huku halmashaur ya mkalama hatuna waalimu jaman maguful amamu hii tuangalie na sis jaman tunajua kuwa mazingra ya huku haya feviHuku Biharamulo sasa ndo balaa, shule tano ambazo zipo karbu na halmashauri ambazo ni Kagango, Rubondo, Bisibo, Ruziba na Biharamulo sec mwaka huu ajira mpya zmepewa walimu karibia 30 na kupanda juu na walio wengi ni wanawake. Huku shule za ndani ndani zkipata walimu watano, wakizidi sana ni saba. Hii inatokana na rushwa iliyokithiri pale Halmashauri pamoja na wafanyakazi wa halmashauri kuwagegeda hao mabinti. Yaani sasa hivi walimu wanagawana topic hasa masomo ya sanaa, hii ni hatar kwa ustawi wa Taifa.
hilo, unalosema kweli lipo kweli hata kwenye halmashauri zetu....
walimu, wengi wanaokuja kuripoti wanakuja na vimemo na wengi tunaoshia porini
Hii Si hoja.Nani afanye kazi vijijini.Atueleze Ni wapi mwajiriwa wake aliwahi mueleza kwamba atafanya kazi mjini tu.
Ni miaka mingi sana nchi yetu haijafanikiwa kutatua moja kwa moja uhaba wa walimu nchini, zaidi walimu wapya wameendelea kuajiriwa kila mwaka na idadi wa walimu tarajali imeongezeka siku hadi siku... wengi wamejiuliza je ni kweli walimu hawatoshi? hao wanaoajiriwa kila mwaka wanaenda wapi? SASA NATUMBUA JIPU
ukweli ni kwamba upangaji wa walimu katika shule umetawaliwa na uhuni mkubwa, walimu wanapangwa shule kwa kujuana, utakuta wilaya moja kuna shule (hususani zile za mjini au karibu na barabara) zina walimu wa kutosha (wakike wakiwa wengi) huku shule nyingine zikiwa na walimu wachache (na nyingine hazina mwalimu hata mmoja wa kike) nitaandika siku nyingine kwanini walimu wa kike wengi wanapangwa karibu na halmashauri lakini kwa leo hebu niendelee kupasua hili jipu....
sasa wakati ajira za walimu zikitangazwa walimu wanapokuja kuripoti wanakuja na "vimemo" tayari wanapangwa shule za town na vijijini wanapangwa wale wanyonge... hivyo kama jipu hili lilisipotumbuliwa ipasavyo shule nyingi zitaendelea kuwa na walimu wachache daima na milele.......
jipu nimelipasua najua kuna walioumia lakini hebu tumsaidie raisi wetu haya majipu...
kwa yule ambaye anabisha afanye utafiti wake wakati wa ajira mpya za walimu 2016
wachanijimwage sasa naweka wazi kwa wilaya ya kilindi japo takwimu ndogo tu ya walimu kwa shule chache ninazo zifahamu za mjin na kijijini SEUTA sekondari ina walimu 42 shule niya kutwa kidato cha kwanza hadi cha Nne tu...Nkama sekondari nayo inawalimu 34..Mafisa sekondari inawalimu 25...pagwi sekondari inawalimu 9...kikunde sekondari inawlimu karibia 20...kibaoni sekondari walimu 5.sasa najiuliza hawawalimu 42,34,20 wengine wanafundisha kweli?..na taarifa nilizo zipata ni kwamba walimu wanagawana topic zakufundisha wakati shule zingine hazina walimu kabisa wa hayo masomo wanayogawana topic....NAFIKISHA TU MWENYE KULIA NA ALIE UKWELI NDIO HUO..Mtindo wakupangiana vituo vya kazi kwa kujuana SIO MZURI kabisa watanzania wote ni sawa hakuna alie zaliwa ili aishi mjini wala kijijini jawani kazi kwa HAKI na sio upendeleo...
Mleta mada anasema ukweli mtupu,wengine tunapiga pindi hivyo hivyo tu,tena kwenye mazingira magumu,tunaishi kifalsafa na kisaikolojia zaidi,wanaume watupu na ni wachache kazi kubwa.
mbona muhimbili alipeleka vitanda rais magufuli kwani ile kazi ya kuleta vitanda wizara haikuona....mie namuamini magufuli kuwa anaweza kufanya kazi peke yake hata kama hakuna wizara.....tunachosema ni kwamba mgawanyo wa post za walimu uzingatie uhaba wa walimu kwa shule husika sio uhuni uhuni tu.....haiwezekani walimu mshahara ni ule ule lakini kwa walimu wa vijijini wanagawana masomo mengi tena mengine ambayo ata hawakusomea na mjini wanagawana topic tena engine subtopic....BASTARD ORGANISMTuliaminishwa kuwa Ualimu ni wito, acha kulia lia & fanya kazi. Wewe kama hupataki huko bush, unataka nani aende?! Hamuwezi kulingana hata siku moja, ndo maisha hayo. Anyways, hiyo sio kazi ya Rais ni kazi ya Wizara husika; Wasiliana na wizara.