Nimejitahidi kuishi maisha ya umri wangu ila hivi vitu vimenishinda

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
6,002
19,433
Nimejitahidi kuishi kulingana na wakati na kuishi kwa umri wangu ila kuna vitu vimenishinda, sijui wengine wameviwezaje au wamevipendea nini.

1. Movies, nimejitahidi kuangalia muvi au filamu nyingi sana,za aina tofauti na ladha tofauti ila naona nimeshindwa,sielewi uzuri wake au utamu wa muvi ni nini au hasa lengo lake katika maisha ya binadamu ni nini.

Mfano unakuta muvi ina manyoka makubwa yanatembea juu ya gorofa au wanyama wakub wa kama mlima wanakanyaga magorofa, kwa kweli sijaona uziri wa muvi na zimenishinda.

2. Mpira, nimejitahidi kupenda mpira lakini nimeshindwa,nimejitahidi kuangalia mechi tofauti,ligi tofauti na kujua wachezaji karbu wote nione kama ntaupenda mpira ila imeshindikaa,wachezaji karbh wote nawajua waalimu lakini mwisho wa siku nimeamua kuacha,najikuta nashindwa kuupenda mpira.

3. Kwenda club, karibu club zote maarufu hapa nchini nilishaenda na nimeenda mara nyingi tu lakini najikuta kama nalazimisha aina ya maisha nayoishi,mwisho wa siku najikuta nikienda club kesho siku nzima sina furaha,najutia,sijui kwa kweli,mwisho nimeamua kuacha.

4. Pombe, sigara, na aina zote za madawa ya kulevya, hivi nashukuru sijawahi kuvijaribu katika maisha yangu na sina mpango huo.

Mimi hivyo vitu vimenishinda na nimejitahidi kuishi maisha ya umri wangu kama wengine lakini naona vimenishinda,sijui wenzangu mmewezaje au mnafanyaje, nilitamani hasa kati ya hivyo vinne nipende angalau kimoja cha club nacho naona kimenishinda, nimebakia nikitoka job naenda tu hom kulala. Sijuo hata nimekuaje.
 
Ukiondoa kipengele namba nne.

Kuanzia moja mpaka tatu.

Kweli nimeamini Watu/Binaadam tunatofautiana
 
Hauko pekee yako.
Mimi napenda kusikiliza mahubiri tu na hot discussion kwa watu walio na uwezo mkubwa wa uchambuzi.
Hapo utakuta hata tabasamu linatokea, nje na hapo sioni hata raha ya dunia hii.

Nahisi nitakuwa mhubiri.
 
mi muvi naangalia ila kwenye muvi ambazo za kufikirika huwezi ukanikuta naangalia, eti sijui mtu anapaaa kama ndege ...............
 
1.Penda kuangalia Movies za Kidaktari (Kuokoa Maisha) na za Kivita (Kuua)

Anza na movie inaitwa Lone survivor.

2.Penda Kwanza Mpira Wa kitaa, mfano anza na Abajalo Fc.. Nenda Ligi kuu ya Bongo.. Mfano Simba Sc.. Maliza ligi za ulaya.. Mfano Chelsea FC

3.Jifunze Kwanza Kudance na Kubambia, anza na nyimbo za kibongo, Nijeria, Kwaito, na Mwisho za Mbele... Usiende na demu wako kila siku.

4. Bangi itakufaa zaidi.

Kila la kheri Kijana
 
Mimi zaidi ya movie hamna kitu kingine napenda ila movies za kufikirika kama vampires siangalii,ila mi nadhan kuna kitu unakipenda sema hujakijua bado
 

aisee!
 
Kwenye muvi na mpira (michezo kwa ujumla wala sio siifa njema kutovipenda.

Naamini kwa sasa ndio umri wako wa kuvijua na kushiriki in positive way.

Maisha mafupi haya, but angalia umri usije kupita ndo ukaanza kuvipenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…