyo uongozi wa ummma ni kipaji ambacho mtu anazaliwa nacho na kukiendeleza kukijenga kupitia jamii inayomzunguka.
 
Kiongoz mwenye taaluma ya ualimu hapaswi kuongoza nchi ,maana wananchi atawaongoza kama wanafunz
 
Tanzania tungekua tumejenga mifumo thabiti na kusimamia kwa dhati malengo ya kitaifa U-Rais ungekua ni taasisi hivyo mtu yoyote hata wasanii wa Bongo movie wangeweza kua Rais na maendeleao yakaonekana.
Tatizo kubwa tulilonalo hatuna malengo makuu kama taifa,na kama yapo kila Rais anayeingia anakuja na malengo yake,kwa namna hii tutateseka sana mpaka Wananchi watakapojitambua maana wao ndio wanaomuweka Rais madarakani.
 
Tanzania tunabahati ya kuongozwa na waalimu halafu nyongeza yake uwe na jina la Mwisho lenye M au hata uwe na moja ya majina yenye K . Haha.

Mfano: Julius .K. Nyerere JK.

Jakaya Mrisho Kikwete JK.

Ali Hassan Mwinyi. (M).

Benjamin Wiliam Mkapa. (M).

John Magufuli (M).

Rais wa awamu ya sita naye jina lake litakuwa na (M).
 
Back
Top Bottom