Tajiri wa matajiri
Senior Member
- Apr 17, 2024
- 166
- 640
Nimemfumania MKE wangu na mwanaume mwingine, nimemsamehe lakini hataki kurudi!
Mimi ni kijana wa miaka 40, nimeoa na ndoa yangu ina miaka 15 sasa. Wakati nakutana na huyu mke wangu, wote tulikuwa bado wadogo na ndiyo tumemaliza chuo. Ni mtu ambaye tumekua pamoja, na kila kitu kilikuwa vizuri.
Mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kupata kazi. Baada ya kupata kazi, tulikubaliana nimchukulie mkopo mke wangu tufungue biashara. Kweli nilifungua biashara ya duka la vyombo kwani ni kitu ambacho mke wangu alikuwa anajua sana, hasa kipindi tuko chuoni kama aliuzia hiyo biashara.
Mambo yalikuwa vizuri, na mpaka sasa Mungu ametujalia watoto wanne. Mke wangu ni mtu ambaye nilikuwa namuamini sana. Anasafiri kwenda kuchukua mzigo, anaenda anapotaka bila hata kuniaga, lakini mimi nachukulia poa kwa sababu najua kuwa hawezi kufanya kitu kibaya.
Mwezi wa sita niliona kuna mabadiliko, mke wangu alianza kuwa mkali sana na mara nyingi alikuwa akikumbusha makosa yangu ya zamani. Ndoa ina miaka 15 lakini kipindi cha uchumba, wakati tuko chuoni wote, kuna mahusiano nilikuwa nayo, kwamba niliwahi kumchanganya mke wangu na rafiki yake. Ulikuwa ni utoto, na tuligombana mpaka tukaachana, na baada ya hapo nilimuomba msamaha na kumuahidi kuwa hicho kitu hakitajirudia tena.
Kweli nilijuta na niliona umuhimu wake kuwa ni mke wa kuoa, na tulirudiana mpaka tukamaliza chuo, tukatafuta kazi na nikaamua kumuoa. Hajawahi kunikumbushia kwa miaka 15 yote ya ndoa na hiyo ishu tulishaiacha. Hata wakati mwingine tukikutana na huyo rafiki yake tunacheka tu, lakini hata hajawahi kuniambia kuwa hicho kitu kinamkera. Alipoanza kuzungumzia hicho kitu nikawa na wasiwasi kuhusu kuwa kuna kitu. Sina kawaida ya kushika simu yake, lakini nilianza kumfuatilia. Niliposhika simu yake, nilichokutana nacho huwezi kuamini.
Mke wangu ana mahusiano na kaka mmoja ambaye wanafanya biashara pamoja. Wanasafiri wanalala chumba kimoja, hata kununua mzigo wananunua pamoja, na wanakopesha pesa bila kuniambia. Na ubaya ni kwamba huyo mwanaume mara nyingi anakuja kwangu na namchukulia kama rafiki. Mke wangu alishawahi kupeleka mpaka watoto wangu kwa huyo mwanaume.
Soma Pia: Msaada wakuu, nimekamata SMS za mke wangu akichati na kijana mdogo mambo ya ajabu
Kweli nilipaniki na nilim*piga sana. Baada ya hapo aliondoka kwa hasira na kwenda kwao. Mimi sikujali, ila baada ya kama siku nne hivi akili yangu ilirudi, nikajua nimefanya makosa. Kwamba pamoja na kuchepuka, lakini ni mama wa watoto wangu hivyo sikupaswa kumuadhibu vile. Nilijutia, nikamtafuta kwenye simu ila akaniambia kuwa yeye hawezi kurudi.
Nilienda mpaka kwao na kuongea na mama yake. Nikamwambia tuna watoto, nimeamua kumsamehe ila akagoma. Nikaongea na baba yake, akaniambia kama ni kumsamehe basi nimsamehe kwa maandishi, niandike kuwa sina kinyongo na kitu kibaya kikimtokea niwajibishwe. Nilifanya hivyo. Mke wangu akaniambia ondoka, nitarudi, lakini sasa hivi inakaribia mwezi hajazungumzia mambo ya kurudi wala nini!
Ni kama vile hataki kurudi. Nikimpigia simu anakuwa kama mkali hivi, yaani nachanganyikiwa. Ukiangalia tuna watoto, ni mwanamke mtafutaji, tumeishi vizuri mambo mengi amenisaidia. Vitu vingi tulivyo navyo ni juhudi zake. Sio kwamba ananizidi kipato au anajihudumia, hapana, nimemzidi sana kipato. Pamoja na yeye kuwa na biashara, sihitaji pesa yake ila nafikiria wanangu wataishije bila yeye. Kila siku wananiuliza mbona mama harudi, nakosa jibu. Nisaidie nifanye nini mke wangu arudi, nimsahau kila kitu.
MIMI: Mwanaume, kama unaona kuwa wanawake wanakusumbua, kuanzia kukutongoza mpaka kukuheshimu, kama mke wako anaweza kuchepuka na ukachanganyikiwa hivi, basi soma kitabu changu cha “SIRI 11 Za Kumfanya Mwanamke Kukuheshimu Na Kukupenda.” Huna haja ya kulialia sana, mwanamke habadiliki kwa kulialia na kulalamika. Anabadilishwa kwa kumuonyesha uanaume wako.
MWISHO