Habari ndugu zangu,
Mie nimetumikia industry ya Media upande wa Printing, Design, Social Media Management na Video Production kwa miaka 3 sasa. Nimeamua kujiajiri kwa kuwa na kampuni ya Web Design & Development, kazi ambayo inahitaji Laptop yangu tu na ninaweza kuifanyia nyumbani.
Changamoto niliyonayo ni anuani, yaani wakati mwingine wateja watahitaji wanitembelee nilipo, kwahiyo ni lazma niwe na kituo. Lakini mtaji wangu haukutosheleza kujifungulia ofisi au kuchukua fremu mahali.
Sasa nahitaji kijiwe cha washkaji (Web & Graphic Designers) waliojishika pamoja kwenye fremu eneo flani ili hicho kiwe kituo changu pia au kuajiriwa (kwa makubaliano maalumu k.v. kukufanyia kazi zako zinazomatch skillset yangu kwa bure au nusu mshahara kutegemeana na wingi wake) na wewe utaniruhusu kuwa nakuja ofisini kwako kama mfayakazi wa kawaida lakini nina Uhuru wa kutoka muda wowote kwenda kumuona mteja aliyeniita.
Tayari nina Domain yangu na Website italaunch hivi karibuni. Please PM me if you are touched to support my entrepreneurship efforts.