Nina 40,000 Nifanye nini ifike 80,000 ndani ya siku 7

Unataka ifike 80 ili ufanyie nn? Watu tunaweza kukusaidia kama ni kitu cha maana
 
1.nunua jiko la mkaa-choma maindi jioni
2.kakodi banda (ulipe kwa siku) kisha uza matunda
3.azima brenda kwa jirani kanunue matunda kisha tengeneza juisi-utembeze
4.Kama Mkoa uliopo kuna shida ya maji kodisha mkokoteni kwa siku nadhani ni 2000 kisha kanunue madumu 6 ubebe maji upeleke penye uhitaji.
5.Kanunue mboga za majani tofauti tofauti kutoka kwa wakulima-ukauze sokoni.
6.Kalangue miwa kisha upange kwenye kijisenta uuze.
7.tengeneza mandazi ukauze kwenye shule za msingi na sekondari.
 
Vijana wana shauri kubeti tu, acheni ujinga mazee huko ku bet ni kurisk sana.
 
Inawezekana lakini weka aibu pembeni na uwe tayari kuwekeza juhudi..

Kanunue mahindi mabichi na jiko la mkaa, weka barabarani anza kuchoma mahindi.
 
Back
Top Bottom