Niite bazinkulu
JF-Expert Member
- Nov 19, 2022
- 1,326
- 3,210
Kwa hapa nilipo nashukuru, nimefanya kazi ya kupika na kuuza chakula hapa mjini kwa miaka 10 sasa tangu mume wangu alipoamua kuniacha na kuoa mwanamke mwingine.
Mume wangu aliponiacha nilipitia hali ngumu ya maisha haswa kulipa kodi, kuwapatia watoto chakula, kuwavalisha na huduma nyingi ambazo wanastahiri kupata.
Sikuwa na kazi yoyote muda huo nilikuwa mama wa nyumbani tu, elimu yangu ni darasa la saba, hivyo mume wangu aliniacha akijua nitahangaika ila Mungu amtupi mja wake siku zote.
Nilianza tafuta kazi ili watoto wangu wapate vitu muhimu, hatimaye nikapata kazi ya House girl.
Kazi hiyo nilikuwa nalipwa Tsh30,000 kwa mwezi japo chakula na malazi nilikuwa napewa ila nilikuwa nimepewa mashart makubwa sana na miongoni mwao nilitakiwa kutoka nje baada ya miezi mitatu kwa ajili ya kwenda kuwaona watoto wangu.
Kutokana na hali nilikuwa nayo nilikubali kisha nikaanza kufanyakazi, nilikutana na changamoto na mitihani mikubwa sana kutoka kwa mke wa Bosi wangu ila nilijitahidi sana kwa sababu nilijua kila kazi ina changamoto zake, hivyo sikuwa na budi kuvumilia.
Baada ya miezi mitatu tangu nianze kufanya kazi nilipata habari kuwa mtoto wangu mdogo mwenye umri wa miaka mitano anaumwa.
Nilivyopata habari hizo nilimuomba ruhusa Boss wangu wa kiume akaniruhusu ila mke wake alikataa kabisa na kuniambia kuwa mkataba wangu unasema naruhusiwa kutoka nje baada ya miezi mitatu.
Ilinibidi nivumilie tu, kila baada ya wiki jirani yangu alinipigia simu kuwa mtoto hali yake inazidi kuwa mbaya, sikuwa na jinsi zaidi ya kufunga vitu vyangu kisha kuomba kuondoka.
Mke wa Boss wangu alikubali kuwa kama nimeamua kuondoka hamna shida na mkataba unasema; "Mfanyakazi akivunja mkataba halipwi pesa yoyote", hivyo nilitoka bila chochote zaidi ya matusi nyuma yakinifata.
Nilipofika nyumbani nilimchukua mtoto wangu na kumpeleka hospitali kisha akapata huduma, mtoto alipopona nilikuwa sina nafasi ya kurudi tena kazini nilipokuwa, hivyo ilibidi nitafute kazi nyingine, ilibidi nitafute mtaji ili niweze kujiajiri mwenyewe.
Hatimaye nilipata mtaji niliokuwa nataka kisha nikaanzisha biashara ya kupika chakula na kuuza, mwanzo biashara ilikuwa poa il