Nimetapeliwa ajira za wanaojifanya ni World Vision Tanzania

munguwetusote

New Member
Aug 15, 2023
2
3
Habari wanajamvi wenzangu. Pasipo kupoteza muda wa mtu yeyote, nipende kushiriki nanyi juu ya huu mtindo wa utapeli wa ajira/nafasi za kazi zinazotangazwa kila uchwao. Naamini kupitia uzi huu, wanajamvi wengi watapata elimu ambayo itaweza kuwasaidia kwa namna moja au nyingine.

Kumekuwa na tangazo katika majukwaa mbalimbali ya ajira linaloonesha nafasi za kazi za muda wa miaka miwili katika idara mbalimbali ndani ya shirika la World Vision Tanzania. Tangazo lilionekana kuchapishwa na kuthibitishwa na Afisa mtendaji mkuu wa shirika hili kwa kuwa na sahihi yake na muhuli wa shirika. Muda wa mwisho wa kutuma maombi kwenye shirika hili kwa njia ya barua pepe ya shirika wvt-recruitment@wvi.org na nyingine wvt-recruitment@hotmail.com ilikuwa ni 31/11/2023. Baada ya muda wa siku kadhaa kupita, tumepokea majibu ya maombi ya kazi tuliyoomba kupitia jumbe za simu na barua pepe zilizothibitisha kuwa maombi yetu yamekubaliwa, hivyo kushare namba ya whatsapp 0759259330 kuhakikiwa kabla ya siku ya alhamisi 21/12/2023 ili kupangiwa kituo cha usaili. Namba hii ya whatsapp inaonekana ni namba iliyosajiliwa na kuthibitishwa na META kutumika kama business account kwa ajili ya shirika hili la World Vision, kitu ambacho sicho kirahisi kufanikisha kama hutokuwa na legal documents to determine your eligibility. Naomba tuelewane hapa wanajamvi wenzangu, ili kuweza kusajili "To officially migrate/register your whatsapp account to whatsapp business management platform to help you engage audiences, accelerate sales or drive better customer support" ni lazima uwe na legal docs ambazo zitasaidia META wathibitishe taarifa zako na kusajili account yako. Kwa maana hii huu mtandao ni mkubwa sana. Mawasiliano ya whatsapp ni chanya kiasi cha kutokuwa na dukuduku juu ya hili swala kwa sababu kuna muda niliombwa kutuma baadhi ya vyeti nilivyotumia kuomba kazi kwa barua pepe tajwa hapo juu ili kufanya uhakiki wa taarifa nilizotuma kabla na sasa, nikajaribu kutuma docs tofauti ili kuona kama wanaweza kutambua au laah, aise bwana hawa majamaa ni hatari maana walinitaka nitume vyeti kama vile nilivyotumia kuomba kazi kwa barua pepe tajwa hapo juu. Then baadae nikapokea ujumbe wa kuonesha kuwa uhakiki umekamilika hivyo niwasiliane na mratibu wa kituo hicho cha kazi nilichopangiwa kufanya usaili kwa namba 0683937065. Jamaa akasema niwe kituo cha kazi tarehe 22/12/2023 saa mbili asubuhi. Mchakato wote huu umehusisha matumizi ya fedha za kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo jingine, utumaji wa taarifa binafsi za mtu ikiwa pamoja na vyeti na vitambuli huku wengine wakitoa vilio kuthibitisha kuzulumiwa fedha ambazo walitakiwa kulipia kama nauli za kuwafikisha vituo vya kazi ambavyo vipo pembezoni sana na miji walipofikia.

Hoja ni kwamba inawezekanaje mtu nje ya mfumo wa kazi husika awe na email ID ambayo ni web based mail ya shirika? Ok, labda ni mtu alikuwepo ndani ya mfumo ila akatolewa, sasa kwanini awe na uwezo kuendelea kuwa na access ya resources like mail servers na nyaraka muhimu za ofisi husika?

Ukijaribu kufanya mawasiliano na namba za shirika, wanasema hao ni matapeli na mpaka sasa siyo chini ya watu 3000 wametapeliwa. Sasa kwanini shirika lisichukue maamuzi yakufungua kesi ya uharifu ambayo itasaidia kuipa mamlaka husika kuwatafuta watu hawa na kuwatia mbaloni? Je, ni haki kuambiwa wew binafsi kama muhathirika ukatoe taarifa polisi halafu mamlaka itajua utaratibu wa kufuata? Ulinzi wa taarifa binafsi za mtu huko wapi?

