HSE Officer
JF-Expert Member
- Apr 10, 2023
- 665
- 887
Habar ndugu zangu wa Jf
Awali ya yote napenda kutoa shukran zangu za dhati kwa muanzilishi wa Jf kwani naburudika na naelimika kwa mada zinazotolewa humu.
Nisipoteze muda niende kwenye mada iliyonileta kwani kama kichwa cha habar kinavyosomeka " Nilivyonusurika kutapeliwa mtandaoni"
Ilikuwa muda wa saa nne asubuhi nipo katika kutafuta maokoto kama vijana wa sasa wanavyosema, ndio nilivyoiona namba ya simu yenye utambulisho wa US yaani imeanza na (+1) (000-000-000-) ( code) , hiyo namba ikinisabahi kupitia WhatsApp na kuanza kujitambulisha
Baada ya kutambulisha akanieleza wao ni online shopping wanahusika na kuuza bidhaa online ila mbali na kuuza bidhaa online pia wana tenda ya kutangaza vivutio vya utalii duniani
Kwa upande wangu nikamuambia sawa nimekuelewa , baada ya kumuambia hivyo akaniambia nakutumia link ya kuangalia video za YouTube baada ya kuangalia hizo video Ni- subscribe na ni like halafu ni screenshoot nimtumie baada ya kumtumia atanitumia elfu sita 6000
Baada ya dakika chache akanitumia link ya YouTube na mimi nikafanya kama alivyoniambia baada ya kumtumia screenshot akanitumia link ya mdada yeye alisema kama receptionist wa kampuni yao na yeye ndie anayehusika na malipo
Baada ya kunipa namba ya receptionist haikuwa shida kwenda telegram kwani Application ya telegram nilikuwa nayo, baada ya kwenda telegram kwenye inbox ya receptionist nikamsalimia na yeye aka anza kujitambulisha
Receptionist akaniambia kuwa inabida niseme jinsia yangu , umri wangu namba ya simu na jina litakalotoka atakaponiingizia 6000 pia vile vile aliniambia pesa ikiingia nimtumie screenshot, nami sikusita fasta nikamuandikia baada ya dakika kama nne muamala ukasoma umepokea shilingi elfu sita .
Baada ya kupokea ile pesa nikamtumia screenshot shoot , baada ya hapo receptionist akaanza kuelekeza jinsi ya kufanya ili nipate pesa nyingi
Receptionist akaanza kuniambia kazi yao wanaanzia saa 2.30 asubuhi mpaka saa 1.30 usiku nikasema sawa hamna shida , pia akaendelea kuniambia kuwa kazi zao huwa wanaita task yaani kwa siku task zao zina range kuanzia 23 hadi 27
Lakini katika hizo task , 20 task ni za kuangalia video YouTube then una like na subscribe then una screenshot halafu unawatumia wao kila video moja shillings elfu moja , nikasema chaka ndio hili kwa siku video 20 yaani elfu 20 kwa mwezi laki sita
Tuendelee nikaanza kuangalia video kama mbili hivi mara ikaja task ya tatu kasheshe ikaanzia hapa , hii task ilikuwa inaitwa investment task
Hii investment task ukiweka hela unapata asilimia 30% ya ile hela yako kwa kima cha chini ilikuwa elfu 50 na hii kwa new comers ( njuka) yaani ukiweka 50k unapata elfu 65
Kiasi kinachofata ilikuwa 100,000 hii unapata 130,000
Kiasi kinachofata 300,000 hii unapata 390,000
Kiasi kinachofata 500,000 hii unapata 650,000
Kiasi kinachofata ilikuwa 1,000,000 hii unapata 1,400,000
Basi bwana kwa kuwa mi ni mgeni nikasema ngoja niruke na hii ya 50 k ili nipate 65k , baada ya kufanya muamala nikamtumia screenshot yule receptionist niliyekabidhiwa na ile kampuni ya kitapeli.
