Nilipata pesa na kujiona mwanaume ndani ya ndoa

Rosemin

Member
May 21, 2023
51
432
YAMENIKUTA; nilipata pesa na kutaka kuwa mwanaume ndani ya ndoa yangu!

Maisha haya acha tu, hivi kwanini kuna mambo yanatokea halafu ndiyo mtu unakuja kujutia baadaye. Nilinunuliwa Kitabu na rafiki yangu, yaani rafiki yangu yuleyule ambaye alikua akinishauri nimuache mume wangu ndiyo kaninunulia Kitabu baada ya mwanaume niiiyekua nikichepuka naye kuniachamiaka miwili iliyopita mimi nilipandishwa cheo hivyo kumzidi mume wangu kipato.

Nakumbuka rafiki yangu aliniambia, “Utachangiaje kikubwa kuliko mume wako, acha ujinga wanaume wanabadilika, nunua kiwanja chako jenga kivyako, hiyo ambayo mnajenga ina majina wote changia kile anachochangia.” Nilifanya hivyo, ingawa mume wangu aliumia lakini hakujali, aliendelea kuhudumia familia kama kawaida. Kwakua nina kipato kikubwa nikaacha kuaga tena natoa taarifa.

Yaani mume namtumia meseji tu nitachelewa halafu nikirudi nina chips zangu nakula sijali kama kumepikwa au la. Akinigusa nimechoka, sijui ni mdudu gani lakini baada ya kupanda cheo nilibadilisha marafiki, yaani wale wengine niliwaona kama ni wa mume wangu, nakumbuka kuna kipindi mume wangu aliniambia kuwa nimebadilika lakini sikujali, nilimuambia nipo bize na kazi.

“Mambo mengine huwezi elewa, ni mambo ya kikazi…” Nikimaanisha kuwa kwakua ana cheo kidogo basi hawezi kujua mambo ya wakubwa kazini. Aliumia sana lakini alijishusha, mume alianza kunyenyekea, alianza kuniona kama Mungu.

Nilijikuta tu namchukia, naanza kumuona kama kakinyago fllani. Bila kujijua nikaanzisha mahusiano naye, na Kaka mmoja ambaye alinisaidia kufungua duka la spea. Kila nikitaka kutoka naye basi nampa taarifa mume wangu kuwa naenda kununua mzigo wa dukani kumbe niko kwa mwanaume. Aliniambia kuwa yeye kaoa lakini mke wake wamegombana akamfukuza na mimi niliamini. Nilikua nachepuka, nikachanganyikiwa kwa mchepuko mpaka nikamtambulisha kwa wanangu.

Mume wangu alijua na kila alipolalamika nilimuambia kama kanichoka tuachane hivyo yeye ndiyo aliishia kuomba msamaha kwani aliona aibu kuniacha. Mambo kazini yalizidi kumuwia magumu kwani alichukua mkopo, alikua anadaiwa kila sehemu mpaka watu wengine wananitafuta namlipia madeni kwani mimi mbali na kazi Biashara zilikua ziko vizuri sana.

Nikimlipia madeni nampigia simu namsema mpaka anaishia kulia, sikujali. Kiburi kilipanda mpaka nikawa namtukana mbele ya watoto, lengo langu lilikua aniache tu lakini nilishangaa ananing’ang’ania nilimuambia kabisa sikutaki ila analia mpaka namuonea huruma. Sijui ni nini kiliniingia lakini nilibadilika sana.

Mambo yalibadilika mwezi wa tatu mwaka huu, ndipo mabalaa yalianza, kwanza nilisimamishwa kazi kwakua nilikua bize sana na maisha nikasahaua kazi, watu wa chini yangu walikua wakipiga pesa kijinga jinga nasaini mimi hivyo nikasimamishwa. Sijakaa sawa siku moja nipo kwa huyo mwanaume mchepuko wangu ambaye aliniambia kuwa kamfukzua mke wake kwakua hapendi ndugu zake mke wake kaja.

Aisee hakuna siku nilijiona takataka kama siku hiyo, Dada kaja kumbe alikua kikazi nnje ya nchi, mwanaume hata hajui kuwa karudi. Anatukuta mwanaume anajitetea kuwa mimi ni binti yake wa kazi, mwanamke aliniangalia kisha akacheka akamuambia

“Sitaki kujua, ondoa takataka yako hapa!” aliingia ndani na kuniacha sebuleni. Kumbe mwanaume naye kawekwa hapo tu ni kama analinda nyumba, hana kazi, hata udalali si Dalali magari yote ni ya mwanamke, nilitolewa ndani kama mwizi mwanaume ananiambia tusijuane.

Nikawa sina mtu wa kuongea naye, baada ya msala kazini marafiki zangu wote wale wapya hakuna aliyetaka kujihusisha chochote na mimi. Kusema kweli nilichanganyikiwa, natoka pale nikakamatwa nikawekwa ndani siki mbili, mtu aliyekuja kuniwekea dhamana ni mume wangu, hakuna cha rafiki wala ndugu, wale wote waliokula pesa zangu walinigeuka.

Aisee pesa zilinipa ulimbukeni, nikasahau kazi nikasahau na familia. Mume wangua lipambana kunitafutia wakili, alihangaika sana akafuatilia kwa watu wake mpaka nikaja kutoka kwa kuonekana kuwa sikula pesa bali nilikua mzembe tu basi, kama unavyojua binafsi, hawataki mambo ya kusumbuana, tukaambiwa tulipe, niliuza karibu kila kitu kurudisha pesa ya watu, Biashara nikauza yote nikarudisha sasahivi nipo nyumbani hata kazi sina.

Siku mume wangu anajua kuwa ameshakamilisha kila kitu, sina kesi tena wakati mimi najiandaa kumuomba msamaha ili turudiane nishajifunza ndiyo siku ananipa Talaka yangu namuuliza kwanini ananiacha wakati nishabadilika mbona kanihangaikia hivyo mpaka kuwa huru alichonijibu.
“Naoa mwanamke mwingine, sikutaka kuanza ndoa yangu mpya na watoto, nimekusaidia ili ubaki na watoto mimi naoa!”

Sikuamini mpaka alipofunga ndoa mwezi huu na hajali chochote kuhusu mimi. Nimemuomba sana niwe hata mke wapili lakini kagoma ananiambia akikaa na mimi kwa mambo niliyomfanyia ataniua. Natamani ningekusoma mapema ningeacha ulimbukeni wa pesa.

Ningejua thamani ya mwanaume na kujua kuwa pesa kamwe haimfanyi mwanamke kuwa mwanaume, niko mwenyewe na wanangu, kazi sina nimenunua Kitabu chako cha Biashara ili angalau nacho kinisaidie kuanza biashara kwani hiki cha ndoa yangu nimesoma nikiwa nimechelewa, ningekisoma mapema ningekua na adamu kwa mume wangu.
 
Mkuu kuna mazito kuliko hiyo C&P. Uliwahi kuisikia stori ya Kafulila na mtaraka wake Jesca Kishoa kina Katelephone. Atakuja kujuta huyu dada siku ubunge ukiisha

Privilege aliyonayo kafulila ni kubwa Sana .

Kama huyo mke wake alimuacha kisa pesa basi alifanya mistake kubwa Sana .

Hiyo code kuhusu "Katelephone" unamaanisha yule mzee wa kuweka Bkack katika Nywele ndo anaishi hapo? Na amehusika kinamna Fulani?
 
Chai, sema hujui kuweka viungo vizuri, kama sio iliki nadhani tangawizi imepitiliza
 
FB_IMG_17352966683031593.jpg
 
Back
Top Bottom