SOFTWARE Nimeikuta Play Store: Inaweza kuisaidia Jamii.

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
24,736
24,790
Kuna App nimeikuta Play Store inaitwa e-livestock Auction, inatoa huduma za kutangaza bidhaa za Mifugo na pia inakupa furusa ya kumpata Muuzaji Kwa njia ya Simu pia inakuonyesha umbali alipo na muda unaweza kutumia kumfikia.

Naona Masharti ya kujiunga ni ama kutumia namba ya simu ya mkononi ama email ya jamii ya google tu (Gmail). Kama hatuna email App inakuongoza kutengeneza email ili ujisajili. Mle unaweza kuuza kuku aina zote na mayai, ng'ombe, samaki, kondoo mbuzi, na Mifugo mingine!!

Kwa sababu masharti ya hapa hakuna kuweka link, nashauri kama unaona umuhimu kuangalia inavyofanya Kazi basi tembelea, Play store!

Naona ni kitu kizuri kinachoweza kuisaidia Jamii yetu Na Dunia kwa ujumla.

Nawasilisha!
 
Hongera kwa kutujuza wakulima na wafugaji wanaepushwa na vishoka/madalali wasopenda maendeleo ya wafugaji na wakulima
Madalali ni adui mkubwa wa wakulima/wafugaji. Unatafuta bidhaa, ambayo huenda iko kwa jirani tu mtaa wa pili lakini huwezi fahamu. mfano ungependa kufahamu bei, kiasi gani kinapatika na ni wapi mwenye bidhaa husika yupo. na kibaya zaidi, huenda usipate mahala pa kulinganishia hivyo vyote. Unaamua kumtafuta dalali.. anakupiga parefu kwa sababu yeye ndiye ana taarifa (information). Naamini hii app itabadilisha mambo mengi sana.. naomba tu wahusika waendelee kuiboresha na kui promote.. :LIKE:
 
campaign dec_9.png
 
Back
Top Bottom