Nilibatizwa kwa muda mrefu

Daktari wa Meno

JF-Expert Member
Sep 5, 2019
509
1,610
Najua hamjambo humu ndani, pia najua kila mmoja ana tahadhari kubwa kuhusu Corona hivyo naomba tuchukue tahadhari kubwa sana.

Kabla sijaanza kuelezea namna nilivyobatizwa kwa muda mrefu isivyo kawaida naomba viongozi wa humu wasije kufuta habari zangu au kuziunganisha popote pale kwani watakuwa wananionea na mimi sina akaunti nyingine zaidi ya hii.

Mwaka 2003 nikiwa na umri wa miaka 21 nilibatizwa ziwani nikiwa na waumini wengine ambao tulikubali kwa imani zetu tubatizwe, awali ya hapo nilikuwa nasali kwenye dhehebu tofauti na hili ambalo nilibatiziwa. Dhehebu langu la awali watu walikuwa wanabatizwa kwa kutumia vifaa vya kunawia mikono (Kibeseni kidogo na kikombe) na wabatizwaji walimwagiwa maji kichwani.

Nilihama dhehebu la kwanza baada ya shangazi yangu kuja nyumbani kunihubiria na nikakubali kuhama na kwenda kwenye dhehebu lake, baada ya miezi 6 alikuja mchungaji kutoka jimbo kuu na kuleta habari za ubatizo kwa waumini wapya ili tuwe waumini wa dhehebu lile kwa ubatizo pia. Wakati huo tabia zangu zilibadilika nikawa kijana mwenye kuimba muda wote kwaya na kuheshimu sana wakubwa kwa wadogo. Kijijini nikawa na historia nyingine na hata kule kwenye dhehebu langu la awali nikawa naonekana msaliti ila nikajua Mungu aliyeniita atanipa nguvu ya kushinda yale yote mabaya yatupwayo juu yangu.

Basi watu kijijini wakawa wanasema kuwa dhehebu lile linaua watu nisiende maana wanaenda kuniua, habari mbaya kuhusu lile dhehebu zikaenea sana nikawa nakata tamaa ila nguvu kutoka rohoni inaniambia simama na utembee utashinda dhidi ya waovu wako katika mabaya wanenayo juu yako. Nikawa naenda kanisani na tukaanza kupewa semina kuhusu ubatizo kisha mafunzo ya wiki mbili pia yakafuata kanisani pale.

Shangazi akawa ananisihi nibaki pale kanisani nisirudi kule kwa zamani nikasema sawa haina shida shangazi na hata nyumbani waliona mabadiliko yangu baada ya kujiunga na lile kanisa jipya, mafunzo ya ubatizo yakafika mwisho na tukawa na maandalizi ya kubatizwa siku ya Jumamosi ambayo ilikuwa tarehe 12 mwezi wa 4. Maandalizi yalifanyika nyumbani na kwa nguvu ya Roho Mtakatifu nikaweza kupata kitoweo kwa wageni baada ya kubatizwa.

Basi asubuhi ya tarehe 12 safari ya kuelekea ziwani ikaanza shangazi na ndugu wengine waliongozana na mimi na yule mchungaji kutoka jimbo kuu akiwepo, katika mwendo wa dakika 50 tukafika ziwani na ikaendeshwa pale ibada ya kuombea maji na usalama wetu eneo lile. Mchungaji akaomba eneo lile liwe salama kama kuna wadudu wa aina yoyote wasiweze kutudhuru, hapo alikuwa anasema kuhusu nyoka na mamba.

Nikaanza kuogopa maana kule ziwani kuna visa vya watu kuliwa na mamba na nikamuita shangazi nikamwambia mimi naogopa kwenda kubatiza huko kwenye maji, akanisisitiza eneo lile limezingirwa na nguvu ya Roho Mtakatifu hivyo nisiogope niingie zamu yangu ikifika, kwa kweli nilikuwa sina amani na nikaaona nilifanya maamuzi ya mapema sana kukubali kubatizwa ningesubiri hata mwaka upite.

Basi mchungaji kutoka jimboni akavaa mavazi meupe akaingia yeye kwanza kwenye maji akiwa na msaidizi wake na Biblia mkononi, akatembea kama hatua 5 nikaona anasimama na kunyenyua mguu mmoja huku anatazama chini, akasema pepo wa mauti na kujeruhi ushindwe huna mamlaka katika mwili huu.

