Nimeota nadaiwa USD. 6000/ kwa kulala siku 3

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,735
15,197
Hii ndoto nimeitafakari sana Na sijaielewa. Nimeota niko kwenye nyumba Fulani nzuri sana, ndio naamka kitandani. Nikaanza kujiuuliza hapa ni wapi?

Nikaingia washroom, nikapuuh kisha nikasema nitoke nje huenda nikajua niliko.

Kiunoni Nina taulo tu, nikawaona mabinti wamekaa kwa nje, nikawa najificha wasinione, nisije kupigiwa kelele za mwizi.

Basi nikafanikiwa kutoka pale, upande wa kulia kulikuwa Na jengo lingine, akatokea mlinzi Na kuniulizia naenda wapi? Nikamjibu nipo tu, akaniambia nimekuwepo kwenye jengo hilo nimelala mfululizo kwa siku Tatu bila kuamka.

Hivyo nafaiwa dola elfu sita kwa hizo siku Tatu. Nikatoka Na taulo langu nikamwambia mlinzi nikirudi nitakuja kulipa, nikazama mtaani Na taulo langu ndio nikashtuka.

Ndugu zangu naombeni tafsiri
 
GGen Z wa Tz.
 
Kama uliziona PAMPERS eneo la tukio baada ya kushindwa kulipa ujue Haina maana nzuri
 
kuota tu dollar tayar we tajir
 
Mzee kazi unayo kama una appointment na demu ya kulala nae lodge/hotel cancel utanishukuru.
 
Ulipopuuh tu ndiyo ulipoagana na utajiri. Ulikuwa mtego, na taulo ni kwamba utavaa malonyalonya. Mkuu badili ID tu...
 
Kuota unatembea Na taulo ni Jambo la aibu, utakumbwa Na aibu
 
Ulipopuuh tu ndiyo ulipoagana na utajiri. Ulikuwa mtego, na taulo ni kwamba utavaa malonyalonya. Mkuu badili ID tu...
Poop dreams are often a symbol of spiritual release. Pooping/seeing poop is a sign that your problems, though messy, are out in the open. In several cultures, poop dreams are a sign of prosperity. Seeing an animal's poop in your subconscious is a good omen of upcoming wealth
 
Thumb up
 
Ngoja nijaribu;
Unadaiwa milioni 13,800,000/= za kitanzania na HESLB.
Iliyokufadhili kwa miaka mitatu ya masomo yako.
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
Sikusoma kwa mkopo, Zama zile tunasoma serikali ilikuwa ikitupatia ruzuku Na si mikopo. Mikopo imekuja juzi tu hapa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…