Baada ya kumtumia screenshot ya malipo receptionist akasema inabid aniunganishe na Teacher au tutor yeye ndiye atakayenisimamia katika suala zima la malipo , punde si punde receptionist akanitumia link ya telegram ya teacher ili anisimamie kwenye investment
Ndugu msomaji wakati mambo haya yote yanafanyika nilikuwa nawaza hela ya 50k huku nikijipa moja risk taker ndio wanaofanikiwa basi muda ule ule akili ikanijia nizuie muamala na kwa upande wangu haikuwa kazi ngumu baada ya dk kazi mtandao husika wakasema muamala umezuliwa.
Basi wakati naingia kwenye inbox ya teacher wa investment kitu cha kwanza akasema nimtumie screenshot za malipo haikuchukua muda nikamtumia screenshot ya malipo na yeye ndio akaanza kunielekeza kufanya investment, jambo la kwanza kabisa akaniambia nijisajili kwenye hiyo online shopping
Hii online shopping nakumbuka inaitwa "falabella descuentos " basi nikajisajili then nikamtumia screenshot ya usajili yule teacher wangu akaniambia nisubir dakika chache anaandaa risit ili nipewe hela yangu elfu 65 , kweli bhana baada ya dakika chache muamala ukasoma umepokea shilingi elfu 65 , basi nikascreenshot muamala niliopokea nikawatumia.
Baada ya kupokea ile elfu 65 nilikuwa na wenge sana nakasema maisha ndio haya bhana wakati huo huo huku naendelea kuangalia video YouTube na namtumia screenshot receptionist na kwa siku hile iliishia video 9 maana yake nina elfu tisa ila haikuwezekana kunipatia kwan kutuma wanaanzia elfu kumi
Siku ya pili iliamkia jumamosi yaani tarehe 18.11.2023 ilivyofika asubuhi saa 2.30 nikaingia kazin kama ilivyoratiba yetu , kazi ya kwanza ikaja ya kuangalia video YouTube hivyo ikafanya video zangu ziwe kumi na baada ya dakika kama tano hivi muamala ukasoma umepokea shilingi elfu 10 , nikasema maisha ndio haya
Task ya pili ikaja ya investment mi nikawaambia nataka kuinvest 50k wakakataa wakasema hii ni kwa ajili ya new comers tu basi nikasema na invest 100,000 laki moja wakakubali
Basi baada ya kulipa ile laki moja kwa lengo la kupata 130,000 yaani faida elfu 30 , basi nikamtumia screenshot teacher wangu akasema anaandaa paycheck ili nipate faida yangu ila kabla ya hapo teacher akaniambia kwamba kanuni ya ile trading haina refund yaani kama umekosea imekula kwako
Kabla ya kunitumia ile 130,000 teacher akaniambia inabid uongeze elfu ishirin ili niweze kupata elfu 26 na ile 130k itakuwa 156k jumla yote kwa kuwa pale kwenye simu nilikuwa nayo ile hela basi nikalipa elfu ishirin kama kwaida nika screenshot nikamtumia screenshot
Baada ya kulipa elfu ishirin wakaandaa malipo wakanitumia 156,000 faida elfu 36 nikasema haya ndio maisha huku naendelea kuangalia video YouTube kila video moja elfu moja nimejifungia geto na kila baada ya dakika 20 task inakuwa tayar na kwa hii siku nakumbuka niliangalia video ishirin lakin pesa hawakunitumia waliniambia malipo kesho
Nakumbuka jpili tarehe 19.11.2023 baada ya task kama tatu hivi kupita za kuangalia video YouTube ndipo task ya nne ikaja ya investment nikawaambia mi nataka ku invest 100,000 ila wakakataa na kusema kuwa hiyo laki moja imeshawahiwa inabid uchague nyingine na kwa kuwa nilishaanza kunogewa na ule mchezo nikasema ngoja nijitoe muanga kwenya laki tatu
