Uwesutanzania
JF-Expert Member
- Feb 9, 2019
- 1,266
- 1,561
Nimefanya makosa makubwa na nimekukosea pakubwa imetosha sasa na nimeamua kukuomba msamaha popote pale ulipo.
Baba nimekua mjeuri kwako kwa kuzani kuna mahitaji ulipaswa kuyatimiza kwangu na umeshindwa kizembe,
Nilikuwa nawaza kuwa:
1) Kusomesha mtoto kwenye shule za gharama ni kitu rahisi
2) Kujenga mjini ni kitu rahisi na ulijisahau kwa hanasa za mjini
3) Kumiliki mashamba na viwanja ulizembea na kuendekeza starehe
4) Pia nilikuwa najua ni uzembe wako ndio maana hauna mali kama wazee wenzako, ni uzembe wako ukashindwa kumiliki gari, pikipiki, hata baiskeli
Baba haukupaswa kulaumiwa kumbe.
Sasa na mimi mwanao naanza kuzeeka na hakuna nilichounda katika dunia,. Nilichogundua ni kuwa Maisha ni ghali sana na hakuna mtu anayependa kufedheheka, ni Mungu tu mwenye umchagua nani asimame wapi na wapi. Sio kwa uzembe wako wala sio kwa ujanja wao.
Wala sio makosa ya baba wa mababa zako ma babu wa mababu zako ni Mungu tu mwenyewe.
Pia nimegundua kuwa hata kuihifadhi PESA yenyewe ni jambo kubwa sana katika dunia ya leo.
Unapata pesa kidogo mara mtoto anaumwa mke anaumwa mara madeni mara makesi mara PESA hakuna mara uzee nao HUO.
Baba haukupaswa kulaumiwa maisha ni MAGUMU mno.
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏

Usitafute excuse
Umaskini ni uzembe.
Umaskini NI Laana
Umaskini ni uvivu
Umaskini ni ûjinga
Umaskini ni DHULMA
Mungu hajawahi kumpangia Mtu umaskini. Huyo hatakuwa Mungu Bali ni kibwengo.
Binafsi Naamini MTU kuwa Maskini íwe NI Baba, Mama au Mimi mwenyewe Mungu hahusiki.
Na kama anahusika Basi huyo hastahili kuitwa MUNGU.
Baba au Mimi ninastahili kulaumiwa Ikiwa nitasababisha Umaskini.
Hapo anachofanya ni kumtetea Baba yako tuu ili kutafuta kichaka cha kujificha na kisingizio cha wewe nawe kuwa Maskini ili usilaumiwe na Watoto wako.
Umaskini pia unatokana na mfumo wa dhulma àmbao upo kwèñye jamii.
Kama Baba au kama kijana kitendo cha kukubaliana kuishi kwèñye mfumo unaomkandamiza ili awe Maskini ni Sababu tosha inayomfanya astahili lawama kwa kizazi chake.
Mungu Hana Muda wa kumpangia Mtu Mvivu, Mjinga, mzembe, na anayekubali kuonewa na kudhulumiwa.
Baba anastahili Lawama kama vile àmbavyo angepatia angestahili Pongezi.
Wenzako walivyokuwa wanashushwa na magari ya njano ulikuwa unawaonea gere eeh, ushakuwa umeyaona sasa.
Wengine toka udogoni tulitambua hali ya kweti, sikuwahi kumuona mama yangu kanifanyia dogo, mie vitu vingi saana nilikuwa naona ananifanyia kwa kujiumiza,
Nilikataa kununuliwa nguo za sikukuu nikiwa darasa la 4, nyumbani kuna watoto kibao, mara sijui wa mjomba, mara wa mama mkubwa, mara sijui wa nani, na wote anawajali kama wanae, hakuwa na ubaguzi, sikukuu moja nikamsikia anaongea na mama wa jirani sikukuu inakuja na hajui pakushika, jioni yale nikamwambia kuanzia leo, kuanzia sikukuu hii sitaki kabisa nguo za sikukuu, nikaulizwa kwaninj.
1. Sikukuu nguo zinauzwa kwa bei juu sana tofauti na uhalisia, hiyo pesa ikitumika siku za kawaida huwa napata nguo 3 mpaka 5 za kawaida na ni nzuri tu.
2. Siinjoi, kuvaa miguo ile na kuzurura kwangu ni kero, napenda kwemda beach niogelee tu.
Nikamshawishi akanielewa, kumbe lengo langu ni kumpunguzia gharama.
Bimkubwa katulia kisteringi saaana, ukizingatia dingi alikata moto mapema.
Mama yangu ni mtu special kuliko maelezo, ♥️♥️♥️