George Betram
JF-Expert Member
- Oct 10, 2015
- 4,536
- 6,053
Nilikuwa sijawahi kufanya manunuzi ya kitu mtandaoni, kwa mara ya kwanza tarehe 5/08/2024 nilifanya manunuzi ya miwani ya macho katika mtandao wa eBay, hii ni baada ya miwani yangu kupasuka.
Niliingia katika mtandao wa eBay, nikasearch aina ya miwani ninayoitaka, nilishangaa sana bei nilizoziona, kuna miwani ya macho inauzwa mpaka dollar 3 😂😂😂.
Nilichagua aina ya miwani inayonifaa, bei yake ilikuwa ni dollar 5, free international shipping.
Tarehe 18/09/2024 nilitumiwa sms kuwa mzigo wangu umefika posta ya wilaya niliyopo, hivyo natakiwa niende kuuchukua, jana tarehe 19/09/2024 nimeenda Posta kuchukua mzigo wangu, miwani nimeikuta iko vizuri, na prescription zangu zimefuatwa vyema kabisa.
Sasa kuna mama nilimkuta pale ofisini posta, ni mtoa huduma wa pale. Nilimuuliza maswali kadhaa kuhusu kuagiza vitu nje na gharama ambazo ninatakiwa kulipia pale Posta. Yule mama alinielekeza kuwa hii mizigo tunayoagiza nje huwa tunapewa tracking number, kama tracking number yako inaanza na herufi R, ina maana mzigo wako umetumwa kwa kutumia Registered tracking code, inamaana mzigo wako ukifika Posta utapigiwa simu ukauchukue na hautolipia kodi yoyote, utachukua mzigo wako bila malipo yoyote. Lakini akaniambia kuwa kama tracking number yako inaanza na herufi tofauti na R, mzigo wako ukifika Posta utalipia kiasi cha shilingi 3000. Hii 3000 unapewa control number kisha unafanya malipo, baada ya kukamilisha malipo unapewa mzigo wako.
Lakini nilimuuliza swali, vipi kama mzigo wangu ni mkubwa unavuka kilo 5, yule mama aliniambia package za aina hiyo huwa zinakuja na maelekezo kutoka makao makuu, ila kodi yake haizidi shilingi 10000, hivyo aliniambia niache uoga kama kuna kitu nataka kuagiza niagize tu.
Okay, sasa mimi nina swali wataalamu wa hizi mbanga. Ninawezaje kuagiza mzigo kwa dealer ambayo nina uhakika atanimba tracking number ambayo ni registered, yaani tracking number inayooanzia na herufi R?