Nimemuelewa Rais Magufuli, sasa namuunga mkono

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Rais John Pombe Magufuli na serikali yake wamewashika watanzania. Wameamua kufanya jambo moja kubwa kisiasa:kujitangaza. Kila tendo au neno la Rais au wa chini yake linatangazwa. Kama si luningani,redioni basi litachomoza gazetini au hata mtandaoni. Uongozi matangazo!

Kujitangazatangaza huku kunawafanya waamini kuwa serikali inafanya kazi na Ilani inatekelezwa. Wananchi wanaoneshwa,kutangaziwa au kuandikiwa maagizo,maelekezo,teuzi na hata maigizo yasiyo na ujuzi. Ilimradi wananchi wasiache kusikia,kusoma au kuona.

Kauli hazitoi nauli. Vyeo havileti maendeleo. Lakini,kusemasema na kutajwatajwa kuna uzito wake wa vito kisiasa. Viwanda vitajengwa na kuoneshwa. Tanzania ya viwanda yaja!Vyombo vya habari,ni muda wenu kuajiri wengi kwakuwa kila kiongozi atataka filamu yake ionekane na kutamba. Naunga mkono ubunifu na usanifu huu maarufu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Zanzibar)
 


WALIOKUWA WANATAKA KUUZA SURA KWENYE TV WAKATI WA BUNGE LILOPITA NI WAKINA NANI KAMA SI UKIWA, sasa coz unawaza ki ukiwa ukiwa unadhani na wengine ndio hivyo,... hapa kazi tuuu, longo longo peleka ukiwa
 

Uongozi matangazo? I love this one.
Nitaishushia na lager, wallah!
 
sijaona chochote kilichofanywa na serikali hii zaidi ya porojo na matangazo kwenye media ni full maigizo na watz ni vipofu wa fikra na wao muda wote wako kwenye media kuangalia leo kuna tangazo gan
 
Na Rais baada ya kuona Clouds wamepunguza speed akaona aruke nao hewani kipindi cha 360.
Wakati wengine wanaambiwa wawahi kazini yeye yuko na mama chumbani wanaongea na mtangazaji wa studio.
Na bado senema ndio zinaanza, kama Isidingo vile
 
hapo ndo ushange sasa, maana pamoja na kujinasabukwenye media kuwa ukusanyaji wa mapato umeongezeka maradufu, bado hospitali hazina dawa, hakuna vitanda, shulen madawati na vyumba vya madarasa havitoshi pamoja na matatizo mengine rukuki, sasa hiz hela zinazokusanywa sjui nani anakula
 
sijaona chochote kilichofanywa na serikali hii zaidi ya porojo na matangazo kwenye media ni full maigizo na watz ni vipofu wa fikra na wao muda wote wako kwenye media kuangalia leo kuna tangazo gan

unakaa kwenye computer unafunga macho alafu then unafungua ukute ghorofa imetokea hapo mbele yako ghafla ndio utasema magufuli kafanya kitun( no miracle in development but the dev. is processes moving from one stage to another), wewe mwenyewe umefanya nini tangu magufuli achaguliwe,
 
Nyumbu wewe
 


hivyo uwezi fanya kwa mkupuo kaka(development sio miracle bali ni process) embu mpe muda baada ya miezi tisa tuu, hata kama ni wewe pale nyumbani kwako uwezi pata kazi tuu baada ya miezi mitatu tukuone unaporomosha nyumba, laasha kwanza utaanza kuziba kwanza maden, kurekebisha mlo ndio uanze kujipanga vizuri kujenga na kadhalika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…