Mmh!! uwoga wa kuingia majini ukawa mara mbili ya awali nikaita shangazi nikamwambia nataka kurudi nyumbani akasema hapana mwanangu utanitia aibu huyo pepo asikuondoe katika njia ya Mungu. Nikaheshimu tena shangazi kwa mara nyingine nikaanza kuomba kimoyomoyo nikiingia nisikutane na mamba au kiumbe mwingine mwenye madhara ndani ya maji mle.

Tukajipanga mstari na nikawa mtu wa pili kutoka mwisho, mchungaji akasema naomba tujipange kutoka na umri hivyo wakubwa watangulie, eeeh mbona nikajikuta nakuwa m-batizwaji wa pili maana nilikuwa na miaka 21 wengine watano waliobaki walikuwa wadogo kwangu, basi yule mtu wa kwanza akaitwa na mchungaji aingie majini alipofika akaanza kuomba baada ya muda nikaona anazamishwa majini, nilitamani niwe na miaka 9 wakati ule maana nilijua ukifika unamwagiwa maji kichwani bila kuzamishwa mwili mzima ndani ya maji,

yule jamaa akatoka anakohoa na kupiga chafya sana kumbe aliingiwa na maji wakati amezama, hofu ikawa maradufu nikasema ikiwe wewe bwana umeniita basi mikononi mwako naiweka roho yangu na nikaitwa Yakobo (ndilo jina la ubatizo nililotaka nitumie) nikaitika naam mtu wa Mungu sema nakusikiliza, akasema ingia kunako maji na upate kuzaliwa upya katika roho.

Nikaanza kukanyaga maji kwa umakini na uoga ukiwa umejaa kwenye miguu na macho yangu yakipepesa kila upande kuona kama usalama upo. Ndani ya hatua 6 nikaona maji yanacheza akili inasema huyu ni mamba ila roho ikasema songa mbele wewe ni mwana wa mfalme hakuna baya litafanikiwa juu yako.

Nikasimama sikuendelea kutembea, shangazi akaniambia kwa kilugha mwanangu nenda basi na mchungaji anasema njoo Yakobo uzaliwe upya, yule msaidizi wa mchungaji wa jimbo kuu akaja akanishika mkono na kutembea nami kuelekea kwa mchungaji, nikafika maji usawa wa tumbo maana nilikuwa mrefu kwa mchungaji basi akaniombea na kusema Yakobo uko tayari kuzaliwa mara ya pili?

Nikasema ndio mchungaji, basi akampa yule msaidizi wake Biblia ili sasa anizamishe majini, nilikuwa naogopa sana. Basi akaniambia fumba macho nikafumba na akanishika kichwa na bega sasa ananizamisha majini nikagoma kuzama, ananikandamiza nizame sizami naogopa sana.

Tukahangaishana sana mle ndani kama vile ugomvi wakati huo waumini wengine wanakemea shindwa pepo mimi nahangaika nisizame kwenye maji, ndani ya dakika 5 mchungaji akasema haleluya watu wa Bwana... Wakajibu amen.

Akauliza nani anamjua Yakobo? Shangazi akasema mimi hapa baba namjua. Basi shangazi akaja akaongea na mchungaji na kuniambia kwa kilugha kubali ubatizwe nikasema hapana naogopa kuzama majini, wakaniambia ili uzaliwe upya lazima mwili wote uzame majini ili kuonesha mwanzo mpya wa maisha ya kiroho. Shangazi akatoka nikaendelea kupambana na mchungaji ananizamisha sizami nikawa nakataa anakandamiza bega nakakamaa shingo akasema Yakobo sogea pembeni.

Nikasogea akaita wengine na wakabatizwa wote nikabaki mimi sasa, mchungaji wa kanisa letu akaingia ndani ya maji na yeye wakawa watatu sasa pamoja na yule msaidizi, Biblia ikatolewa nje sasa nikajua hapa nazamishwa bila diplomasia kati yangu na wao, akasema Yakobo sogea nikaenda akaniombea na akaanza kunigandamiza mabega nizame nikawa nagoma akaja yule msaidizi na mchungaji wetu sasa mmoja akakamata bega la kulia mwingine kushoto na mwingine kichwani, wakati huo waumini wanasema shindwa pepo, shindwa pepo nikaanza kugangamala nisizame ila nguvu ikawa kubwa nikazama ndani ya maji kwa sekunde kama 3 nikatoka nakohoa maana maji yaliingia kwenye pua.

