Nimeshituka baada ya watu kuanza kuniamkia na kuniita mbaba

Omopa

JF-Expert Member
Nov 26, 2022
260
1,244
Aisee hamna kitu kinachoninyima usingizi kama watu mtaani kuanza kuniamkia na kuanza kuniita mbaba sasa najiuliza kwanini waniita mbaba na kuanza kuniamkia ila nahisi miahafikia umri wa utu uzima natakiwa kuacha kufikiria kuhusu maisha maana sio kwa kasi hii ni maisha na utu uzima kiukweli unakuja less mpaka naogopa ndugu zanguni

Sijui nifanyeje ili nisionekana mtu mzima ili watu wasiniamkia na kuniita mbaba naombeni ushauri cha kufanya kiukweli nakua moodless kiukweli na kukosa usingizi(insomnia) aisee
 
Nilichokuja kugundua umri ukisogea kwanza unakua hauamini amini, kuna wakati unapewa shkamoo unaanza kujiuliza mbona kama niko sawa nae huyu, au mbona kama nimempita kidogo tu .
Hayo yote yanaletwa kutokana na kutojua/kukubali umri ukienda ila baada ya mda unaelewa na maisha yanaendelea
 
IMG-20240925-WA0000.jpg
IMG-20240925-WA0000.jpg
 
Wewe unakitambi in short bonge Fulani hivi, lazima utaitwa mapema sana mbaba.
Mimi mwenyewe ni mshangazi ila Kuna namna nimejiweka bado naitwa mdada

It's all about daily lifestyle
Fanya mazoezi
Pata muda wa kusali as a part of meditation
Jipende
Furahi
 
Ndiyo maana Mimi mwenzio ninakata laki kila mshahara kwaajili ya scrub na kupaka pico ,siko tayari kuitwa mbaba au kupewa salamu za kitumwa sijui shikamoo .
Kuhusu kunyanzi ni mwendo wa kujisugua na magadi na majivu ,sitakula kuzeeka kizembe hivyo
 
Back
Top Bottom