OMBI
Ombi langu ni kuiomba mamlaka husika kulivalia njuga swala hili maana mpaka sasa limekuwa kidonda sugu kisichoponeka. Tunahitaji ulinzi wa taarifa zetu binafsi maana hawa watu wanaweza tumia taarifa hizi kufanya ubadhilifu au uhalifu na kutufanya sisi tuingie katika hali ngumu ya mikono ya sheria

Natanguliza shukrani na poleni kwa uzi mrefu ambao unaweza kuwa umekuchosha kwa kusoma lakini ni muhimu kwa baadhi ya vijana na watu mbalimbali wanaopambana kujitafuta na kusaidia familia zao.
 
Then baadae nikapokea ujumbe wa kuonesha kuwa uhakiki umekamilika hivyo niwasiliane na mratibu wa kituo hicho cha kazi nilichopangiwa kufanya usaili
☝🏿...Inawezekana vipi kupangiwa kituo cha kazi kabla ya interview? Je, umetuma hela ya nauli kwa logic ya wao kuja kukusafirisha?

USHAURI: mashirika yote ya kimataifa likiwemo World Vision hayawasiliani na watahiniwa kwa WhatsApp na maombi ya kazi yanatumwa kupitia WorkDay. Tulishauri mara nyingi Sana hapa kuwa Nafasi yeyote ya kazi unayotakiwa kutuma hela (hata TSH 500) ni utapeli.
 
Wewe ni kilaza, world vision wanatumia email ya hotmail toka lini
Kuna Barua pepe 2 hapo juu moja official nyingine mchepuko

nadhani wametumia ujanja sana baada ya kugundua watu wamestukia e mail zisizo za Kampuni
 
Wewe Ni mjinga hizo e-mail zinaonesha kabisa za kutapeli. Pia kuwa verified Meta unatakiwa kulipia Ada peke yake. Unatakiwa kujitafakari
 
Mtu una smartphone ina google umeshindwa kujiongeza tu lakini bado unatapeliwa kirahisi mno kama mtoto wa kindergarten!
 
Mtu una smartphone ina google umeshindwa kujiongeza tu lakini bado unatapeliwa kirahisi mno kama mtoto wa kindergarten!
mpaka leo Jeshi la Polisiti linatoa tahadhari tusitume ela wala kufuata maelekezo. Mpaka leo malalamiko ni mengi yanayoomba serikali kupitia tcra na jeshi kudhibiti matapeli. Hoja yangu...watanzania tulio wengi ni vilaza. Tunatapeliwa kwa ujinga wetu na sio vinginenvyo. Tunaamini tuishatapeliwa serikali itaturejeshea tulichokipoteza kwa kuwa ni jukumu lake
 
Watanzania wengi ni wajinga sana ni rahisi kuwatapeli.
Mtoa mada na wenzake walioibiwa wana akili finyu(Low-minded).
 
Kuna jamaa yangu alinipigia simu akaniuliz kaka hv hiz ni ajira za kweli?
Unajua kwann alinipigia kwa kuwa mm kwa sasa nipo ndan ya shirika hilo, basi nikamwambia hata mm nimeziona lakin katika website zetu zote wala pages hata groups hakuna hiyo kazi kwahiyo usijaribu utalizwa.
Basi akanambia nilikuw nataka kupata uhakika ili nisiyakanyage.

Anyway
WVT wana mfumo wa pool, na careers ukion tangaza nje ya hapo umeliwa

Na lingne huwa wana kupa option ya kuapply through Workdays site tu yaan huko kwingn unaend kulizwa
 
Kuna jamaa yangu alinipigia simu akaniuliz kaka hv hiz ni ajira za kweli?
Unajua kwann alinipigia kwa kuwa mm kwa sasa nipo ndan ya shirika hilo, basi nikamwambia hata mm nimeziona lakin katika website zetu zote wala pages hata groups hakuna hiyo kazi kwahiyo usijaribu utalizwa.
Basi akanambia nilikuw nataka kupata uhakika ili nisiyakanyage.

Anyway
WVT wana mfumo wa pool, na careers ukion tangaza nje ya hapo umeliwa

Na lingne huwa wana kupa option ya kuapply through Workdays site tu yaan huko kwingn unaend kulizwa
Workday ni mfumo gani na unafanyaje kazi? Tafadhali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom