Nilivyopata mpenzi siku ya valentine nikiwa na ex wangu

KING ASSENGA

JF-Expert Member
Oct 8, 2016
926
1,469
Habari ndugu yangu. Bila shaka upo salama kabisa na Afya tele . Pole kwa misukosuko ya hapa na pale katika kulisaka tonge 🙏

Waungwana maisha ni safari ndefu ila sio kwa Kila mtu inakuwaga ndefu sana. Kuna wale wenye bahati waliosoma kwanzia madarasa ya awali mpaka chuo bila kurudishwa ada na baada ya kumaliza wakapata kazi hapo hapo akaingia kwenye mahusiano na Moja kwa Moja mpaka kwenye ndoa na sasa wanafamilia nzuri iliyonyooka tu.

Halafu Kuna sisi ambao tulirudishwa sana ada tumesoma kwa taabu sio kidogo tumemaliza ajira imekuwa kizungumkuti dana dana, mambo sio mambo, Kwenye mahusiano nako tumeacha na tumeachika mpaka hatuelewi tena yupi mbaya yupi mwema 😅 hakika sisi ndio tuna haki ya kusema maisha ni safari ndefu.

Nisiwachoshe tusichoshane . Valentine day ya mwaka huu kwangu nilishusha Tanga nikapandisha Tanga safari ikaendelea 😅

Unafikiri ilikuwaje?
Kama wengine Mimi na mpenzi wangu wawakati huo tulipanga kutoka pamoja tukaenda reserve Moja nzuri sana ipo jirani na dar es salaam.

Ilikuwa ni surprise kubwa sana kwake
Hakutegemea siku hiyo ningeweza kuacha biashara zangu na kuwa na yeye. Tulitembea tukielekezwa vivutio mbalimbali vilivyopo na mwanamke mmoja mrembo sana alikuwa mcheshi aliyefanya safari yetu isichoshe kabisa ndani ya reserve ya kuvutia sana.

Basi kama kawaida punda hasahau kurusha mateke hata umlishe vipi. Mpenzi wangu wa wakati huo akaanza kunilaumu sikumjulisha kuhusu dressing code kulingana na nature ya eneo tulipaswa kuvaa raba ila sikulifahamu Hilo na sikutegemea kosa dogo hivyo lingeharibu surprise nzima niliyomwandalia. Nikajikita kwenye kumtuliza asinielewe yule mrembo naye akanitetea kuwa sikujua maana ni mara yangu ya kwanza pia kufika.

Hapo ndio alipaniki kabisa akafoka unamtetea unamjua hakuna jambo anafanyaga huyu liende lote vizuri. Basi tukanyamaza tukawa tunatembea tukiwa kimya kabisa . Mrembo mwelekezaji akaendelea kutoa maelezo Mimi nikimpa ushirikiano bila kujali mpenzi wangu yupo kwenye Hali gani. Basi tulifika sehemu nzuri ya kupumzika na kupata mahitaji muhimu.

Kwa haraka nikaenda kujichukulia wine naye akaenda kuchukua soda na maji tukakaa tukiongeleshana kawaida tu. Mrembo mwelekezaji akaja na kutoa maelezo ya sehemu ambayo tutakwenda baada ya kujipatia chakula maji na Vinywaji . Mpenzi wangu wa zamani akakataa . Mimi nikaweka msimamo wa kwenda basi akasema niende atanisubiri.

Basi Moja kwa Moja tukaondoka na mrembo mwelekezaji. Nikaanza kulaumu kuhusu tabia za mpenzi wangu. Akawa ananisikiliza tu mwisho akasema kazi unayo. Mtu unatolewa out mtu anakupa muda wake kosa dogo tu lawama nyingi hivyo.

Kuna wengine hata kutolewa out kwenda kununuliwa soda ya 600 haijawahi kutokea na sio kwamba sio warembo ni warembo sana tu ila ndio bahati mbaya waliyonayo kwenye mahusiano. Tulipiga sana stori zaidi ya lisaa na nusu tukitembea wenyewe.

