KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 30,263
- 69,496
Asalaam alyeikum wana wa sensa..?
Hii dunia inamambo na watu wa kila namna, wengine sijui tujiweke kundi la namna gani..!
Weekend fulani hivi tulivu,mida ya saa sita usiku nilikuwa bar fulani (jina kapuni),natandika vinywaji hatari vile ambavyo vinafanana na maji lakini sio maji!,na ukimeza lazima ukunje uso! Huku nikishushia na Serengeti lager baridi tena ikitoa jasho fulani hivi la kejeli kuwa leo lazima lianguke jitu!.
Mi sio mtu wa vinywaji vikali ila sikuhiyo baada ya kuzinguliwa na "asiefunzwa na ***** hufunzwa na ulimwengu!".. Sasa mimi kuna mlimwengu mmoja alinifunza ndo nikaamua nikachambe koo kidogo ili nami nifanane na walimwengu na bila hiyana nilionana na hao walimwengu!.
Ile bar ilikuwa na ukumbi mpana kiasi na kwa muda huo wateja tulikuwa tumebaki wachache tu,kamziki fulani hivi kakizamani kalichangamsha kiaina.
Mnyweso ulianza kuniingia vilivyo mpaka nikaanza kuhisi joto!,hapo ubongo unatembelea tairi la mbele tu!
Katika kutupia macho nikaona jimama linacheza mziki japo kiuchovu,akili ya pombe ikanivaa ikaniambia "ushapata wa kufanana nawewe".
Hata sikukawia haraka nikachupa kwenye kile kiti cha kaunta nikaanza kusogea kwa yule jimama huku nami nalisakata!,punde nikamkaribia nyuma yake!.. kucheki uno lote lipo mbele yangu nikalibambia!.
Mshangazi wa watu hakuwa na hiana ndo kwanza akanikabidhi uno lake nami nikakamatia nakuanza kulisakata!.
Baada ya Kama dakika tano hivi nikarudi kwenye kinywaji changu nakugida tena!,Sasa mara hii ndo joto likanikolea kinomanoma nikaona hata hili t-shirt nililovaa lanifaa nini..?
Nikaamua kulivua nakulitundika begani,nikamfata tena yule mshangazi nakuanza kulisakata tena upya!.. wakati huo nae yupo chakali!.
Wakati haya yakwetu yanaendelea kumbe na jambo jengine ambalo mimi sina taarifa nalo lilikuwa likiendelea!,wakati sisi tunasakata rumba kumbe moja ya wafanyakazi wa hii bar alikuwa anafanyiwa happy birthday na saa sita hii ya usiku wafanyakazi wenzake ndo walianza maandalizi ya kuandaa kameza kadogo wakaweka keki na tumapambo mapambo!, zaidi nilichoambulia kuona ni harakati za hawa wahudumu tu ila binafsi sikujua kama kuna birthday ya mtu humo!.
Mimi na mshangazi wangu ngoma ilikuwa imepamba moto kiasi kwamba inataka kuchanika!..
Msakato ulisakatwa haswa,kifua wazi,uno lote nilipewa wimbo nao ulikonga nyoyo zetu na wawili sie tulijua kucheza na kana kwamba mafundi dansi kumbe walevi wawili tu!.
Nikiwa nyuma yake nae kainama anakata mauno yakufa mtu,hapo nishajisahau mikono yangu nimenyanyua juu,ndipo mwenzangu alipoamua kuachia pigo la mwisho la wimbo kwani wimbo nao ndo ulikuwa ukifika tamati!.
Ghafla tu nikapigwa na makalio yake kiunoni "pwaaa" Kama pigo la wimbo lilivyoishia!..
Kutokana na nilivyokuwa hoi kwa ulevi balance zilikuwa zinasoma nusu nusu,pigo la uno lake lilinisukuma kwenda nyuma hata nilipojitahidi kutia breki za kilevi zilifeli!.
Tambo ya kwanza kurudi nyuma nikaenda nayo,yapili nayo nikaenda nayo pia na ya tatu ile nafika ya nne breki na balance zote zikawa zimechoka zikaamua kama mbwai iwe mbwai!!.
Nikiwa kifua wazi kimgongo mgongo nikaenda kuangukia keki ya watu!!
"Pwaaaaaa"
Mishangao ya kila namna ikafuata mwenye kuguna akaguna!,mwenye kucheka akacheka ila kuna mishangao miwili ndio ilikita zaidi kwenye kichwa changu!.
Mmoja nilisikia akisema
"TOBA WEEEE"
huyo alikuwa wakike!.
Sauti nyengine yakiume ikamalizia
"KWISHA HABARI!!".
Sauti nyengine yakilevi ndio ikafunga kazi ikisema..
"ALIPE HUYO!!"..
Waswahili walisema siku ya kufa nyani miti yote huteleza wakati najitapanya ili niinuke ikatokea njemba ikanikanyaga tumboni nirudi nilipoangukia ile keki!.. sikuwa na pingamizi nikarudi kimgongo mgongo huku keki ikiwa imeshanitapakaa utafikiri mimi ndie nilikuwa mwenye hiyo happy birthday!.
Walimwengu tayari wakawa washafika eneo husika wakinishangaa unajisi nilioufanya ile njemba nayo haikutoa mguu wake nikajua kabisa hapa leo nishayakanyaga!.. wenye simu zao wakaanza na mikamera mwenye kuchukua video twende mwenye kuchukua picha nae twende!.
