Nimefarijika na hotuba ya Raisi.

Zee1

Senior Member
Jul 17, 2015
103
24
Kwa muda nimekuwa nikimfuatilia jinsi serikali ya JP Magufuli ikifanya kazi, inaleta matumaini ukifananisha na mtangulizi wake mzee wa Msoga. Jana kwenye hotuba yake amegusia mambo nyeti japo sio yote lakini unaona dhamira ya kweli ndani yake. Niwaase watanzania ugonjwa kuingia mwilini mwa binadamu ni rahisi sana lakini matibabu yanachukua muda. Na hata ukipona bado unahitaji muda wa ku recover! JP Magufuli yupo sahihi tumuombee na tumpe ushirikiano. Tumezidi kulalamika tafakari, chukua hatua nchi hii inakuhitaji wewe na mimi kutoka kwenye mkwamo.
 
Tuendelee kumuombea ili nchi hii aiongoze kwa hekima kubwa sana
 
"Jengo la Ghorofa nne limejengwa zaidi ya miaka 20 na halijaisha"-Magu
 
Kwa mara ya kwanza nitakuwa mzalendo kwa nchi yangu. Nitalipa kodi bila shuruti kwa sababu nimeona jinsi Rais anavyojitolea kuwa mzalendo wa kweli.
Hotuba yake ya jana ilikuwa inayogusa sana na sio zile za kuandikiwa kama alivyokuwa JK. Wito wangu tumuunge mkono jamani bila ya kujali itikadi zetu.
tumempata kiongozi ambaye anaongea kile kilichoko ndani yake na sio kwenye makaratasi. Mtihani pekee ninaouona ni mfumo uliokuwa proved failure kwa miaka zaid ya 20 akibalidili mifumo hakika atatuvusha vyema. Lets support him
 
Nchi hii sio masikini, sio ya kuomba misaada, nchi hii inatakiwa kuombwa msaada!! Duh Mungu amesikia kilio cha watanzania.
 
Tutofautishe kuna watu wantakiwa wafanye siasa ndio wale, je mimi na wewe siasa zinamsaada, tufanye kazi man wangu!
 

Zidumu Fikra za Mwalimu John Pombe Magufuri!
 
Nchi hii sio masikini, sio ya kuomba misaada, nchi hii inatakiwa kuombwa msaada!! Duh Mungu amesikia kilio cha watanzania.
He is a Visionary leader. JK hakuwahi kusema nchi hii ni tajiri alisisitiza ni masikini na kule ughaibuni akajibu hajui kwanini sisi ni masikini, ama kweli tulikuwa na white president miaka kumi iliyopita. Hongera kwa JPM kuliona hili kuwa sisi ni matajiri naamini hutakatishwa tamaa.
 
Watanzania wanaipenda nchi yao lakini walilazimishwa kuichukia na wakaichukia kweli kweli. Lakini sasa naona mwanzo mpya, fikra mpya. Nikuombe Mheshimiwa JP Magufuli kaza buti kidogo tena ili nidhamu ya nchi na hata majirani na nchi za magharibi waliotuzadharu watusalimie kwa heshima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…