Nimemuacha Mume wangu kwaajili yake yeye hajali kanitelekezea watoto wake!
Hapa ofisini kuna kaka mmoja ni mwalimu mwenzangu. Wakati naajiriwa alinikaribisha vizuri sana kiasi kwamba alihangaika kunitafutia nyumba, na kipindi hicho nilikuwa na changamoto kidogo ya kipato hivyo alinikopesha ila baadaye akaniambia hapana, hakuna haja ya kulipa. Basi tukawa marafiki, anakuja kwangu mara kwa mara, nampikia, mara nyingi analeta kila kitu mimi sitoi hela yangu.
Mimi nimeolewa, tangu kumaliza chuo mwaka 2016 nilikuwa sijaajiriwa mpaka mwaka juzi ndio nilipata hii kazi na kupangiwa mkoani mbali na mume wangu. Mume wangu anahudumia vizuri tu, alikuwa ananijali ila kipindi nahama kuna pesa alinipa nikafanyia mambo mengine hivyo nikashindwa kumuomba tena.
Baada ya kuanza kupata mshahara, mume wangu aliacha kunihudumia kwa sababu watoto walikuwa kwake kwani walikuwa shuleni, hivyo tulipanga nikishaweka vizuri huku ndio tutawahamisha. Aliacha kunitumia pesa na mimi sikumuomba kwa sababu kipato chake si kikubwa ukiangalia chakula na kulipia ada watoto 3, niliona si sawa kumwambia wakati nina mshahara.
Lakini kama unavyojua wanawake, ukipata mwanaume anakujali unachanganyikiwa, nilikuwa namuonea wivu mke wa huyu kaka kwa sababu nilikuwa nawaza jinsi anavyonijali hivi, sijui mke wake anamfanyia nini. Yeye ana pikipiki hivyo alikuwa ananibeba kila siku, anakuja kunichukua nyumbani, yani mpaka ikafika kipindi mke wake akajua kuwa niko na mwanaume wake. Aliponiuliza nilimtukana sana na akatishia kumtafuta mume wangu nikamwambia amtafute tun a namba nakutumia, kwakiburi nilimtumia namba ya mume wangu kwani nilikua sijali, nilijua kama utani ila aliscreenshot meseji na picha nilizokuwa natumiana na mume wake, akamtumia mume wangu.
Mume wangu alipogundua aliniuliza, nilijua kabisa kama huyu mwanaume ananipenda na atamuacha mke wake na kunioa mimi, nilimuambia wazi kuwa kama anataka kuniacha aniache ili aache kunifuatilia. Alinitumia talaka huko huko na mimi sikujali, niliishia kumtukana mpaka eda ikaisha sikuomba msamaha.
Mwanaume alipojua kuwa mke wake kamtafuta mume wangu, aligombana sana na mke wake, alim*piga mpaka mwanamke akaondoka na kumwachia watoto wawili. Mimi nilizidi kufurahi kwa sababu niliona kabisa nimeachiwa mume. Kwa kuwa wote tunaishi nyumba za kupangisha, mimi nilirudisha nyumba na kuhama kwake kwa sababu yeye nyumba yake ni kubwa, na alikuwa anaishi na watoto wake wawili.
Nina miezi 3 sasa naishi hapa kwake lakini mwanaume kabadilika. Hanihudumii kwa chochote, naishi na watoto wake tena mmoja ni mgonjwa kila siku hospitalini lakini mwanaume hata mia hatoi. Yale mapenzi aliyokuwa ananipa hayapo tena, kibaya zaidi nina mimba yake nakaribia kujifungua lakini mwanaume hata mia ya kujifungulia hatoi.
Naomba ushauri nifanye nini, nimempigia simu mke wake aje kuchukua watoto wake hajajibu chochote, zaidi ya kucheka tena kwa dharau. Ninatamani kuhama hata hapa lakini sijui nifanyaje, nimeharibu ndoa yangu na yeye hata hajali, ndio kwanza kurudi nyumbani ni asubuhi!
Msaada!!