Nikawaambia poa na invest laki tatu basi nikatuma fasta laki tatu , screenshot nikamtumia teacher kama kawaida baada ya kumtumia teacher akasema subir kama dakika moja niangalie kama kuna uwezekano wa option nyingine kumbuka nilivyoweka 100,000 ikaja option ya pili niongeze elfu 20 , sasa kwa upande wa huu laki tatu wakasema niongeze laki nane ili niweze kupata hela yangu
Kutokana na wenge na kwenye simu ilibaki elfu mbili nilishindwa kujua kabisa kuelewa kile kias anachotaka niongeze badala yake nikaona elfu themanin (80k) pale pale mawazo yakanijia ya kuzuia ule muamala wa laki tatu then nikampigia mwanangu anikopeshe laki moja ili nikalipie elfu 80 ili nipate hela yangu
Baada ya kutuma ile elfu themanin 80k nikascreenshoot nikamtumia teacher baada ya kuona ule muamala aka hamaki na kuuliza hii umetuma laki nane au 80 , mi nikamjibu elfu 80 basi akaniambia unahitajika utoe laki 7 n 20 ili ugomboe hela yako, baada ya kuniambia vile nilichanganyikiwa sana nilikula sijanywa chai ila nilikuwa sihisi njaa basi mawaza yakanijia ya kuzuia muamala ule wa elfu 80k
Basi nikajaribu kumuomba teacher ani refund laki 3 na 80 yangu tu alikataa kata kata na kusema kuwa nilishakuambia ukikosea hamna refund basi nilichanganyikiwa sana
Kumbuka yule mshikaji wangu alinitumia laki nililipa elfu 80 ikabaki kama elfu 19 hivi nikaenda kutoa ili nipate chakula
Kutokea muda ule nikaachana na teacher nikarud kwa receptionist kwan yeye ndiye anayehusika na video za YouTube na malipo anafanya yeye kila moja buku nikasema ngoja nikomae kwenye buku buku mpaka jion elfu ishirin na ile ya jana itakuwa elfu 40 nikasema sio mbaya .
MUNGU NI MWEMA majira ya saa 9 jion naona muamala wa laki tatu unaingia kwenye akaunti yangu na kusema kwamba ule muamala uliokosea umerudishwa nikafurahi sana , nikamcheki yule jamaa alienikopa laki nikamtumia muda ule ule nikabakiwa na laki mbili , kidogo nikawa na amani
Nikakumbuka kuzuia muamala wa laki moja ilikataa nikajaribu wa elfu ishirini ukakubari kwa hiyo kwa upande wangu miamala niliozuia ulikuwa wa 50k ,80k na 20k
Jion ilivyofika upande wa video YouTube nilikuwa nishaangalia 20 na jana 20 kitu kama 40 sawa na elfu arobaini nikamrudia receptionist nikamuambia naomba commission yangu akasema huwezi kupata commission kwa sababu ulikuwa unaruka baadhi ya task.
Hapa baada ya kuwagundua hawa ni matapeli na wezi nikasema task za investment nitakuwa naziruka nafanya task za kuangalia video YouTube tu
Basi bhana baada ya kukataa kunilipa commission yangu nikaanza kumtukana matusi ya kiswahili nikakashangaa anajibu nikaanza kujua kumbe hawa matapeli wa kibongo
Basi leo jtatu kwa majira tofauti ukaanza kuingia muamala wa elfu 50k baada ya lisaa ukaingia wa elfu 20k na saa 9 jion leo jtatu umeingia muamala wa 80k nikasema wale wajinga hawajanipata .
My take :
Tupunguze tamaa hamna hela ya bure hapa duniani pia vile vile ukimtumia mtu hela kama humjua jaribu kuzuia muamala hela zangu zote laki nne na nusu zilirudi kwa kuwa nilizuia muamala.
Nimeattach mfano wa maelezo aliyonijibu baada ya kumuomba pesa yangu