Sasa binti mwenye birthday yake nae alikuwa hapohapo na hakuwa peke yake alikuwa na boyfriend wake!...
Mkitaka kujua nilikuwa kwenye hatari kiasi gani au mimi nilikuwa naonekana ni jambazi kiasi gani kwenye hii birthday ya watu ni hii picha niliyokuwa siijui kwa wakati huo ila picha kamili ilikuwa hivi...
Hii couple huyu binti alikuwa akifanya kazi kwenye hii bar ila boyfriend wake wasasa hafanyi kazi hapa,isipokuwa huyu binti alikuwa na ex wake ambae alikuwa anafanya kazi hapa.. likatokea lakutokea wakaachana na huyu binti.
japo jamaa alikuwa bado anamtaka huyu binti!.. kiufupi ex wa huyu binti alikuwa hajapenda kuachana na huyu binti na mbovu mbaya kabla ya hii birthday alimtolea maneno mabovu huyu binti ya kuwa atahakikisha anaharibu birthday yake!...
Ukisikia kwenye msafara wa mamba na kenge tumo hii ndio maana yake sasa, maeneo kama haya ndio huwa naona ule usemi wa ya ngoswe muachie ngwose huu usemi haufai!.
Mbele ya hii couple nilikuwa naonekana kama jambazi nilietumwa na jambazi mkuu!,hivyo nastahili kupewa kichapo kikali ili nikifika kwa alienituma asinitume tena!.
Kwa shauli ya pombe nikaona hapa nikiwa mpole nitatoka uchi ya mnyama niuze nyago ndani na nje ya nchi maana walimwengu wa leo nitofauti na wale wa kule kwenye swimming pool,Hawa waleo wanakamera na wameshaanza kunimulika!.
Si nikajitia ugaidi nikamsukuma yule jamaa alinikanyaga jamaa akaondosha mguu nikainuka Sasa ile kabla sijainuka vizuri boyfriend wa yule birthday girl sijui alikuja kwa spidi ipi ila nilishangaa napigwa mtama wa kimo cha mbuzi! Nilirudi tena chini pwaaa huku nikitapanya vitu pale chini hovyohovyo nakujikuta nikitamka
"YESU KRISTO!".
Visauti vya wadada kadhaa vikasikika vikisema Muache wengine hawana hata habari ndo kwanza wanachukua muvi na jambazi wao tayari nishaingia mkenge!..
Situation ilivyokuwa ni Kama kulikuwa na mabishano wengine wakisema niachwe, wengine wakisema nitiwe adabu ati nimetumwa na wengine walikuwa hawatii neno wao wapo tu lolote litakalosemwa wanaunga mkono na wengine hayo yalikuwa hayawahusu wao walikuwa wanaagiza bia tu!.
Katika hiyohiyo situation nikaona hapa pazito si nikaanza kutaka kutafuta upenyo nikimbie niinusuru roho yangu!,bahati nzuri nikaona upenyo kwanza nikajilegeza zaidi ili nionekane ule mtama tu umenishibisha kwenye sekta ya vipigo!.
Nikapimishia jicho pande zote upenyo wangu nikaona upo kwenye target Sasa ama zangu au ama za yeyote atakaekaa mbele zangu lazima nipitenae!!.
Lahaula ile najikoki naamka harakaharaka nataka kukimbia kumbe hesabu nilizopiga sizo bana! Upande niliochagua kutokomea ulikuwa ndio upande aliopo baunsa wa bar!.. mbio zangu za kutaka kuponyoka ghafla zitulizwa na banzi moja zito nafikiri lile banzi nilipe jina niliite "Mandonga classic!".
Mbinu zangu zakivita ziliisha zote isipokuwa ilikuwa imebaki moja tu ya kujifanya nimezimia!.
Na ndio nilichokifanya hapo nilitulia tuli sipwesi,sitikisiki na kupumua nikapunguza spidi!.
Taharuki ikazidi hata ambao walikuwa wamezira kunishuhudia ikabidi waje tu!,sijui Kuna watu wanapenda kuona watu wakiuliwa sijui wapoje tu!.
Hapo hata meneja wa ile bar ikabidi aingilie,yakaletwa maji kwenye ndoo nikaona sasa mambo ya swimming pool yanaletwa kwenye nchi kavu kutokana na kuwa na historia mbaya na maji mengi nikaona nijikoholeshe tu kabla hawajanimwagia!.
Mara hii hata kipigo kikapungua maana waliona huyu mlevi asije akatufanya tukaenda jela bure!
Kwa huruma ya meneja nikainuliwa nikapakiwa kwenye bodaboda na keki zangu mgongoni ili niende nyumbani!
Wala haikuwa mbali na nyumbani nilimuelekeza bodaboda akapajua hadi gheto.. Sasa ile tunakaribia kufika gheto taa ya pikipiki ikamulika pale mlangoni kucheki hivi kumbe yule kivuruge alienivuruga mpk nikapata huu msala alikuwa ameketi nje akinisubiri!.
Hapohapo nikamuambia bodaboda geuzi turudi tulipotoka!
Ile tunageuza nae akakeshatufikia akanidaba suruari kwa nyuma nikaona hapa nabaki nami nikamshika bodaboda wangu kichwa tubaki sote huu msala anisaidie kusolve....
Narudi.