Waumini nje ya maji wakasema amen, shangazi akasema kwa kilugha Asante sana kijana wangu umeniondolea hii aibu ningekuwa mgeni wa nani leo.

Nikatoka majini na tukaanza kurudi nyumbani na wageni wangu ili kula na kunywa.
 
Nilijua mwisho wa haka ka stori angetokea mamba halafu waumini mkatoka nduki huku mkiamini mmemuacha mchungaji anapambana kwa maombi na yule mamba mwenye hasira kali.

Lakin ile kuja kugeuka mnamuona mchungaji amekunja ile kanzu na anawapita kwa spidi kali sana ya 180 mkimuangalia mkononi hana hata ile biblia halafu anawapigia kelele kuwaambia......kila nafsi itaonja mauti lakini sio kwa njia ya kufa kibudu namna hii, kila mmoja aokoe nafsi yakeeeeeeee........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimecheka kifala sana aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui fundisho la andiko hili ni nn?
Maana sijauona uhiari wa mbatizwa

Shangazi anapata aibu gani?

Shiriki Sana kwenye ibada na matendo mema , hayo Mambo mengine ni ishara tu za utakaso, iwe maji mengi au machache takasa roho yako.
 
Dah niliendelea kusoma nikisubiri mamba aanzishe varangati lakini mpaka mwisho hamna mamba. Disappoimted.
 
Mtakuja kuliwa na mamba bure alafu mseme nimajaribu ya shetani.
Kwani bibilia imeelekeza wakristo wabatizwe vipi, nilazima maji mengi?.

Nakumbuka yesu wakati anapaambinguni sikuya mwisho wakati anawaaga wanafunziwake alielekeza kuhusu kubatiza akasema.

Enendeni ulimwenguni kote mkawafanye watu wote kuwa wanafunzi wangu,

"MKAWABATIZE KWA JINA LA BABA NALA MWANA NA LAROHO MTAKATIFU"

Hakuna sehemu iliyo elekeza jinsiya kubatiza zaidi ya maneno hayo aliyoyasema Yesu mwenyewe kwahiyo maji mengi,maji kidogo sio ishu.

Ingawa siodhambi kubatiza kwa maji mengi lakini siolazima kwenda kumjaribu MUNGU kwenye mamba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mmm
Najua hamjambo humu ndani, pia najua kila mmoja ana tahadhari kubwa kuhusu Corona hivyo naomba tuchukue tahadhari kubwa sana.

Kabla sijaanza kuelezea namna nilivyobatizwa kwa muda mrefu isivyo kawaida naomba viongozi wa humu wasije kufuta habari zangu au kuziunganisha popote pale kwani watakuwa wananionea na mimi sina akaunti nyingine zaidi ya hii.

Mwaka 2003 nikiwa na umri wa miaka 21 nilibatizwa ziwani nikiwa na waumini wengine ambao tulikubali kwa imani zetu tubatizwe, awali ya hapo nilikuwa nasali kwenye dhehebu tofauti na hili ambalo nilibatiziwa. Dhehebu langu la awali watu walikuwa wanabatizwa kwa kutumia vifaa vya kunawia mikono (Kibeseni kidogo na kikombe) na wabatizwaji walimwagiwa maji kichwani.

Nilihama dhehebu la kwanza baada ya shangazi yangu kuja nyumbani kunihubiria na nikakubali kuhama na kwenda kwenye dhehebu lake, baada ya miezi 6 alikuja mchungaji kutoka jimbo kuu na kuleta habari za ubatizo kwa waumini wapya ili tuwe waumini wa dhehebu lile kwa ubatizo pia. Wakati huo tabia zangu zilibadilika nikawa kijana mwenye kuimba muda wote kwaya na kuheshimu sana wakubwa kwa wadogo. Kijijini nikawa na historia nyingine na hata kule kwenye dhehebu langu la awali nikawa naonekana msaliti ila nikajua Mungu aliyeniita atanipa nguvu ya kushinda yale yote mabaya yatupwayo juu yangu.

