Mmea Jr
JF-Expert Member
- May 20, 2016
- 829
- 1,972
Siku ya tarehe 19 ,, mpenzi wangu aliniomba kiasi fulani cha pesa ,, nikaona nitumie mwanya huu kupima kiasi cha upendo alicho nacho mpenzi wangu ..
Nilimpatia kiasi alichoniomba bila tatizo lolote lile .. alipofika siku ya tarehe 20 ambayo ni pasaka .. muda wa saa tano nikamtaarifu mpenzi wangu kuwa naenda kupokea mzigo katika moja ya ofisi fulani za mabasi yaendayo mikoani ambayo huwa tunaitumia kuagiza na kupokea mizigo yetu na bila tatizo akanitakia safari njema .
Ilipofika muda wa saa saba nikiwa na mshikaji wangu nikaona acha nimpe mtiani huyu bidada .. nikampanga mshikaji wangu ajifanye askari ,, afu atumie simu yangu kumpa taarifa mpenzi wangu kuwa wamenikama na nipo kituo cha kati cha polisi ,, hivyo anatakiwa afike haraka kituoni hapo akiwa na sweta au koti pamoja na chakula , maelezo zaidi atayapata hapo hapo kituoni ..
Basi siku ikapigwa , ikapigwa pale huku kidume nikiwa nimetulia pembeni nikisikiliza muitikio au reaction ya huwa mpenzi wangu ..
Baada ya sekunde kadhaa simu ikapokelewa na maongezi yao ikawa kama ifuatwavyo
Askari
(Wachongo ) : haloooo
Bidada : haloo
Askari : samahani ,, unaongea na askari mwita toka kituo cha kati ,, nimekupigia kukupa taarifa kuwa bwana (mmea ) tumemkamata yupo kituoni baada ya kuanzisha fujo katika ofisi za mabasi za (jina la kampuni ). Hivyo tulikuwa tunaomba ufike haraka kituoni
Bidada : samahani mimi nipo mbali sana ,, nipo mkoa mwingine
Mpigie kaka yake inaitwa (jina ) namba yake ipo humo humo kwenye simu
(Hapa bidada aliongea hivi sauti ikiwa kavuuu hamna mshutukio wowote ule alionesha kuwa anaezungumziwa ni mpenzi wake ambaye yupo kwenye matatizo )
Askari : kwani wewe si mkewe ?? ,, maana tumeona wewe ndiyo unaonekana kuwa mtu wa karibu sana na huyu bwana ndiyo maana tumekupigia wewe ..
Bidada : hapana mimi rafiki yake tu wa kawaida ..
( Hapa alinikana kata kata kama petro alivyofanya kwa yesu ,,, daaa !! Hii sehemu iliniuma sana moyoni )
Baada hapo ,,, nilipata jibu kuwa kumbe bado nipo peke yangu ,, nipo gheto nimechill,, siku ya pili leo kwenye buffer ngoma inayolia ni ya harmonize ~ im single