Yakki Kadaf
Member
- Jan 8, 2023
- 29
- 94
Habarini wakuu, Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nipo maeneo ya bunda,mkoani Mara. Ijumaa iliyopita tarehe nilipata mwaliko kuhudhuria kikao cha wazazi na walimu katika shule ya Sekondari Nyiendo kujadili mustakabali wa shule kwenye maeneo tofauti na hasa eneo kuu la taaluma. Nilibahatika kuongea na baadhi ya wanafunzi, walimu na wazazi na nikabaini yafuatayo:
1.Mwaka 2017 mkuu wa shule aliidhinisha kuhamishiwa shule za msingi walimu wapatao 10 wa masomo ya sanaa kwa kigezo cha shule yake kuwa na walimu wa ziada. Leo hii anahangaika kutafuta mwalimu wa muda kwa somo la Geography!
2.Pesa inayolipwa kwa ajili ya waalimu wa muda(Part time teachers) hupokelewa mkononi cash badala ya kulipwa moja kwa moja bank kitu ambacho kinaibua maswali miongoni mwa wazazi na kupelekea baadhi yao walisusie kiaina zoezi la uchangiaji.
3.Kuna mwalimu mmoja wa kiume anayefundisha somo la kiswahili kuonekana kwake shuleni na hasa darasani ni kama kakakuona.Ndani ya mwezi mmoja anaweza kuhudhuria shuleni kwa siku 4au 5!Na inadaiwa mara nyingi kuonekana kwake hutokana kuona kipindi hicho kuna issue za fursa mfano michango ya T-shirt, nembo au kama kuna function yoyote iliyo na manufaa kwake. Walimu wenzake kutoka idara husika wamekuwa wakilalamika sana kuhusu mwenzao kuwategea ufundishaji huku wakigusia kwamba ni mwalimu anayeogopwa mno na mkuu wa shule. Wanadai siyo kuogopwa tu ila hawajawahi kusikia au kuona akionywa kama wengine.
4.Ofisi ya makamu mkuu wa shule ina wahusika wawili ila hawajui hata majukumu yao zaidi ya kusimama parade jumatatu na alhamisi kumkaribisha mkuu wa shule.
5.Shule ilipewa matanki ya kuvuna maji ya mvua ikiwa kama mnufaika wa project za Grumeti, lakini kuna koki imeharibika na hivyo kupitisha maji chini 24hrs na huku gharama za koki husika ikiwa ni 5000/=mpaka 7000/=. Mkuu wa shule na walimu wake wapo tu.
6.Bodi ya shule haina watu wabunifu wa kukaa na kutatua changamoto za kiufundi zaidi ya kukutana kwa ajili ya kufukuza watoto wenye nidhamu mbovu na kisha kuchukua posho tu. Inadaiwa bodi ya awali ya Dr. Masige ilikuwa active ila kutokana na kutokukubaliana na baadhi ya mambo ya mkuu wa shule ilitengenezewa zengwe na hatimaye mazingira yaliandaliwa kutafutwa watu wa karibu na mkuu wa shule.
6.Kuna mwalimu anaitwa Edward Mayela, huyu ndio engine ya shule. Yeye ni mtaaluma wa shule. Inasemekana siku akiondoka na shule inakufa kifo cha mende. Huyu bwana ni kama mkuu wa shule au mwalimu wa nidhamu kwa jinsi anavyopambania shule.
7.Kichekesho kingine ni kwamba wakati wa zamu, zamu hushikwa na walimu wawili wawili ila wale wasiojua kiingereza hubaki na majukumu ya kuandika taarifa kwenye daftari la zamu na wale wenye uelewa ndio husimama parade na kuzungumza na wanafunzi.
8.Walimu wengi toka kata ya kabarimu wanamuomba Afisaelimu halmashauri ya mji kuwabadilishia Afisaelimu kata aliyepo (Tabu) maana hana approach nzuri zaidi ya kutumia muda mwingi kutisha walimu, kutokubali mawazo yao na muda mwingi kuwa na visasi. (Uchunguzi ufanyike kubaini haya). Afisaelimu kata anafikia hatua ya kukagua mpaka walimu wa mazoezi wakati wapo chini ya mkuu wa chuo. Kama siyo kuleta mkanganyiko hapo ni kutafuta migogoro isiyo na maana. Mwanachuo akaguliwe na mkufunzi hapo hapo akaguliwe na mratibu kweli?
9.Walimu wanalalamika wapatapo matatizo mfano kuuguliwa, kufiwa mkuu wa shule huwajibu kwa sms kwa neno moja 'noted' bila hata maneno ya kuwapa nguvu, faraja au kuwatembelea
10.Mkuu wa shule huwa hana kawaida ya kutembelea kwenye makazi ya walimu wa mazoezi shuleni(Block Teaching Practice) - BTP ili kubaini changamoto zinazowakabili. Hii huwafanya walimu wengi wafikao shule hii kujihisi ukiwa.
🙏Nawasilisha.
====
Kuhusu mrejesho wake, soma: Ujumbe kuhusu shule ya sekondari Nyiendo umewafikia walengwa

Last edited: