Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 16,326
- 34,548
Duniani kote, Kanisa linalofahamika kuwakabili Waziwazi watawala dhalimu ni Kanisa Katoliki.
Kutokana na kuijua vizuri dunia, Wakatoliki hawajawahi kuwa sawa na uongo, hawajawahi kuwa sawa na udhalimu, hawajawahi kuwa sawa na Uzandiki.
Baada ya CHADEMA kuanzisha No Reform No Election, sasa ni rasmi agenda hii imekuwa rasmi Agenda ya Watanzania.
Kwa utafiti wangu mdogo niliyoufanya kuhusu maoni ya Wananchi tena wa kawaida kabisa, almost asilimia 98 wanakubali kuwa Chaguzi za Nchi yetu ni mazingaombwe na zinahitaji mabadiliko makubwa ili zifanywe kuwa huru na za haki. Ambapo tutapata viongozi wazuri wanaowajibika kweli kwa Wananchi ili kuwapatia maendeleo ya kweli.
No Reform No Election sio ajenda ya CHADEMA. Ni ajenda ya Watanzania wote wanaoipenda kweli nchi yao na kuiwazia mema.
Nikiwa najiandaa na pasaka, macho yangu yote nayaelekeza kwa Baraza la Maaskofu Katoliki TEC.
Kutokana na historia ya Kanisa Katoliki kupigania tawala za Haki duniani, naamini hawatawaangusha Watanzania.
Nategemea waraka mzito kutoka TEC, ambao utatengeneza a new road map kuelekea kuipatia Tanzania mabadiliko ya kweli.
Nategemea Waraka utakaosema Maaskofu Katoliki na Mapadre wako tayari kuunga mkono maandamano ya amani kudai Reforms za Katiba na Sheria za Uchaguzi ili kuipatia nchi yetu mifumo itakayowezesha tupate viongozi wazuri wanaowajibika kweli kwa Wananchi.
Nategemea baada ya Waraka wa TEC, Tutapata waraka kama huo pia kutoka KKKT.
Nategemea watu wa Mungu kweli, Watafanya jambo la maana mwaka huu na Tanzani tutaenda kupata Mabadiliko ya Kweli.
Mungu ibariki Tanzania.