Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 14,085
- 28,695
Tangu mjadala wa makubaliano ya Tanzania na Dubai kuhusu masuala ya uwekezaji ikiwemo bandari uanze, hadi sasa sijaona mtu aliyesema kuhusu ubaya wowote wa kipengele cha mkataba na akakidadavua vizuri kisheria nikamuelewa.
Mimi ni mwanasheria, nimesoma mkataba, nimesoma maelezo ya Serikali kuhusu mkataba kusema kweli sijaona hoja za wanaopinga zaidi ya kuelezea hofu zao na tahadhari zao.
Leo nimemsikiliza Padre Kitima ambaye nae pia ameelezea hofu yake kuhusu mkataba ikiwemo vifungu kadhaa. Kusema kweli hakuna alipoweza kusema kuhusu mapungufu ya kipengele chochote zaidi ya kuelezea hofu yake na kuweka tahadhari
Padre Kitima ameelezea kuhusu suala la Ardhi na kusema kweli hakuna sehemu katika mkataba paliposema mwekezaji atamilikishwa ardhi. Nilitegemea atakisema hicho kifungu na kukisoma ila nimemsikiliza zaidi nimeona nae kapiga siasa tu. Kwa nilivyokisoma kifungu cha 8 (3)(b) cha mkataba kimesema wazi haki za kutumia ardhi zitatolewa kwa mujibu wa Sheria na taratibu zetu na inajulikana kwenye sheria zetu mwekezaji hapewi haki ya kumiliki ardhi ila haki ya matumizi tu ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji( derivative right)
kuhusu ulinzi na usalama wa bandari. hakuna kipengele chochote kwenye mkataba kilichosema mwekezaji atasimamia masuala ya ulinzi na usalama katika bandari. hata mwekezaji aliyepita tics aliyekuwa anaendesha sehemu ya bandari yetu hakuwahi kusimamia masuala ya ulinzi na usalama. Hapa pia Padre wangu Kitima ameelezea hofu tu na wala sio ubaya wa mkataba kwa kudadavua vizuri
Kuhusu Serikali kuwataarifu Dubai kuhusu fursa zingine za uwekezaji (Ibara ya 4) kusema kweli sijaona tatizo lolote kuhusu kifungu hiki. Ningeelewa kuwa kuna tatizo juu ya hichi kifungu endapo kingesema Serikali italazimika kuwapa maeneo hayo baada ya kuwataarifu. Sioni tatizo lolote kuhusu mtu kutaarifiwa tu kuhusu fursa zilizopo. Kwenye hili naona tafsiri isiyo sahihi na hofu isiyokuwepo inayolazimishwa kuwepo.
Mwisho ameelezea sehemu wawekezaji hawa walipofanikiwa na kuna sehemu amesema hawajafanikiwa. Hili sioni kama ni hoja maana mifano mizuri inaweza kuwa kwetu
Mwisho Padre Kitima amesema kuhusu Loliondo. Kusema kweli hapa naona amekuwa mwanasiasa maana sioni hoja yake kuhusu watu waliopelekwa msomera kulalamika kwa sababu hata kwa watumishi wa Umma waliopelekwa Dodoma wapo waliolalamika na kusema wanapata changamoto Dodoma! Sasa ninachojiuliza ni Je kwa wale waliolalamika inamaanisha zoezi la kuwahamishia watumishi wa serikali Dodoma halikuwa zoezi zuri lenye maslahi mazuri kwa nchi?