Nimeamua kuvunja ndoa, mke kaniambia mtoto sio wangu

Sikununu

JF-Expert Member
Jan 27, 2015
341
100
Nilifika mkoa flani kutafuta maisha ambapo nilianza kwa kusua sua na hali ngumu ya maisha ndipo nilipokutana na binti mmoja ambaye nilimtokea akanikubali hivyo tukajikuta tunafanya ngono bila kinga kwa mara kadhaa.

Binti huyu alikuwa msaada mkubwa kwangu ikizingatiwa nilikuwa na hali ngumu ya kiuchumi ambapo alikuwa ananiliwaza sana na kunitoa kwenye sononeko la maisha, ghafla nilianza kupata mafanikio ndani ya mwaka mmoja na biashara zikaanza kuninyookea ndipo aliponiambia ana ujauzito (mimba) wangu nilipigwa na butwaa nisijue la kufanya lakini mwisho wa siku huruma na mapenzi nikamkubalia.Nilitoa huduma zote mpaka anajifungua mtoto ,niliamua kwenda kwa wazazi wake kujitambulisha ndipo tukaanza kuishi pamoja kama mume na mke

Nimepata mafanikio makubwa sana kwa kiwango cha kuridhisha katika umri wangu huu wa miaka 27 ambapo nimeshajenga nyumba nzuri na ya kisasa hapa mkoani na mashamba kama mawili nalimisha pia gari ya kutembelea pamoja na ya mama mtoto.

Mimi ni mnywaji mzuri sana wa pombe (kila siku lazima nitandike bia za kutosha) na kutokana na shughuli zangu nakua na campani kubwa ya mambo ya bata na hapa na pale,kuna siku tukiwa kwenye pombe na kilaji kuna jamaa akanijoke kwamba mimi nalea mtoto ambaye siye wangu na watu wote wanajua nilishtuka lakini nikajikaza kama sijasikia na utani huu ukajengeka kwangu ikawa kama mazoea.

Ndipo nikatafuta siku nikamuuliza wife kwa kumtega mbona huyu mtoto sijafanana nae na kwetu hajafanana na mtu yoyote,wife alijichanganya mwishowe akaniambia ukweli kwamba huyu mtoto sio wangu bali ni wa kijana mmoja kinyozi mimi nilimkuta tayari wapo kwenye mahusiano na yule kijana na pia kwavile aliikataa mimba na alivyoniambia mimi nikakubali basi ikabidi tuendelee.

Nilikasirika sana kama binadamu na kijana wa kiume nilitafakari na kumuuliza kama kuna mtu yoyote anayejua suala hili akanijibu hajamwambia mtu yeyeto hata wazazi wake hajawaambia,nikaamua kumsamehe na tukakubaliana tufanye siri maana tulishakuwa ndani ya ndoa.

Katika hali ya kawaida tunagombana isitoshe tabia yangu ya unywaji sana wa pombe haipendi lakini sasa nimechoka maana hata huyu mtoto wetu imefikia hatua anamwambia mbele yangu kwamba mimi sio baba yake na hatakiwi kuniita baba kwani baba yake si ameshamuonyesha,pia ananitukana matusi makubwa mpaka ya wazazi wangu.

Ninavyoandika hivi sijarudi nyumbani kwangu siku ya 5 na ninapanga kuvunja ndoa muda wowote maana huyu mwanamke ananidhalilisha sana pia nimepata habari leo amerudi nyumbani kwao kwa wazazi wake.
 
Pole sana ndugu, vizuri umeshaamua cha kufanya. Kweli amekudharau sana kwa maneno a-ayomwambia mtoto wa kinyozi.

Kwa hiyo nyumba ndio umemuachia au? Sababu hujarudi kwenye nyumba yenu...

Umeshaona sura ya baba mtoto?

Halafu kweli kabisa unasema eti ni siri juu ta mtoto wakati unajua sio siri, kweli wanawake wajanja kakuambia ukaamini huku unajua ni uongo wengi wanajua na kwao lazimaaaa.
 
pole sana mkuu ila nakushauri
1.usivunje ndoa
2.tuma mjumbe kule kwao ili akasuluhishe hili suala
3.tabia ya kunywa mno acha inakufanya ukose muda wa kukaa naye karibu ndo mana upendo wake kwako unapungua

anza na hayo kwanza
 
Mambo haya ni vyema kukubali maumivu ya miezi mitatu makali na ya kuchoma kuliko kukubali kufa pole pole ukijiona. Piga chini huyo japo utaumia sana kwa muda kama miezi 3 ila utapata mke mwema soon ni suala la kutulia tu
 
Jipange tu mgawane vitu hapo kila mtu asepe kivyake..Ni maisha tu haya mdau. Bado umri unaruhusu mambo yatakaa poa. Wanawake akili zao wao wenyewe hawazielewi.
 
Mkuu....
Nakushauri tena nikiwa sijalewa, nenda ukavunje hiyo ndoa aiseeee.....
Kubali hata kugawa nusu ya mali yako kuliko kuendelea na maisha ninayo yafanya kisha na kuishi na nyoka mwenye sumu ndani ya nyumba moja.
Bora ungemkuta na mtoto, hapo ungekua umeridhia kwa dhati kuishi na mwanamke ukijua mtoto sio wako.
Kimbia aiseee usije ukakutwa na masahibu kama yalio nikuta kipindi kileeee.....

Naomba niishie hapa aisee
 
Mbona Huyo mke anajiamini hivyo, mtoto sio wako na kukudharau juu mbele ya mtoto, itajenga picha gani mbele ya Huyo mtoto? Ukiona hivyo na yeye hajali kwa maamuzi yoyote utakayochukua, anza kivyako Bro, otherwise utaishi kimateso. Maybe itakuwa ngumu,but is for the best.umri wako bado mdogo, utapata mwengine tu.
 


Great ushauri....
 

Hapana nyumba sijamuachia nimeamua nikae peke yangu ili nitafakari

Kuhusu kufanya siri jambo hilo tuliliongea muda mrefu kidogo na hii nimejaribu kuunganisha habari nyingi...yaani nmechanganyikiwa sijui hata nisemehe I don't know what to do my dia

Baba mtoto nilishamuona na namjua
 
hahaaaaa umeoa au umejitambulisha sijaelewa

Kwani wewe ndoa unajua ni nini?
Siwezi kuelezea mambo yote hapa kusema nimeoa tayari inatosha coz nilifanya taratibu zote kwa mujibu wa kabila letu na lao kwa kuwahusisha ndugu wa pande zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…