Nina mtazamo kwamba uchumi wa Tanzania unapoteza thamani kwenye soko la fedha

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,663
Ki ufupi ni kwamba viashiria nnavoviangalia vinaniambia kwamba uchumi wetu wa fedha unapoteza thamani.

Tangu mwaka uanze riba za kuwekeza cash zimeshuka kwa kiasi kikubwa. Average return ya interest income ya ku invest kwenye cash liquid assets kama bills na fixed deposit ni around 9% annualized.

Wakati kipindi cha nyuma interest returns kwenye cash assets ilikuwa inacheza kwenye mpaka 18%.

Meanwhile inflation yetu ipo around 6.5 mpaka 7%. Ikimaanisha kwamba the real return of investing in Tanzania liquid cash assets ni only around 2%.

Hapo hapo sasa hiv bank nyingi zimeshakuwa risk aversive kwamba zimekuwa wagumu kuto mikopo kulingana na hali ya ki uchumu ilivo ambapo NPLs za ma bank mengi zinakuwa kwa kasi kubwa.

Kwa maana hiyo gharama za kukopesha kwa sasa in real terms zipo juu mno. At the same time hali ya ki uchumu imekuwa sio ya kuridhisha.. Biashara nyingi hazitengenezi returns za kutosha kama kipindi cha nyuma.

Nimeamua kufikiria sana hichi kitu.. It seems our economy ipo kwenye trap moja mbaya sana.

Nimesoma uchumi lakini hizi situation sijawahi kuzi observe hata kwenye theory yoyote, hata sijawahi kuona uchumi unao behave kama wetu kwa sasa.
- Riba za kuwekeza zimeshuka 5-9%
- Inflation around 6.5 - 7%
- Riba za kukopa zipo juu mno na mazingira ya kukopeshwa magumu.
- Bei ya hisa kwenye soko la mitaji nayo ipo chini haijawahi kushuhudiwa. Na sellers ndo wana dominate market kila mtu now anataka atoke.
- For over a year now public sector haijatoa ajira zozote significant kwenye labour market kama ilivokuwa kipindi cha nyuma.
- Ukuaji wa private sector nao umekwenda chini na performance yake sio nzuri. Profit imekwenda chini na ajira zilizokuwa zinatolewa pia zimekwenda chini.

Nahisi kama nchi yetu ipo kwenye janga kubwa la kiuchumi ambalo lipo against na theory zote za kiuchumi.

Kwa hali ilivo, tunahitaji proper mix ya monetarist na keynesian actions (increasing govt spending) tuweze kutoka hapa tulipo.

Bado naichambua bajeti nijue kuna strategies zipi za kutuokoa. Hapo ndo ilipo Keynesianism.. Kwenye monetarism serikali lazima ihakikishe pesa inarudi tena kwenye mzunguko kama zamani.

So inatakiwa iumize kichwa ni jinsi gani itafanya speed ya growth ya money supply iwe kubwa na ya kutosha.

There is no way unaweza ku boost production wakati money supply ipo inakuwa kwa mwendo wa kinyonga.. No way nooooo way..
 
Asante mkuu kwa elimu ya uchumi master
Hali ya uchumi ni tata nchini kwa sababu ya mfumuko wa bei na sera ya ubanaji matumizi wa serikali hasa ukizingatia Nchi imetilia mkazo kwenye kodi
 
Binafsi zilipoanza tu fununu kuwa serikali haina hela nilipanick kimtindo japo sijui mengi kuhusu uchumi ila kama watu hawana hela na serikali haina hela kuna shida sehemu
 
Asante mkuu kwa elimu ya uchumi master
Hali ya uchumi ni tata nchini kwa sababu ya mfumuko wa bei na sera ya ubanaji matumizi wa serikali hasa ukizingatia Nchi imetilia mkazo kwenye kodi
Mbaya sana.. Na uchumi ukishadondoka mpaka uje kurudi ile level uliyokuwa mwanzo huwa ina take time...

Uchumi kuanguka ni mara moja ila kuja kuinuka na kuwa ulipokuwepo sio kesho wala kesho kutwa.

