Nina wasiwasi huenda nimeshatapeliwa

Dec 13, 2023
51
185
Wakuu bila shaka mnaendelea vyema.

Baada ya kuwaza Thread 'Nawekezaje bumu linisaidie kulipa ada?' Nawekezaje bumu linisaidie kulipa ada?

Nikaona thread ya jamaa humu akielezea kwamba unaweza kuanza biashara ya kuagiza vitu abroad kwa mtaji mdogo.

Niliagiza bidhaa kwa alibaba nikawapa hawa transport agents wanajiita shamwaa.

Wakuu ni mwezi sasa sijapata bidhaa yangu japo niliagiza kwa ndege, nikalipia kila kitu.

Kama walivyoandika ratiba za ndege zao kwenye website kwamba ningepata kwa siku mbili , lakini sioni dalili yoyote ya kupata mzigo wangu hadi sasa.

Kila nikiwapigia wananiambia wiki ijayo, hio wiki ijayo nayo ikifika wanasema hivohvo, .

Wakuu naombeni ushauri wenu.
 
Shamwa hawawezi kutapeli mzigo wako. Je ulipata received notes kutoka kwa shamwa kuwa wamepokea mzigo wako? Kama ndio mzigo uko sehemu salama. Mm nawatumia tangu wanaanza kazi hii mpk sasa kiongozi.kwa meli na ndege.
Kama uko Dar nenda ofisini kwao.
 
Mimi walinitumia invoice kwa whatsapp nilipie, labda kuna namna nyingine ya kunijulisha?, mkuu kwa ndege wewe huwa inachukua muda gani, ama ni hatua zipi unapitia hadi unapata mzigo wako.
 
Ila watanzania bwana! Wakati unafanya yoote hayo hukuomba ushauri Wala kufanya tafiti wa kina. Leo limekukuta ndio unatafuta msaada!

Ila nadhani ondoa hofu mwezi mmoja Bado sio kipindi kirefu Cha kutisha.
Mkuu niliomba ushauri sana kabla sijaanza hii, nilisoma sehemu nyingi lakini pia niliweka uzi humu kuomba ushauri. Thread 'Mwenye uzoefu na kuagiza simu ndogo kupitia alibaba' Mwenye uzoefu na kuagiza simu ndogo kupitia alibaba
 
Mimi walinitumia invoice kwa whatsapp nilipie, labda kuna namna nyingine ya kunijulisha?, mkuu kwa ndege wewe huwa inachukua muda gani, ama ni hatua zipi unapitia hadi unapata mzigo wako.
Umeshaambiwa fika ofisini kwao, sasa mkuu mtaji ndo huo unategemea unashindwa kufika ofisini au hata kuagiza mtu upate majibu ya kueleweka?
 
Wakuu bila shaka mnaendelea vyema.

Baada ya kuwaza Thread 'Nawekezaje bumu linisaidie kulipa ada?' Nawekezaje bumu linisaidie kulipa ada?

Nikaona thread ya jamaa humu akielezea kwamba unaweza kuanza biashara ya kuagiza vitu abroad kwa mtaji mdogo.

Niliagiza bidhaa kwa alibaba nikawapa hawa transport agents wanajiita shamwaa.

Wakuu ni mwezi sasa sijapata bidhaa yangu japo niliagiza kwa ndege, nikalipia kila kitu.

Kama walivyoandika ratiba za ndege zao kwenye website kwamba ningepata kwa siku mbili , lakini sioni dalili yoyote ya kupata mzigo wangu hadi sasa.

Kila nikiwapigia wananiambia wiki ijayo, hio wiki ijayo nayo ikifika wanasema hivohvo, .

Wakuu naombeni ushauri wenu.
Shamwaa hawawezi kukutapeli, nawatupia sana Hawa jamaa
 
Back
Top Bottom