Nimekuwa mgumu kutoa pesa kwa ombaomba

dr namugari

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
10,381
18,030
Hapo awali zamani kdg nilikuwa natoa Kia's Cha pesa na kuwapa omba omba na watu walemavu ,ila Sasa hivi Hali imekuwa tofauti kbsa nimejiona Kama Nina shida kdg yaani omba omba na walemavu wamekuwa wakifika hapa ofcn Kuja kuomba hata Kama IPO Mia 500 mezani nawaambia sina nakuwa mzito sana kutoa na kuwa na hofu ya chuma ulete.

Kisa mwaka Jana nilikuwa mitaa ya general iliko hospitali ya mkoa wa dodoma nikapita pale nikaitwa na mama mtu mzima akiniomba nimnunulie chakula kwani alikuwa ndani anasema hajaletewa chakula na ndgu zake Basi akanipanga Hadi na chakula anayo taka yeye kula wali nyama jumla elf 3k na mm nilikuwa na buku 3 nikatoa nikampa buku 2 atafute mwingine amuongezee buku ili akale anacho taka ktk mghahawa aliyonielelekeza jiranj tu.

Basi nikatoa hyo buku 2 yangu Kisha nikasogea mbele kdg napiga hatua naitwa na muuza machungwa Akaniambia broo mban nakutonya ulikuwa unioni ,nikamuuliza kwan vip ,ndipo akanimbia huyu mama aliyempa pesa ni tapeli haumwi Wala nn Ni Muda mrefu Yuko hapa anawaomba watu pesa kwa kujifanya anaumwa ,nilichukia sna kidg nirudi kuchukuwa pesa zangu.

Kwa dodoma omba omba ni wengi sna na hasa kutoka katka Hili kabila la wagogo wanapenda sana kuomba omba ,nimesikia Yuko radhi kuharibu macho yake au kujikata mkono ili aingie barabarani kuomba omba Ni wavivu mno kwa kufanya Kaz ,wasukuma wamejazana dodoma wanapiga kazi za ujenzi vzr sna

Swali: Je, wewE una moyo wa kutoa pesa kwa omba omba na kiwaango gani unaweza mpa?
 
wew una moyo wa kutoa pesa kwa omba omba na kiwaango gani
kama ni hawa unawazungumzia,


jibu ni hapana
 
kama ni hawa unawazungumzia,


jibu ni hapana
heeee
 
Hapo awali zamani kdg nilikuwa natoa Kia's Cha pesa na kuwapa omba omba na watu walemavu ,ila Sasa hivi Hali imekuwa tofauti kbsa nimejiona Kama Nina shida kdg yaani omba omba na walemavu wamekuwa wakifika hapa ofcn Kuja kuomba hata Kama IPO Mia 500 mezani nawaambia sina nakuwa mzito sana kutoa na kuwa na hofu ya chuma ulete

Kisa
mwaka Jana nilikuwa mitaa ya general iliko hospitali ya mkoa wa dodoma nikapita pale nikaitwa na mama mtu mzima akiniomba nimnunulie chakula kwani alikuwa ndani anasema hajaletewa chakula na ndgu zake Basi akanipanga Hadi na chakula anayo taka yeye kula wali nyama jumla elf 3k na mm nilikuwa na buku 3 nikatoa nikampa buku 2 atafute mwingine amuongezee buku ili akale anacho taka ktk mghahawa aliyonielelekeza jiranj tu

Basi nikatoa hyo buku 2 yangu Kisha nikasogea mbele kdg napiga hatua naitwa na muuza machungwa Akaniambia broo mban nakutonya ulikuwa unioni ,nikamuuliza kwan vip ,ndipo akanimbia huyu mama aliyempa pesa ni tapeli haumwi Wala nn Ni Muda mrefu Yuko hapa anawaomba watu pesa kwa kujifanya anaumwa ,nilichukia sna kidg nirudi kuchukuwa pesa zangu


Kwa dodoma omba omba Ni wengi sna na hasa kutoka katka Hili kabila la wagogo wanapenda sana kuomba omba ,nimesikia Yuko radhi kuharibu macho yake au kujikata mkono ili aingie barabarani kuomba omba Ni wavivu mno kwa kufanya Kaz ,wasukuma wamejazana dodoma wanapiga kazi za ujenzi vzr sna



Swali
je wew una moyo wa kutoa pesa kwa omba omba na kiwaango gani unaweza mpa
Soma " strength perspective theory " mwandish Albert Bandula.
 