Nilivutiwa sana na upole na ustaarabu wake mpaka nikajikuta naomba kuwa na mahusiano naye. Akakaza aisee akidai ni siku ya kwanza tu tumeonana hawezi kunipa jibu. Basi nikakaza kuomba namba akakubali nikachukua nikasave.

Ila kwakuwa safari iliendelea nikazidi kumwomba tuifanye hiyo siku kuwa spesho kwetu yule mpenzi lawama nitaangalia namna ya kumtoa akakataa. Basi nikakausha tukawa tushamaliza safari kumfikia mpenzi lawama basi akalianzisha tena tumechelewa kuwa nafanya Nini na huyo mwanamke 😅. Huwezi kuamini ninachokueleza ila huyu mwanamke alijaa visirani visivyofanana nae kabisa

Basi tulikaa tukala pamoja Mimi akili yangu ikiwa kwa mrembo mwongozaji.

Nilitamani kumaliza nae siku nzuri ya valentine. Nilitamani kuanzisha mahusiano mapya badala ya kuendelea kulaumiwa kwa Kila kitu.

Basi muda kama wa saa tisa alasiri basi nikaharakisha tutoke kwenye reserve nikisingizia kuumwa kichwa basi tukatoka na baada ya safari fupi nikataka kwenda nyumbani na mpenzi wangu aende kwake nahitaji kupumzika. Akagoma akataka tuende wote kwangu .

Nilimwomba kuwa nahitaji sana utulivu kichwa kitulie na kusingizia kwangu nimetembelewa na mdogo wangu. Hapo lawama zikaamka kuwa Kuna mtu nitakuwa nae ndio maana sitaki nilijitetea mwisho akakubali .

Tulivyoachana tu. Nikamwibukia mrembo mwelekezaji hewani kama ametoka kwenye reserve au la akawabado. Nikamwomba tuonane sehemu fulani ndani ya reserve basi hakuwa na hiana akakubali siku ikaanza kuniendea vizuri. Nilimkuta ashatoa uniform ya kazi kavaa kapendeza kama malkia.

Tukaendeleza mambo mengi tukapiga picha pamoja tukaendesha boti na baadae tukatoka pamoja kwenda kwenye hotel nzuri kumalizia siku ya valentine pamoja.

Upinzani mkubwa niliupata kwenye kuchukua chumba tu. Niliomba sana nikisema niliomba kwa juhudi gani mpaka kufanikiwa nitapewa adhabu kwenye kikao Cha wanaume maana hairuhusiwi kuomba kiasi hicho.
Basi nihitimishe tu sijutii uamuzi wangu wa kushusha Tanga na kupandisha Tanga siku ya valentine.

Nimepata mrembo anayefaa kuwa mke kabisa. Kama ni wimbo. Dj nipigie wimbo wa mboso Nadekezwa Tafadhali 🙏
 
Tulivyoachana tu . Nikamwibukia mrembo mwelekezaji hewani kama ametoka kwenye reserve au la akawabado. Nikamwomba tuonane sehemu fulani ndani ya reserve basi hakuwa na hiana akakubali siku ikaanza kuniendea vizuri . Nilimkuta ashatoa uniform ya kazi kavaa kapendeza kama malkia. Tukaendeleza mambo mengi tukapiga picha pamoja tukaendesha boti na baadae tukatoka pamoja kwenda kwenye hotel nzuri kumalizia siku ya valentine pamoja.
Upinzani mkubwa niliupata kwenye kuchukua chumba tu . Niliomba sana nikisema niliomba kwa juhudi gani mpaka kufanikiwa nitapewa adhabu kwenye kikao Cha wanaume maana hairuhusiwi kuomba kiasi hicho.
Basi nihitimishe tu sijutii uamuzi wangu wa kushusha Tanga na kupandisha Tanga siku ya valentine . Nimepata mrembo anayefaa kuwa mke kabisa.
Kama ni wimbo . Dj nipigie wimbo wa mboso Nadekezwa Tafadhali 🙏

Yani upo palepale kiumeni, hamna kulizwalizwa tulishasema analeta kujua unasonga mbele tu kiongozi! Hamna kujuta
 
Hongera mkuu kwa kuitengeneza AKILI yako isizidi HISIA ZAKO. Japo kwenye kuombea huwezi kupata adhabu ilimradi uliichakata basi wewe ni mwamba ila ulikumbuka kutumia ndom?
 
