Nina damu group O+, Ufafanuzi kuhusu group hii

nanjanga

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
330
111
Nimepima leo group la damu yangu, nina group 0+ Rh,

Nini faida ya hili group na hasara zake, na je naweza kumpa damu mtu wa group gani?

Nitashukuru nikisaidiwa mawazo, asante.

Kwa faida yetu sote nitaeleza kila group la damu:
Kwanza kuna Magroup 8 ya damu nayo ni: A+, O+, B+, AB+, A-, O-, B-, AB-

(1) GROUP A+
Anauwezo wa kutoa damu kwa mtu mwenye: A+ na AB+
Anauwezo wa kupokea damu kwa mtu mwenye: A+, A-, O+ na O-

(2) GROUP O+
Anauwezo wa kutoa damu kwa mtu mwenye: O+, A+, B+ na AB+
Anauwezo wa kupokea damu kwa mtu mwenye: O+ na O-

(3) GROUP B+
Anauwezo wa kutoa damu kwa mtu mwenye: B+ na AB+
Anauwezo wa kupokea damu kwa mtu mwenye: B+, B-, O+ na O-

(4) GROUP AB+
Anauwezo wa kutoa damu kwa mtu mwenye: AB+ TU
Anauwezo wa kupokea damu kwa mtu mwenye: KWA KUNDI LOLOTE

(5) GROUP A-
Anauwezo wa kutoa damu kwa mtu mwenye: A+, A-, AB+ na AB-
Anauwezo wa kupokea damu kwa mtu mwenye: A- na O-

(6) GROUP O-
Anauwezo wa kutoa damu kwa mtu mwenye: KWA KUNDI LOLOTE
Anauwezo wa kupokea damu kwa mtu mwenye: O- TU

(7) GROUP B-
Anauwezo wa kutoa damu kwa mtu mwenye: B+, B-, AB+ na AB-
Anauwezo wa kupokea damu kwa mtu mwenye: B- na O-

(8) GROUP AB-
Anauwezo wa kutoa damu kwa mtu mwenye: AB+ na AB-
Anauwezo wa kupokea damu kwa mtu mwenye: AB-, A-, B- na O-

Hii ni kwa mujibu ya mitandao ya afya.

Kwa ishu ya RH+ na RH- (RHESUS FACTOR) naona mdau Helcobacter Pylori kalielezea vizuri sana kwa lugha rahisi kueleweka.

NOTE: MITANDAO YA JAMII IKITUMIKA VIZURI NI MSAADA MKUBWA SANA KWA JAMII
 
Hujaelewa somo, mke akiwa - ve na mme naye -ve ndio tatizo. Sasa wewe - ve na mmeo + ve huoni kama Kuna tofauti kwenye Rh factor?? Group O hasa +ve ndio kindi la damu lililo ngangari kwa kujikinga na magonjwa na hata vvu hufanya kazi ya ziada kushambulia kundi hili. Mtu mwenye group hili akipata vvu havimsumbui na akikuambukiza mwenye group jingine kama A, B au AB lazima muondoke ila yeye atakuwepo. Mara nyingi hawa huwa hujulikana kama carrier
 
Back
Top Bottom