Basi watu kijijini wakawa wanasema kuwa dhehebu lile linaua watu nisiende maana wanaenda kuniua, habari mbaya kuhusu lile dhehebu zikaenea sana nikawa nakata tamaa ila nguvu kutoka rohoni inaniambia simama na utembee utashinda dhidi ya waovu wako katika mabaya wanenayo juu yako. Nikawa naenda kanisani na tukaanza kupewa semina kuhusu ubatizo kisha mafunzo ya wiki mbili pia yakafuata kanisani pale.

Shangazi akawa ananisihi nibaki pale kanisani nisirudi kule kwa zamani nikasema sawa haina shida shangazi na hata nyumbani waliona mabadiliko yangu baada ya kujiunga na lile kanisa jipya, mafunzo ya ubatizo yakafika mwisho na tukawa na maandalizi ya kubatizwa siku ya Jumamosi ambayo ilikuwa tarehe 12 mwezi wa 4. Maandalizi yalifanyika nyumbani na kwa nguvu ya Roho Mtakatifu nikaweza kupata kitoweo kwa wageni baada ya kubatizwa.

Basi asubuhi ya tarehe 12 safari ya kuelekea ziwani ikaanza shangazi na ndugu wengine waliongozana na mimi na yule mchungaji kutoka jimbo kuu akiwepo, katika mwendo wa dakika 50 tukafika ziwani na ikaendeshwa pale ibada ya kuombea maji na usalama wetu eneo lile. Mchungaji akaomba eneo lile liwe salama kama kuna wadudu wa aina yoyote wasiweze kutudhuru, hapo alikuwa anasema kuhusu nyoka na mamba.

Nikaanza kuogopa maana kule ziwani kuna visa vya watu kuliwa na mamba na nikamuita shangazi nikamwambia mimi naogopa kwenda kubatiza huko kwenye maji, akanisisitiza eneo lile limezingirwa na nguvu ya Roho Mtakatifu hivyo nisiogope niingie zamu yangu ikifika, kwa kweli nilikuwa sina amani na nikaaona nilifanya maamuzi ya mapema sana kukubali kubatizwa ningesubiri hata mwaka upite.

Basi mchungaji kutoka jimboni akavaa mavazi meupe akaingia yeye kwanza kwenye maji akiwa na msaidizi wake na Biblia mkononi, akatembea kama hatua 5 nikaona anasimama na kunyenyua mguu mmoja huku anatazama chini, akasema pepo wa mauti na kujeruhi ushindwe huna mamlaka katika mwili huu.

Mmh!! uwoga wa kuingia majini ukawa mara mbili ya awali nikaita shangazi nikamwambia nataka kurudi nyumbani akasema hapana mwanangu utanitia aibu huyo pepo asikuondoe katika njia ya Mungu. Nikaheshimu tena shangazi kwa mara nyingine nikaanza kuomba kimoyomoyo nikiingia nisikutane na mamba au kiumbe mwingine mwenye madhara ndani ya maji mle.

Tukajipanga mstari na nikawa mtu wa pili kutoka mwisho, mchungaji akasema naomba tujipange kutoka na umri hivyo wakubwa watangulie, eeeh mbona nikajikuta nakuwa m-batizwaji wa pili maana nilikuwa na miaka 21 wengine watano waliobaki walikuwa wadogo kwangu, basi yule mtu wa kwanza akaitwa na mchungaji aingie majini alipofika akaanza kuomba baada ya muda nikaona anazamishwa majini, nilitamani niwe na miaka 9 wakati ule maana nilijua ukifika unamwagiwa maji kichwani bila kuzamishwa mwili mzima ndani ya maji,

yule jamaa akatoka anakohoa na kupiga chafya sana kumbe aliingiwa na maji wakati amezama, hofu ikawa maradufu nikasema ikiwe wewe bwana umeniita basi mikononi mwako naiweka roho yangu na nikaitwa Yakobo (ndilo jina la ubatizo nililotaka nitumie) nikaitika naam mtu wa Mungu sema nakusikiliza, akasema ingia kunako maji na upate kuzaliwa upya katika roho.

