Nimelipia cheti cha kuzaliwa hadi leo hamna, vijana walinihakikishia control number ikitoka tu basi

Anonymous Caller

JF-Expert Member
Sep 8, 2016
678
860
Salaam kwenu wabongo wenzangu,

Bila kupoteza muda naomba Kusaidiwa ushauri kama ifuatavyo;

Ninataka cheti cha kuzaliwa cha binti yangu wa nje mwenye miaka 13.

Nilipewa procedures kwamba niombe mtandaoni.

Kwa kuwa nilikuwa bize ilibidi hilo jukumu niwape vijana ktk steshenari fulani wanisaidie kwa charge ya elfu sita.

Niliwapa kadi ya clinic (copy)
Barua ya uthibitisho toka shuleni sikuwa nayo kwani mtoto huyo siishi nae.. anaishi na mama yake huko mbali

Mara control namba ikatoka.
Wale vijana wakanambia nikalipe kwa wakala au benk.

Kesho yake asubuhi nikalipa 20,000 na risiti nikapewa vizuri tu.

SASA cha kushangaza hadi Leo cheti hamna.. wakati wale mayanki walinihakikishia kwamba control number ikitoka tu Baaasi.

Nafanyaje sasa au ndo nimetapeliwa.

Je refund ipo kama nikighairi..maana naona naunguza muda wangu bure.
 
Kama sehemu ya kuchukulia hicho cheti n tofauti na sehemu hospital alipozaliwa yaan mikoa tofauti hapo usubiri mana kinaandaliwa wilaya ya hospital alipozaliwa.

Pengine aliyepokea ombi la usajili kalipokea halafu kaenda likizo hivyo mpaka arudi.

Ushauri nenda Rita wilaya unapochukulia hicho cheti wape namba waangalie watakwambia shida ipo wapi Kwan cheti ni ndani ya siku tano za kazi za Serikali.
 
Cheti cha kuzaliwa mtihani kukipata yaani mimi mwenyewe hadi nimekata tamaa, nishadhurumiwa sana, tunaomba mamlaka husika wekeni mazingira Rafiki namna ya kukipata hicho cheti, hebu rahisheni mambo ili kupunguza Nenda rudi kumbe mnatengeneza mazingira ya Rushwa.
 
Kila mtu anaweza kufungua akaunti eRITA na kuomba cheti cha kuzaliwa mwenyewe bila kwenda kwaa mkuu wa wilaya wala stationery,ni rahisi sana inakubidi uwe na smartphone au laptop tu na bando lako tu.
 
Jamaa hao wa Rita ni wapuuzi tu,kuna kipindi nilifuata cheti cha mwanangu wakasema kimepotea(kwenye ofisi yao sikuwahi kukabidhiwa)
Wakaniambia niende polisi nitoe taarifa nipate rb alafu niende nikaanze process upya na nilipie tena
 
Salaam kwenu wabongo wenzangu,

Bila kupoteza muda naomba Kusaidiwa ushauri kama ifuatavyo;

Ninataka cheti cha kuzaliwa cha binti yangu wa nje mwenye miaka 13.

Nilipewa procedures kwamba niombe mtandaoni.

Kwa kuwa nilikuwa bize ilibidi hilo jukumu niwape vijana ktk steshenari fulani wanisaidie kwa charge ya elfu sita.

Niliwapa kadi ya clinic (copy)
Barua ya uthibitisho toka shuleni sikuwa nayo kwani mtoto huyo siishi nae.. anaishi na mama yake huko mbali

Mara control namba ikatoka.
Wale vijana wakanambia nikalipe kwa wakala au benk.

Kesho yake asubuhi nikalipa 20,000 na risiti nikapewa vizuri tu.

SASA cha kushangaza hadi Leo cheti hamna.. wakati wale mayanki walinihakikishia kwamba control number ikitoka tu Baaasi.

Nafanyaje sasa au ndo nimetapeliwa.

Je refund ipo kama nikighairi..maana naona naunguza muda wangu bure.
Tatizo lako Una mkono mfupi Utateseka sana
 
Back
Top Bottom