Ukweli ni kwamba wanaume wengi sana wanalea watoto ambao sio wao, mabinti /wanawake wakibebeshwa mimba huko hutafuta wanaume wenye unafuu wa maisha na kuwabebesha mimba ambazo sio zao.
Niende kwenye mada,
Miaka ya nyuma nilikuwa na uhusiano na binti fulani ambae alinizidi umri kidogo(ingawaje alikuwa hajui) sasa ilitokea nikapelekwa kozi fulani kazini, nilivyopata barua nikamuita akaja kwangu ili tuagane, akakaa siku 2 akarudi kwao baada ya kuingia kwenye siku zake, mimi nikawa nimesafiri, baadae ya mwezi mmoja na nusu binti akawa anang'ang'ana aje nilipo, nikajitahidi kumkatalia na kumweleza mazingira yalivyo ikashindikana.
Yeye shida yake ikawa na kutaka kuja huko tena kwa gharama zake, kishingo upande nikamkubalia akaja, nilichokifanya siku amefika tu nikaenda dukani nikanunua kipimo cha mimba, kumpima kitu kikasoma vistari viwili, sikutaka maelezo nilimwambia abebe kilicho chake asepe, ukawa mwisho wangu na wake.
Mkasa wa pili ni wakati nipo chuoni mwaka wa pili, nilikuwa na binti mmoja kwenye uhusiano sasa tukapangiwa field mikoa tofauti, field ilikuwa inachukua wiki 6 baada ya hapo kila mtu anaenda likizo kwao, huyu binti alikuwa akiingia kwenye siku zake anaugua tumbo sana, akiwa na wiki moja field aliniambia anaumwa tumbo la hedhi na tulivyokaribia kumaliza field akawa analazimisha turudi chuoni tukutane halafu ndio kila mtu aende kwao, nilijaribu kumkatalia hasa nilimwambia kuhusu gharama maana kila mtu alikuwa mkoa wa karibu na kwao lakini akagoma. Nikaamua kumkubalia ingawaje alarm iligonga kichwani, kama yule wa mwanzo, nikanunua vipimo alivyofika tu nikampima kitu kikasoma positive, kumuuliza ni ya nani akaniambia ni ya mfanyakazi ofisi aliyokuwa anafanyia field, na huyo mfanyakazi alikuwa ameoa, biashara yangu na yeye ikawa imeisha hapo.
Wa mwisho ni binti mmoja niliyekutana nae nilivyorudi kusoma tena, yeye alikuwa undergraduate, katika uhusiano na huyu binti nilijitahidi kutumia kinga, maana alikuwa mzuri mno kiasi kwamba nilijua sipo peke yangu. Lakini ghafla tu akakataa matumizi ya mpira eti unamuumiza wakati hapo awali alikuwa hata yeye mwenyewe hataki peku, nikampima na yeye akawa ana kitu.
Kwa hakika bila ujanja wangu ningelikuwa nalea watoto wa watu, wanaume tuwe makini sana, mimba nyingi ni za kushikizwa.