Niliuziwa pasi feki ya phillips kwa shilingi elfu 45, epuka haya kuuziwa mbuzi kwenye gunia

round kick

Senior Member
Feb 3, 2025
196
679
Mwezi uliopita nilienda kutafuta pasi dukani, pasi yangu pendwa ni PHILLIPS, nilipoambiwa bei ni elfu 45 nikawa na imani kitu nachonunua ni original kumbe nimuziwa chambi, nashukuru alieniuzia ni mwelewa alinitafutia nyingine duka lingine

Nafika nyumbani nikalinganisha pasi yangu ya zamani na mpya,

kwanza pasi ya mwanzo original ilikuwa nzito, mpya ilikuwa nyepesi sana.

Pili ya kwanza ilikuwa na maandhishi ya phillips kwenye ubavu, mpya ilikuwa haina

1739862792091.png


Tatu: , kwenye box ;a pasi mpya imeandikwa made in Indonesia lakini baada ya uchunguzi nikaona pasi imeandikwa made in China

1739866918944.png
 
Pasi za PHILIPS ORIGINAL, nafikiri miongoni mwa pasi imara kuwahi kuuzwa hapa Tanzania.

Jamaa walitengeneza kitu durable na quality nzuri sana. Bidhaa nyingi sasa ni counterfeit.

Tanzania ni dampo la Low quality products, na sasa hadi Pombe ni FAKE.
 
Back
Top Bottom