Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,189
- 67,763
Anaandika, Robert Heriel
Sitaki matusi, hata Mimi najua kutukana Sana tuu! Kila mtu na maisha yake. Kwanza Niko na hasira Kama Simba mwenye njaa.
Taikon niliwahi kuleta uzi humu 👉👉 Nimesikitishwa sana! Kumbe mama mkwe kaweka CCTV camera kwenye nyumba aliyotupa
Wakwe zangu wakaniambia Mimi na Mke wangu tuhamie NYUMBANI wanaoishi, ukweni. Alafu Ile Nyumba waliyotupa tuipangishe ili tupate pesa za kujikimu Kwa sababu Mimi sina KAZI wala mke wangu Hana kazi. Tukaona wazo hilo ni Sawa. Unajua Masikini ni Kama mtu mwenye njaa tuu, kila atakaloambiwa ataitikia ndio ilimradi apewe Msaada.
Maisha mapya ukweni yakaanza, nataka niwaambie Vijana kutokanatna uzoefu wangu wa kukaa ukweni.
Ukweni usipokuwa na pesa wewe ni Kibarua tuu. Sio lolote, si chochote.
Taikon kibarua Ukweni ukiniita hivyo hutokuwa unakosea, hata hivyo sitojali kwani Mimi ilimradi naishi, nakula, Nakala. Basi nasubiri siku nitakaponyakuliwa.
Ukweni ni kama Jela, Mara nyingi Nyapara ni Mama Mkwe halafu Baba Mkwe na Bwana Jela.
Nadra sana kupatana na Mama Mkwe ukiwa Fukara, yaani lazima akutese Kwa kazi ngumu, hataki kukuona umekaa umetulia.
Wewe unaona maziwa ya ng'ombe ni matamu lakini sio kwa mimi Taikon, nimesombelea majani ya ng'ombe mimi, nimehenyeshwa na kusafisha mabanda ya ng'ombe mimi! Yaani zizi la ng'ombe linatakiwa liwe safi kama chumba cha binadamu.
Nikamwambia mama mkwe kuwa aache kuwadekeza ng'ombe wake. Hilo jibu alilonipa nilitaka liwe siri yangu lakini acha niwaambie ili iwe fundisho kwa vijana wengine, akaniambia; Hao ng'ombe ni bora zaidi yako, wanatupa maziwa na pesa, vipi wewe unatupa nini kama sio mzigo. Niliumia mno, haki yangu iko wapi? Taikon mbaroni ukweni.
Ng'ombe wasilie kidogo nitafurumushwa nikawambeleze ati kama watoto, wasilie. Mama mkwe wangu aliwahi niambie kipindi nafika kuwa ng'ombe wake wamesoma English Medium, nikastaajabu sana. Siku za mwanzoni walivyokuwa wanalia, akaniita kwa ukali; wee Taikon! Wee lofa!"
Nilipofika akaniambia, uhwasikilii ng'ombe huko nje?. Huelewi hata Kingereza, wanasema More! More!"
"More" nikahamaki.
Akaniambia wanamaanisha zaidi! Zaidi!
Duuuh! Kumbe Moo! Ni kizungu, hao ndio ng'ombe za mama mkwe!
Mama mkwe ni nyapara aliyeninyoa kupata. Ati nywele zinamaliza sabuni na zinahitaji Matunzo.
Hayo yote nafanyiwa mke wangu atafanya nini, Mwanzoni aliparangana na Mama yake lakini tulipotishiwa kutumuliwa ikabidi Mimi niingilie Kati. Najua Yule ni mtoto wao, Mimi ndiye nitakayetimuliwa. Hivyo nikamwambia mke wangu avumilie tuu.
Ukweni lazima uwe zoba, ukweni hakuna kufaga ndevu, ukweni hakuna kutoka kifua wazi, immi nakupa sheria za ukweni, unajua tayari ninauzoefu hivyo itifaki zote za ukweni nazielewa.
Ukweni sio kijiweni ati ulete stori zako za kijinga, labda uwe na pesa. Sisi mafukara stori atachagua Mkwe wako.
Ukweni huruhusiwi kucheka kwa kujiachia ati utoe lisauti la juu na kuinua miguu, ukweni usithubutu kufanya hivyo.
Maisha ya ukweni yakakolea Kama hadithi za Allan Quarterman, Taikon nikafunga mkanda kama mpanda nguzo za umeme kutoka Ifunda.
Zile tenzi na nyimbo nilizokuwa nikimuimbia mke wangu zikayoyoma, nitaimbaje nyimbo ya mahaba Ukweni, nitaimbaje tenzi tamu nikiwa jelani.
Mke wangu siku moja akiwa katika kifua changu tukiwa tumelala usiku akaniambia amemisi kuimbiwa, akasema sauti yangu nikiimba inampa Raha isiyokifani, nikasema sawa acha niimbe, nikasafisha koo kisha nikaachia Vocal;
" Karibu na wewe nisogee, karibu zaidi nikumbate,
Maneno matamu nikugee, moyoni mwako yanate,
Niwewe wapekee, twenzetu asteaste,
Mitego unitegee, Kama Ndege nikamate,
Nikushike ulegee, Kama mlenda kwenye mate,
Usoni nichekee, mdogomdogo nikuchakate,
Machoni usipotee, siku zote nikupate,
Eeh Ma:ma! Eeh Ma:ma! Nimekufa kilaini, rambirambi zichukue, eeh Be:be! Eeh Be:be! You're kiss inani-make nihisi Niko paradise! Ooh! Paradise! Nanana! Nana! Eeeh! Oooh!"
Wimbo huo niliuimba ukweni kumburudisha mke wangu, aliyekuwa anamimba ya miezi Saba hivi. Akanitazama Kwa macho ya Upendo alafu akatabasamu.
Ingawaje nilikuwa nateseka na mateso ya wakwe zangu Kutokana na kuwa sina pesa lakini mke wangu alikuwa faraja yangu. Nikiri kuwa mchana uligeuka jehanamu nikiwa na Harakati za kazi za pale ukweni, wakati Usiku ukigeuka kuwa Paradiso nikilifaidi penzi la Mke wangu.
Kikakonda nikakongoroka,
Nikachoka, nikasoromboka,
Mwanzoni mke wangu alikuwa akiniibia chakula na kuniita nije Nile chumbani kwetu kinyemela Hali hiyo ilinifanya niwe na rutuba Sana. Lakini baadaye hila yetu ikagundulika, mama Mkwe akatupiga Pini , hapo ndipo nilipoonja joto ya jiwe.
Muda wa Kula Kama sijamaliza kazi sili mpaka niwe nimemaliza kazi zangu. Na nikifanya harakaharaka ili nimalize Mama Mkwe ananiongezea kazi nyingine au anitume mbali na nyumbani. Doooh!
Nimerudi nimekuta wameninyima Vitafunio, Jana sikula kutokana na kuwaacha Mbwa watoke nje ya Geti.
Hata hivyo sina mpango wa kuondoka hapa Ukweni, mpaka nikamilishe Ratiba yangu na Ripoti yangu ili Kuwafunza Vijana na kizazi kinachokuja kuwa Ukweni sio pazuri kukaa ikiwa hauna kipato kizuri.
Utageuka Kibarua Kama barua isiyo na anuani.
Taikon nimemaliza, Leo sitaki maswali. Matusi Ruksa Ila tutapopoana, nimevurugwa na sina ustaarabu Kwa wasiowastaarabu. Kiboko yangu ni ukweni tuu. Ninyi wengine nawamudu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Ukweni, DAR ES SALAAM