Mfano kwa sasa tulipo mpaka tuje tufikie ile standard ya uchumi iliyokuwepo mwaka 2014 itaweza kutuchukua mpaka 2020.

Na hapo ni kama kutakuwa na strategies za maana na sio kama hizi sarakasi za kila siku.

Magu amefanya structural changes za haraka ndani ya muda mfupi ambayo ki utawala na ki sera kwenye mambo ya kiuchumi haikupaswa kwenda kwa speed hiyo.

Matokeo yake ametibua kila mhimili wa kuendesha uchumi.
- Katibua shughuli za uendeshaji wa ki bank.
- Katibua mfumo wa kodi
- Katibua economic diplomacy
- Mfumo mzima wa biashara umetibuka
- Ametibua mfumo wa uongozi wa hizi taasisi.. Hii panga pangua kila uchao sio nzuri hasa kwenye sector nyeti kwa nchi kama Tanzania inayotafuta stability ya kutekeleza plans, sio jambo zuri hata kidogo...
 
Binafsi zilipoanza tu fununu kuwa serikali haina hela nilipanick kimtindo japo sijui mengi kuhusu uchumi ila kama watu hawana hela na serikali haina hela kuna shida sehemu
Kuna mfanyakazi wa serikali kakosa mshahara? Magari ya serikali yamekosa mafuta? Viyoyozi haviwashwi tena kwenye maofisi ya serikali? Hiyo dalili ya kufilisika serikali iko wapi? Kuna miradi mingi inaendelea kujengwa zikiwemo ofisi kadhaa za serikali zikifanyiwa ukarabati. Juzi tu serikali imepeleka vivuko vipya kikiwemo MV kazi cha kigamboni. Unajua nchi ambayo ina dalili za kufilisika au yenye hali mbaya kifedha?
 
Yeah kuna benki na biashara zimefungwa kutokana na hali hii
 
Serikali inayofilisika mawazo na mipango utaona vyote kwenye decisions zao..

Kutumia mabilioni ya walipa kodi kununua ndege wakati ungeweza ku allocate the same money kuboresha huduma za afya vijijini ni moja wapo ya maamuzi ambayo yatazidi kutugharimu
 
Inafilisikaje wakati inanunua ndege kwa pesa cash? Afya ni tatizo la muda mrefu tokea awamu zilizopita kununua ndege ndio kusababishe afya kutetereka mbona tulipokuwa hatuna ndege afya bado ilikuwa haina kiwango kizuri?
 
Wewe ni kilaza je haujui kuna watu wanamiaka nane kazini hawajapewa pesa za likizo??juzi tu tumesikia kwenye bajeti ya wizara ya ulinzi unaambiwa wanajeshi hawajapewa pesa zao za likozo na wengine wanadai pesa za uwamisho na madeni mengine vp wewe unaongea hivyo???Tubu bro
 
Yeah kuna benki na biashara zimefungwa kutokana na hali hii
Na sio za mwisho.. Kuna hii inaitwa TIB siku si nyingi itajibu tu.. Utawala wowote usio heshimu principles za kiuchumi kwenye kufanya decisions lazima ufeli..

Na ubaya principles za ki uchumi always zinakwenda kinyume na mihemko ya mwili.

Kama kuna option mbili

1. Kununua tractor
2. Kwenda kutalii kwenye fukwe za Ibiza na kukaa mwezi mmoja.

Other factor remain constant.. Optimal decision ambayo ni chungu ni kununua tractor kwa sababu ni capital good na inaweza kutengeneza utajiri ikitumika kwenye matumizi ya msingi.

Ila ukiruhusu mihemko ya mwili itende kazi, utatumia ulichonacho kwenda ibiza kula raha, ukiamini kabisa kama ni tractor basi utanunua wakati mwingine.

The same same kwenye decisions nyingi za sasa.. Mambo ya msingi yanayohitaji uharaka hayapewi kipaumbele kinachofaa, yale yasiyo ya msingi na muhimu ndo yamepewa kipaumbele.

Lazima tuumie tu
 
ushauri unaotolewa na wanazuoni wachumi serikali inauzingatia kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…