Nilimlingana BWANA kwa maombi ya Tabesi, naye akasikia kilio changu, akanitajirisha

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,230
13,989
Sukuzaliwa kwenye familia ya kitajiri, wala familia yetu haikuwa fukara. Baba yangu alikuwa ni mhandisi wa mitambo, na mama yangu alikuwa ni katibu mukhtasi ofisi ya mkuu wa mkoa.

Nilisoma hadi cha sita, sikutaka kuendelea na chuo licha ya kwamba nilipata ufaulu wa daraja la pili, wengi waliniona ni mwehu au kichàa.

Niliingia mtaani kuanza kutafuta pesa. Nilijaribu kilimo na ufugaji, nilijaribu biashara za minadani na pia nilifungua duka la rejareja .

Mwaka 2016 TRA walikuja dukani wakitaka niwaonyeshe mahesabu yangu na malipo yangu ya kodi. Nilifanya hivyo, wakayapitia na wakaniambia eti wananidai 275,000,000/-

Wakaweka kufuli lao wakasema hadi nilipe hiyo pesa ambayo kwa walati huo hata sikuwa nimewahi kuishika.

Benki nilikuwa na mkopo wa 50 milioni, ambapo niliweka rehani nyumba yangu. Biashara ikafa na nyumba ikapiga mnada.

Nililia sana, nikaona kulia hakusaidii kitu, nikaona nifunge na kuomba. Nikafunga siku tatu nzima, usiku na mchana bila kula wala kunywa, nilimuomba Mungu awe kiongozi wangu, anipe biashara na anitajirishe, pia anipe watu sahihi wa kufanya nao biashara.

Mungu alijibu kilio changu, nilipata jamaa kutoka Shelisheli wanataka mpunga kwa wingi. Wakaniamini, wakanipa milioni 100 niwakusanyie mpunga. Niliifanya kazi kwa uaminifu mkubwa. Kazi ilipoisha walinipa hela nzuri na huo ukawa ndio mwanzo wangu kushika mamilioni ya fedha.

Mpaka sasa kwangu hayo mambo yamekuwa ni ya kawaida sana.

Hakika ukimuomba Mungu kwa imani, na ukiamini kwamba anaweza kukubadilishia maisha yako hakika atafanya.

Ila kaa ukijua, kadiri unavyofanikiwa ndivyo idadi ya maadui invyoongezeka, na vita kubwakubwa zinainuka kila siku.
 
Mademu wa JF mnapenda sana kujidhalilisha aisee. Kuna mwingine kila siku ananisakama inbox, mara ananipenda mara ni mpe hela, ukimpa kesho anakuomba tena, yaani haridhiki.

Sasa leo akija, namuomba anipe expansion gap, kama ya askari wa Zanzibar. Yule aliyemshangaza Mshana Jr
jaman mie nimefanya utani honestly sjamaanisha kabisa, pole kwa yaliyokusibu
 
Sukuzaliwa kwenye familia ya kitajiri, wala familia yetu haikuwa fukara. Baba yangu alikuwa ni mhandisi wa mitambo, na mama yangu alikuwa ni katibu mukhtasi ofisi ya mkuu wa mkoa.

Nilisoma hadi cha sita, sikutaka kuendelea na chuo licha ya kwamba nilipata ufaulu wa daraja la pili, wengi waliniona ni mwehu au kichàa.

Niliingia mtaani kuanza kutafuta pesa. Nilijaribu kilimo na ufugaji, nilijaribu biashara za minadani na pia nilifungua duka la rejareja .

Mwaka 2016 TRA walikuja dukani wakitaka niwaonyeshe mahesabu yangu na malipo yangu ya kodi. Nilifanya hivyo, wakayapitia na wakaniambia eti wananidai 275,000,000/-

Wakaweka kufuli lao wakasema hadi nilipe hiyo pesa ambayo kwa walati huo hata sikuwa nimewahi kuishika.

Benki nilikuwa na mkopo wa 50 milioni, ambapo niliweka rehani nyumba yangu. Biashara ikafa na nyumba ikapiga mnada.

Nililia sana, nikaona kulia hakusaidii kitu, nikaona nifunge na kuomba. Nikafunga siku tatu nzima, usiku na mchana bila kula wala kunywa, nilimuomba Mungu awe kiongozi wangu, anipe biashara na anitajirishe, pia anipe watu sahihi wa kufanya nao biashara.

Mungu alijibu kilio changu, nilipata jamaa kutoka Shelisheli wanataka mpunga kwa wingi. Wakaniamini, wakanipa milioni 100 niwakusanyie mpunga. Niliifanya kazi kwa uaminifu mkubwa. Kazi ilipoisha walinipa hela nzuri na huo ukawa ndio mwanzo wangu kushika mamilioni ya fedha.

Mpaka sasa kwangu hayo mambo yamekuwa ni ya kawaida sana.

Hakika ukimuomba Mungu kwa imani, na ukiamini kwamba anaweza kukubadilishia maisha yako hakika atafanya.

Ila kaa ukijua, kadiri unavyofanikiwa ndivyo idadi ya maadui invyoongezeka, na vita kubwakubwa zinainuka kila siku.
Safi sana na hongera sana!!!

Positive energy uneileta humu
 
Back
Top Bottom