Mimi Melki
Senior Member
- Mar 31, 2022
- 155
- 259
Habari wasomaji,
Nimekumbuka kisa cha nyuma kidogo, nimeamua kuki share na ninyi. Kabla ya yote naomba kutoa funzo, kamwe husiende mahali bila kuwa na pesa ya dharura mfukoni, huenda la kutokea likakutokea"
Katika pita pita zangu mitaa ya jioni nilipokuwa natoka kwenye interview sehemu, nilikutana na msichana barabarani. Nikaona isiwe haba, nikaamua kumsemesha walau nipate kampani kwa kuwa tulikuwa tunaelekea njia moja. Tulianza kwa kufahamiana majina na mahali kila mmoja anapoishi. Alisema anafanya kazi kwenye mgahawa, mie nilimwambia kwa sasa kuna issue naisikilizia! Kutokana na jinsi alivyokuwa anazungumza alionekana mwema na mwenye tabia nzuri tu (kimuonekano).
Wakati tukiendelea na safari yetu njiani, kiasi cha kama nusu saa tangu kuanza mazungumzo, nilijikuta nikiparamia sinia nne za karanga za kupima ambazo tayari zilikuwa zimeshakaangwa na hazikufungwa kwenye mifuko!
. Ingawa nilikula mwereka wa kutosha, aibu na maumivu, bado nilisindikizwa na sauti yenye hasira kali ya mama mwenye karanga "kiibo ndeshafwooo, haki ya nani andaa pesa! Sijatoka Moshi kuja kucheka cheka hapa" Nilihisi mwili umepigwa ganzi! Nilipotazama mbele yangu niliona watu wakitoka kwenye biashara zao ili kuziandika habari! Pia wapita njia walipiga breki miguu yao na kitega masikio yao kusikiliza ni kipi kilichojiri!
Wakati nikijaribu kuzuga kuwa pesa zangu mbona sizioni huku nikiivuta mifuko ya suruali yangu kwa nje kwa mduwao mkubwa, niligundua kuwa yule msichana niliekuwa nae ambae tumeongea mengi tayari kashaondoka, akiniachia fungu kubwa la aibu nilibebe mimi! Niliganda dakika kama mbili nimeduwaa nikiangalia chini!
Nilishtushwa na mkwido kwenye kola la shati langu huku nikiangazwa na macho makali na meupe! Ndipo nilipomuona yule msichana niliekuwa naye akitokea sehemu ya tukio huku akiwa amejifunika na mtandio aliokuwa nao akiuliza, kipi kimetokea mahali hapa? Duh! Nilimtazama mara mbili asioneshe hata kunifahamu (sio kwamba nilitaka anilipie, bali nilishangaa ni kwa nini aondoke kisha alejee kama asiyenifahamu!
Alimamusura baba mmoja alikuwa akikatisha mahali pale ndiye aliyenisaidia kulipa hilo deni, mola ambariki huko alipo! Niliondoka eneo lile la tukio, hata nilipofika mbele, nilihisi kama watu wanaujua mkasa! Make kila niliemwangalia usoni niliona kama vile ananicheka!
Nimependa tu ku share huu mkasa! Japo utaonekana kutokuwa na mantiki yoyote!