Nikaanza kukanyaga maji kwa umakini na uoga ukiwa umejaa kwenye miguu na macho yangu yakipepesa kila upande kuona kama usalama upo. Ndani ya hatua 6 nikaona maji yanacheza akili inasema huyu ni mamba ila roho ikasema songa mbele wewe ni mwana wa mfalme hakuna baya litafanikiwa juu yako.

Nikasimama sikuendelea kutembea, shangazi akaniambia kwa kilugha mwanangu nenda basi na mchungaji anasema njoo Yakobo uzaliwe upya, yule msaidizi wa mchungaji wa jimbo kuu akaja akanishika mkono na kutembea nami kuelekea kwa mchungaji, nikafika maji usawa wa tumbo maana nilikuwa mrefu kwa mchungaji basi akaniombea na kusema Yakobo uko tayari kuzaliwa mara ya pili?

Nikasema ndio mchungaji, basi akampa yule msaidizi wake Biblia ili sasa anizamishe majini, nilikuwa naogopa sana. Basi akaniambia fumba macho nikafumba na akanishika kichwa na bega sasa ananizamisha majini nikagoma kuzama, ananikandamiza nizame sizami naogopa sana.

Tukahangaishana sana mle ndani kama vile ugomvi wakati huo waumini wengine wanakemea shindwa pepo mimi nahangaika nisizame kwenye maji, ndani ya dakika 5 mchungaji akasema haleluya watu wa Bwana... Wakajibu amen.

Akauliza nani anamjua Yakobo? Shangazi akasema mimi hapa baba namjua. Basi shangazi akaja akaongea na mchungaji na kuniambia kwa kilugha kubali ubatizwe nikasema hapana naogopa kuzama majini, wakaniambia ili uzaliwe upya lazima mwili wote uzame majini ili kuonesha mwanzo mpya wa maisha ya kiroho. Shangazi akatoka nikaendelea kupambana na mchungaji ananizamisha sizami nikawa nakataa anakandamiza bega nakakamaa shingo akasema Yakobo sogea pembeni.

Nikasogea akaita wengine na wakabatizwa wote nikabaki mimi sasa, mchungaji wa kanisa letu akaingia ndani ya maji na yeye wakawa watatu sasa pamoja na yule msaidizi, Biblia ikatolewa nje sasa nikajua hapa nazamishwa bila diplomasia kati yangu na wao, akasema Yakobo sogea nikaenda akaniombea na akaanza kunigandamiza mabega nizame nikawa nagoma akaja yule msaidizi na mchungaji wetu sasa mmoja akakamata bega la kulia mwingine kushoto na mwingine kichwani, wakati huo waumini wanasema shindwa pepo, shindwa pepo nikaanza kugangamala nisizame ila nguvu ikawa kubwa nikazama ndani ya maji kwa sekunde kama 3 nikatoka nakohoa maana maji yaliingia kwenye pua.

Waumini nje ya maji wakasema amen, shangazi akasema kwa kilugha Asante sana kijana wangu umeniondolea hii aibu ningekuwa mgeni wa nani leo.

Nikatoka majini na tukaanza kurudi nyumbani na wageni wangu ili kula na kunywa.
mmm haya mambo
 
Nilitegemea ungekoswa koswa au ungeliwa kabisa na mamba.....huo ubatizo ni batili sababu we mwenyewe haukuwa na imani mpaka mchungaji akaweka Biblia pembeni ili wakuzamishe
 
Nilijua mwisho wa haka ka stori angetokea mamba halafu waumini mkatoka nduki huku mkiamini mmemuacha mchungaji anapambana kwa maombi na yule mamba mwenye hasira kali.

Lakin ile kuja kugeuka mnamuona mchungaji amekunja ile kanzu na anawapita kwa spidi kali sana ya 180 mkimuangalia mkononi hana hata ile biblia halafu anawapigia kelele kuwaambia......kila nafsi itaonja mauti lakini sio kwa njia ya kufa kibudu namna hii, kila mmoja aokoe nafsi yakeeeeeeee........

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenichekesha Sanaa
 
Sitori ya kitoto ata haicheeekesi umeisiwa matirio? Tulia uistake kutoa sitori kila mala utaisiwa uwe unaweka gepu wiki moka moja.
 
Back
Top Bottom