Nilitumia ila nimstaarabu sio Malaya kwa uzuri alionao angekuwa Malaya angekuwa na maisha mazuri sana
 
Habari ndugu yangu. Bila shaka upo salama kabisa na Afya tele . Pole kwa misukosuko ya hapa na pale katika kulisaka tonge 🙏

Waungwana maisha ni safari ndefu ila sio kwa Kila mtu inakuwaga ndefu sana. Kuna wale wenye bahati waliosoma kwanzia madarasa ya awali mpaka chuo bila kurudishwa ada na baada ya kumaliza wakapata kazi hapo hapo akaingia kwenye mahusiano na Moja kwa Moja mpaka kwenye ndoa na sasa wanafamilia nzuri iliyonyooka tu.

Halafu Kuna sisi ambao tulirudishwa sana ada tumesoma kwa taabu sio kidogo tumemaliza ajira imekuwa kizungumkuti dana dana, mambo sio mambo, Kwenye mahusiano nako tumeacha na tumeachika mpaka hatuelewi tena yupi mbaya yupi mwema 😅 hakika sisi ndio tuna haki ya kusema maisha ni safari ndefu.

Nisiwachoshe tusichoshane . Valentine day ya mwaka huu kwangu nilishusha Tanga nikapandisha Tanga safari ikaendelea 😅

Unafikiri ilikuwaje?
Kama wengine Mimi na mpenzi wangu wawakati huo tulipanga kutoka pamoja tukaenda reserve Moja nzuri sana ipo jirani na dar es salaam.

Ilikuwa ni surprise kubwa sana kwake
Hakutegemea siku hiyo ningeweza kuacha biashara zangu na kuwa na yeye. Tulitembea tukielekezwa vivutio mbalimbali vilivyopo na mwanamke mmoja mrembo sana alikuwa mcheshi aliyefanya safari yetu isichoshe kabisa ndani ya reserve ya kuvutia sana.

Basi kama kawaida punda hasahau kurusha mateke hata umlishe vipi. Mpenzi wangu wa wakati huo akaanza kunilaumu sikumjulisha kuhusu dressing code kulingana na nature ya eneo tulipaswa kuvaa raba ila sikulifahamu Hilo na sikutegemea kosa dogo hivyo lingeharibu surprise nzima niliyomwandalia. Nikajikita kwenye kumtuliza asinielewe yule mrembo naye akanitetea kuwa sikujua maana ni mara yangu ya kwanza pia kufika.

Hapo ndio alipaniki kabisa akafoka unamtetea unamjua hakuna jambo anafanyaga huyu liende lote vizuri. Basi tukanyamaza tukawa tunatembea tukiwa kimya kabisa . Mrembo mwelekezaji akaendelea kutoa maelezo Mimi nikimpa ushirikiano bila kujali mpenzi wangu yupo kwenye Hali gani. Basi tulifika sehemu nzuri ya kupumzika na kupata mahitaji muhimu.

Kwa haraka nikaenda kujichukulia wine naye akaenda kuchukua soda na maji tukakaa tukiongeleshana kawaida tu. Mrembo mwelekezaji akaja na kutoa maelezo ya sehemu ambayo tutakwenda baada ya kujipatia chakula maji na Vinywaji . Mpenzi wangu wa zamani akakataa . Mimi nikaweka msimamo wa kwenda basi akasema niende atanisubiri.

Basi Moja kwa Moja tukaondoka na mrembo mwelekezaji. Nikaanza kulaumu kuhusu tabia za mpenzi wangu. Akawa ananisikiliza tu mwisho akasema kazi unayo. Mtu unatolewa out mtu anakupa muda wake kosa dogo tu lawama nyingi hivyo.