Hapo ukimsachi mfukoni ana smart phone kali kuliko yako😂😂 watu wa kuwasaidia ni walemavu ambao hawawezi kufanya kazi. Huyo huwa nampa hela huku nikifanya maombi kimoyomoyo maana siku hizi mambo ya kiroho mengi sana. Mtu mwenye viungo vyote kamili sitoi. Labda awe mzee
 
Na usisahau zile mia 2 from omba omba znauzwa usku hata elfu 20 ....kwa wataalam wa sangatt....... Mm Nliacha zaman sana kutoa pesa labda msosi tuu...Huko kahama mtu unampa jelo anaenda kuiuza hata 10k....kwa wazee wa ndagu....
 
Ambacho sielewi omba omba wa Dodoma, utakuta omba omba yupo barabaran, mchana analetewa msosi na ndugu zake watu wazima kabisa hawana shida 😂😂😂😂 ile issue niliposhuhudia ilinikata sana maini 😂😂
😂😂😂😂
 
kuna kipindi mama yangu alikuja town alikua na harakati zake basi akapita nilipokua naishi alafu akaendelea na safari yake siku inayofuata kwahyo siku alipofika tulikwenda kkoo akanunua baadhi ya vitu akawa anawaona wale omba omba kwenye ukuta wa tbl kama unakuja karume akatoa karibu kwa kila aliemuomba mimi kimya.
basi jioni tukawa tunaongea akaniuliza unaishije hutoi kwa watu wenye uhitaji Mimi nilicheka nikamwambia nitajitahidi niwe natoa.

aliendelea na safari yake siku inayofuata na akarudi akapitia kkoo moja kwa moja kuchukua mazaga ya kurudi nayo home akapita mule mule alikotoa msaada sijui nini kilimkuta ila nilimkuta home ana mizigo ila simu pesa Hana hata nauli ya daladala hakubakiwa nayo nilibaki nacheka maana hajaibiwa na waizi ila anasema katoa msaada kwa mmama kapiga hatua tano au kumi hivi anataka asaidie mwingine anacheki pochi kavu kawaida ya mama wanakua na pochi kubwa na mdogo ya kuweka hela ngoma zimepeperuka na simu imeenda nilibaki nacheka sana...


siku moja tuko moshi mjini tunapaki tu akaja mtu na mwanae wanaongozana wakatuomba hela bi mkubwa ndio alikua wa kwanza kuwakata shombo nilijiskia vibaya ila nikakumbuka yalio mkuta nikacheka tu.....


sina mtindo wa kusaidia omba omba ila kuna wale watu anakuibukia anakuomba kakwama nauli au chakula hao hua nasaidia mara moja moja nafsi inaponituna kutoa yupo alierudisha fadhila ila muda mwingine naamini Mungu ananibariki juu kwa juu kulingana na pale nilipotoa
 
Kuna mmoja alipita dukani anasema hajala siku tatu ila kabeba bonge la furushi, ikabidi nimuulize nguvu za kubeba furushi kubwa lile kalitoa wapi maana njaa ya siku tatu sio mchezo 😂😂😂😂😂
 
RUVUMA kuna ombamba wapya kabisa uongo huu nilisanuliwa majuzi tu kuwa wakipita nisitoe pesa yyte maana walinuvuna haswa nikaapa sitasaidia ombaomba tena
1.Kukitokea msiba wao wanapita na picha ya marehemu kuonesha madai yao kuwa wanachangisha kupeleka msibani lakini hawafikishi wanagawana wenyewe kwa wenyew.niliapa sutachangia msiba tena kwa staili ile.
2. .Anasema katoka hospitality hana pesa ya malipo kulipia bill ya matibabu nanadaiwa hospital hajala na hana anauli..ukimuangalia anaafya njema kabisa

SICHANGII OMBAOMBA TENA walinivuna imetosha
 
Back
Top Bottom