Kuna wengine hata kutolewa out kwenda kununuliwa soda ya 600 haijawahi kutokea na sio kwamba sio warembo ni warembo sana tu ila ndio bahati mbaya waliyonayo kwenye mahusiano. Tulipiga sana stori zaidi ya lisaa na nusu tukitembea wenyewe.

Nilivutiwa sana na upole na ustaarabu wake mpaka nikajikuta naomba kuwa na mahusiano naye. Akakaza aisee akidai ni siku ya kwanza tu tumeonana hawezi kunipa jibu. Basi nikakaza kuomba namba akakubali nikachukua nikasave.

Ila kwakuwa safari iliendelea nikazidi kumwomba tuifanye hiyo siku kuwa spesho kwetu yule mpenzi lawama nitaangalia namna ya kumtoa akakataa. Basi nikakausha tukawa tushamaliza safari kumfikia mpenzi lawama basi akalianzisha tena tumechelewa kuwa nafanya Nini na huyo mwanamke 😅. Huwezi kuamini ninachokueleza ila huyu mwanamke alijaa visirani visivyofanana nae kabisa

Basi tulikaa tukala pamoja Mimi akili yangu ikiwa kwa mrembo mwongozaji.

Nilitamani kumaliza nae siku nzuri ya valentine. Nilitamani kuanzisha mahusiano mapya badala ya kuendelea kulaumiwa kwa Kila kitu.

Basi muda kama wa saa tisa alasiri basi nikaharakisha tutoke kwenye reserve nikisingizia kuumwa kichwa basi tukatoka na baada ya safari fupi nikataka kwenda nyumbani na mpenzi wangu aende kwake nahitaji kupumzika. Akagoma akataka tuende wote kwangu .

Nilimwomba kuwa nahitaji sana utulivu kichwa kitulie na kusingizia kwangu nimetembelewa na mdogo wangu. Hapo lawama zikaamka kuwa Kuna mtu nitakuwa nae ndio maana sitaki nilijitetea mwisho akakubali .

Tulivyoachana tu. Nikamwibukia mrembo mwelekezaji hewani kama ametoka kwenye reserve au la akawabado. Nikamwomba tuonane sehemu fulani ndani ya reserve basi hakuwa na hiana akakubali siku ikaanza kuniendea vizuri. Nilimkuta ashatoa uniform ya kazi kavaa kapendeza kama malkia.

Tukaendeleza mambo mengi tukapiga picha pamoja tukaendesha boti na baadae tukatoka pamoja kwenda kwenye hotel nzuri kumalizia siku ya valentine pamoja.

Upinzani mkubwa niliupata kwenye kuchukua chumba tu. Niliomba sana nikisema niliomba kwa juhudi gani mpaka kufanikiwa nitapewa adhabu kwenye kikao Cha wanaume maana hairuhusiwi kuomba kiasi hicho.
Basi nihitimishe tu sijutii uamuzi wangu wa kushusha Tanga na kupandisha Tanga siku ya valentine.

Nimepata mrembo anayefaa kuwa mke kabisa. Kama ni wimbo. Dj nipigie wimbo wa mboso Nadekezwa Tafadhali 🙏
ulichofanya ni ukware
 
Asa mkuu umeokota mhudumu huko unampamba sijui mke na bla bla,,, jifikirie amehudumia watu wangapi ? Wangapi wamemtaman ? Mtu umeenda kazn kwake na dem wako, kawahudumia umemtaman nae akajaa, the same day/night umeenda kulamba unajisifia ? Hilo ni shenkupe umeokota, ngoja upigwe matukio utamkumbuka huyo unaemuona ana kisirani
 
Hapo huyo dada muongozaji alikuwa mzuri kuliko mpenzi wako. So ni wivu tu ulimsumbua, sisi wadada tukipenda visirani na kununa hakuishi tunahisi tunaibiwa kila wakati na siku tukiacha visirani ujue na upendo umeisha so huyo dada anakupenda. Ila huyo muongozaji hakupendi ni tamaa tu za treatment zako.
 
Back
Top Bottom